Tusipowakemea hawa wabunge wanaobeza elimu yetu na wasomi wetu, tutazalisha Taifa la hovyo kabisa

Tusipowakemea hawa wabunge wanaobeza elimu yetu na wasomi wetu, tutazalisha Taifa la hovyo kabisa

Habari wanabodi...

Nimekua mfatiliaji kidogo wa mijadala ya Bungeni hasa michango inayotolewa na wabunge mashuhuri wawili watatu hivi kuhusu Taifa na maendeleo yake Kiuchumi kisiasa na kiteknolojia.

Lengo la kuandika huu uzi sio kuwataja hao wabunge au kuwadhalilisha bali ni kuwakosoa ili kujenga Taifa bora Zaidi.

Mara zote katika michango yao, wabunge hawa wawili wamekua wakipinga sana ajenda ya usomi na wasomi wenyewe. Kwa haraka haraka wanaamini kabisa wasomi wetu ambao wapo katika sekta mbalimbali hakuna wanalolifanya kwa Kutumia elimu yao. Yaani kimsingi wanaamini mambo yataenda tu kienyeji bila elimu. Kifupi hawaamini kama elimu Ina msaada wowote katika kukuza chumi za nchi na ustawi wa wananchi wake.

Hawa watu ukiwafatilia kiundani ni watu waliofanikiwa kiuchumi kwa njia ambazo wao wanaamini hazikuhitaji elimu, sababu wao wameishia la saba. Hivyo wanaamini mtu yoyote sio lazima asome ili afanikiwe, kisa tu wao hawajasoma na wametoboa.

Tusipowadhibiti au kupinga hizi kauli zao za kibaguzi dhidi ya wasomi wetu, yamkini watoto au wajukuu zetu huko mbeleni wakipata hizi Hansard hawataona umuhimu wa kusoma, wataamini kama huyu "Joshua" alitoboa(ga) bila kusoma basi kumbe kuna short cut ya Maisha inawezekana.

TUWAKEMEE MARA MOJA.

Nawasilisha.
Elimu gani unayoisema?
Hii elimu ni mbinu ya wakoloni kutengeneza watumwa wa akili.
Hata wewe hapo ni mtumwa kwaniunawaza kudhibiti maoni ya wengine kwa kuwa huna hoja,we ni dhaifu na umebaki na cheti kwa ajili ya kutambia tu lakini huna lolote katika kuchangia uchumi wa nchi.
Ningekuwa Rais, wasomi wote ningefuta vyeti vyenu na kutoa elimi mpya ya kuwafanya muwe wabunifu na sio upuuzi tunaouona sasa.
 
Sijaona hoja Kali waliyotoa zaidi ya vioja.... Hakuna hoja hata moja ya kujenga nchi hapo.... Au ishu ya matiti kudondoka ndio umeona hoja Mkuu???

Nina wasiwasi watu wengi hawajui kazi ya bunge ni nini.... Sema tu na katiba yetu ya hovyo Sana.... Mbunge ilipaswa kwa Sasa aanzie form six angalau awe amepata mwanga kidogo.
Ndiyooooooo,kazi yake ndogo sana.
 
Wasomi wa bungeni ilibidi wawe mstari wa mbele kupinga hoja na udhalilishaji wa hao wasio wasomi.

Siku zote wasio wasomi huwa na chuki sana kwa wasomi afu hapo hapo hao std 7C nao wanaanza kujiita Dr 😂 😂
 
Hujui unaloongea wewe , nionyeshe ni nchi gani au taifa gani ambalo lina mfumo wa elimu au Mtaala unaomfundisha mtu kuwa enterpreneur .
Mtu kuwa mjasiriamali au mbunifu ni suala la mfumo wa nchi husika jinsi unavyotoa incentives na means za watu kuwa wabunifu na wajasiriamali .
Kuna mfano mtu katoa huko juu
Leo hii unagraduate WA doctors of medicine , Engineering nk , unafikiri huyu mtu atadevelop service au product ipi kwa sector yake bila kuwa na startup capital kubwa ya kueleweka na miundombinu ya kufanikisha hilo ?
Au unafikiri hao madogo wanaodevelop hizo software programs mpaka zinaingia sokoni na kuanza kugenerate income ni out of nowhere kama fairy tales unazoandika humu ,kwamba dogo kadevelop software Tu ya kushare mziki peer to peer kwenye dormitory halafu paap software ikawa consumed na millions of people na kuanza kuingiza pesa .

Unajua lolote kuhusu venture capital na miundombinu ya kusuport kazi za uvumbuzi na ubunifu mfano pale silicon valley , Marekani ?
Unajua capital and resources injection inayofanyika kule mpaka hizo software kuingizwa sokoni ?
Au unafikiri kazi za ubunifu na uvumbuzi ni kama biashara ya kuuza viazi Buguruni ?

