Changamoto za ujasiriamali katika Afrika zimesababisha ajira ionekane kuwa na usalama wa kipato zaidi ya njia nyinginezo, kwa sababu ya kuwa na uhakika wa kipato kila baada ya muda mfupi.
Kujitegemea ni mbinu mbadala na zenye tija pale mtu anapopata mpenyo. Kwa Afrika hasa Tanzania, waliopata mpenyo ni mmoja kati ya kumi. Wengi wanaishia kulipa Kodi, kula na kukimbizana na madeni, kwa sababu, mfumo wa uchumi si rafiki kwa wasio na ajira.
Taasisi za fedha zimeelekeza nguvu zao kwa wenye ajira kwa sababu ya uhakika wa marejesho ya mikopo. Wajasiriamali wanakutana na hofu ya taasisi za fedha kushindwa kurejesha mikopo, hivyo kuwekewa masharti magumu ambayo ni wachache sana wanaoweza kukidhi vigezo hivyo.
Kwa maana hiyo, pamoja na kuwa ajira si jambo la kujivunia sana, kwa kuwa huwezi kupata mtaji nje ya kukopa, Bado katika mazingira ya sasa, ajira imekuwa mhimili mkubwa na wa uhakika kuendesha maisha ya kila siku.