Acha ujinga
Naamini wewe ni mmoja wa wasomi wetu, maana una behave just exactly the same
nimetoa mfano wa napster na dogo, lengo ilikuwa ni kukuonesha kuwa jinsi elimu inavyoweza kumfanyia mtu awe mbunifu na kujitegemea kama itafundishwa kwa mitaala mzuri, wewe umekuja na mijadala yako ya kutunga tunga ili ku accommodate idea zako binafsi. Eti America Kuna funds za software developments, huu uongo umetoa wapi? Napster yenyewe kwanza ilifungwa kwa kesi kibao maana ilikuwa ina violate music copyrights, halafu ndo useme ilikuwa funded na USA government?
Aliyetoa mfano wa medical graduate eti hawana capital ya kufungua hospitali naye yupo kwenye kifungo hicho hicho mnachohangaika wasomi wetu, hamna clue, ingekuwa elimu yetu ni nzuri mngekua mnaajirika kwenye mashirika ya kimataifa.
 
Mtu kama Warren Buffet ,Bill Gates , Bezos ,Musk nk ,wamezungukwa na teams za brilliant scholars Kwa fani mbalimbali katika miradi yao ,na hao ndio watendaji wa hiyo miradi .
Hao ndio washauri ,wasimamizi na wealth creators kwenye hizo kampuni na miradi na kuwafanya hao mabwana kuwa mabilionea na kuendelea kuwa mabilionea .

Leo hii unaweza ukamchukua kilaza pro max kama King Msukuma ,au Lusinde au Kishimba kuwa manager WA au CEO WA space X , Nvidia JP Morgan au mradi wowote wa bilionea na akauendesha na kusustain wealth generation kupitia huo mradi ?

Watu wapumbavu hawajiulizi hili swali ,wamekalia ku ponda elimu tu .
Hakuna anayeiponda elimu, ni vile wewe umeamua kupeleka mijadala kwenye angle hiyo.
Kinachojadiliwa ni ubora wa wasomi wetu kwenye kufanya maamuzi yenye tija kutokana na fani zao husika.
 
Njaa tu zinatusumbua na wengine uelewa mdogo unatakiwa ukiwa na elimu uwe superman ugundue vitu kwa miujiza, uwe na hela bila ajira tena bila kujali faculty uliosomea kila kitu watakiwa uwe unakielewa mfano umesomea ualimu lakini mambo za sheria, biashara, technology, elimu ya anga, engineer n.k vyote uwe unavielewa na uwe na pesa kuwazidi wasiosoma tofauti na hapo elimu haina maana
Msomi sio lazima avumbue kitu, reasoning yake tu kwenye kutatua chamgamoto ni sifa tosha.
Pale ubungo mataa pamesumbua foleni kwa miaka Mingi sana, Mchina alikuja kuweka roud about, aka maliza tatizo, na tuna wataalamu ila hawakuwa na hiyo clue.
 
Mkuu unachanganya siasa na elimu hivo ni vitu viwili tofauti kwenye siasa njano sio njano ni blue utawalalamikia wasomi sana kwa siasa zetu uchwara
 
Kama unajiona msomi na umesoma prove it Kwa matendo yako na fanya mambo ya maana, naona mnalazimisha kuheshimiwa Kwa sababu tuu mna degree, na kama umesoma unaogopa Nini wakikuita mtu wa hovyo, watu wanajua Mchele upi na pumba zipi, msilazimishe heshima msiyostahili, huyo msukuma hajasoma lakini anaongea mambo ya maana kuliko 90% ya wenye degree
 
Mkuu unachanganya siasa na elimu hivo ni vitu viwili tofauti kwenye siasa njano sio njano ni blue utawalalamikia wasomi sana kwa siasa zetu uchwara
Naelewa sana Siasa na wasomi hawachangamani, lakini naamini Msomi anatakiwa kuwa na mamlaka ya command kutokana na uelewa wake.
Ukishaona Msomi ana compromise integity kwa wanasiasa basi jua Msomi ndo mwenye shida, Akina msukuma huko bungeni wamesimamia kwenye udhaifu huo wa wasomi.
 
Tupe mfano msomi asiyekuwa na mamlaka wala nyenzo pesa anatakiwa afanyeje ili kuonesha uwezo wake ukiachana na wasomi walio kwenye siasa(ajira rasmi na vyeo vya kuteuliwa)
 
Tupe mfano msomi asiyekuwa na mamlaka wala nyenzo pesa anatakiwa afanyeje ili kuonesha uwezo wake ukiachana na wasomi walio kwenye siasa(ajira rasmi na vyeo vya kuteuliwa)
Ndani ya mfumo wa Elimu yetu hii ya kukariri siwezi kukupa mfano wa Msomi anayeweza kuonesha uwezo wa alichosoma ni wachache sana,
Ukishakuwa na elimu ya kukariri jua huwezi vumbua kitu naishia kwenye hiyo hiyo cycle.,
 
Kama unajiona msomi na umesoma prove it Kwa matendo yako na fanya mambo ya maana, naona mnalazimisha kuheshimiwa Kwa sababu tuu mna degree, na kama umesoma unaogopa Nini wakikuita mtu wa hovyo, watu wanajua Mchele upi na pumba zipi, msilazimishe heshima msiyostahili, huyo msukuma hajasoma lakini anaongea mambo ya maana kuliko 90% ya wenye degree
Mambo ya maana kama yapi mkuu fafanua, kuitwa msomi sio kuwa unajua kila kitu kuna area of specialization mtu aliesomea ualimu umahiri wake anaenda kuuonesha darasani akifundisha wanafunzi, aliesomea udoctor umahiri wake anaenda kuonesha akitibu wagonjwa mahospitalini

Hivyo hivyo aliesomea biashara ataonesha umahiri wake kwenye biasha, na mind u wasomi wengi wanaoacha kelele zinakuwa nyingi siku hizi ni walimu, doctors/nurses pamoja na watu wa human resources yaani watu waliosomea utawala sasa hao wataka usomi wao wakauoneshe kwenye biashara?

Sasa ukija kwenye siasa hao maprofesa wa kwenye siasa hata msiwaongelee kwasasabu siasa ni siasa tu ukiwa na akili siasa sio mahari pako waulize walioleta kujua kwenye uringo wa siasa wameishia wapi?

Hao wabunge kama wanaona elimu haina maana waambieni wakawatibu wagonjwa muhimbili kwa elimu zao za darasa la saba
 
Habari wanabodi...

Nimekua mfatiliaji kidogo wa mijadala ya Bungeni hasa michango inayotolewa na wabunge mashuhuri wawili watatu hivi kuhusu Taifa na maendeleo yake Kiuchumi kisiasa na kiteknolojia.

Lengo la kuandika huu uzi sio kuwataja hao wabunge au kuwadhalilisha bali ni kuwakosoa ili kujenga Taifa bora Zaidi.

Mara zote katika michango yao, wabunge hawa wawili wamekua wakipinga sana ajenda ya usomi na wasomi wenyewe. Kwa haraka haraka wanaamini kabisa wasomi wetu ambao wapo katika sekta mbalimbali hakuna wanalolifanya kwa Kutumia elimu yao. Yaani kimsingi wanaamini mambo yataenda tu kienyeji bila elimu. Kifupi hawaamini kama elimu Ina msaada wowote katika kukuza chumi za nchi na ustawi wa wananchi wake.

Hawa watu ukiwafatilia kiundani ni watu waliofanikiwa kiuchumi kwa njia ambazo wao wanaamini hazikuhitaji elimu, sababu wao wameishia la saba. Hivyo wanaamini mtu yoyote sio lazima asome ili afanikiwe, kisa tu wao hawajasoma na wametoboa.

Tusipowadhibiti au kupinga hizi kauli zao za kibaguzi dhidi ya wasomi wetu, yamkini watoto au wajukuu zetu huko mbeleni wakipata hizi Hansard hawataona umuhimu wa kusoma, wataamini kama huyu "Joshua" alitoboa(ga) bila kusoma basi kumbe kuna short cut ya Maisha inawezekana.

TUWAKEMEE MARA MOJA.

Nawasilisha.
Kishimba usimuweke humo yeye hana formal education lakini ameelimika ndio maana kwenye makampuni yake kaajiri walioenda shule
 
Ndani ya mfumo wa Elimu yetu hii ya kukariri siwezi kukupa mfano wa Msomi anayeweza kuonesha uwezo wa alichosoma ni wachache sana,
Ukishakuwa na elimu ya kukariri jua huwezi vumbua kitu naishia kwenye hiyo hiyo cycle.,
Sihitaji unitajie mtu, nipe mfano wa vitu vya maana vinavyotakiwa kufanywa na msomi aliesomea ualimu, udoctor, ukatibu tawala, ufamasia n.k ili aonekane kafanya kitu cha maana kama msomi
 
Sihitaji unitajie mtu, nipe mfano wa vitu vya maana vinavyotakiwa kufanywa na msomi aliesomea ualimu, udoctor, ukatibu tawala, ufamasia n.k ili aonekane kafanya kitu cha maana kama msomi
Fanyeni vumbuzi au consultatations kwenye fani mlizosomea, mbona vijana wa ufundi veta wanaingiza kwenye kujiajiri straight,
 
Back
Top Bottom