Tusipowakemea hawa wabunge wanaobeza elimu yetu na wasomi wetu, tutazalisha Taifa la hovyo kabisa

Tusipowakemea hawa wabunge wanaobeza elimu yetu na wasomi wetu, tutazalisha Taifa la hovyo kabisa

Ila japo hawajaenda shule wanajenga hoja nzuri sana kuliko aliyeenda shule. Wangebahatika kwenda shule wangetoboa kimataifa.
 
Katika huu ulimwengu tunaoishi leo hii , uchumi wa nchi tajiri umejengwa katika maarifa na elimu na si ukanjanja wa maliasili na upuuzi mwingine .
Ukitaka kufail kama nchi ,basi anza kuentertain upuuzi wa watu washenzi kudowngrade elimu .

Nchi kama China ,India ,Singapore , USA nk ,sehemu kubwa ya GDP Yao inatokana na brains na maarifa ya watu na elimu na si ukanjanja kanjanja wa kuwa chawa na kulamba watu makalio ili kuwa mbunge uchwara kilaza na kuanza kuponda umuhimu wa elimu .
Ni upumbavu sana Huu .
Serikali ya China na Marekani wanawekeza hundreds of billoins of USD Kwa mwaka katika brains ,elimu na maarifa ya watu na results zinaonekana mpaka sasa .
Au mnafikiri ni wajinga ?
Kuwekeza kwenye vitu kama research and development ni muhimu sana kwa sasa .
 
Mie nimesoma historia ya zwangendaba na lubalunda empire na hakuna nilipo apply, hovyo tu,

nilimeza kile kitabu cha advanced marth na lile likitabu la physics tulikuwa tunaliita abbott, yaani mwalimu aliandika swali namtajia hadi ukurasa wa jibu lilipo ka mwinjilisti wa kisabato,

Sasa ile story ya manenge na mandawa ilikuwa ya nini? Na stori za juma roza.

Ile research paper niliyogundua uhusiano wa rushwa na umasikini sijawahi hata kupewa tuzo. Kuna kiongozi aliwahi sema hajui kwanini sisi ni masikini, nikafanya research hadi nikagundua kwanini sisi ni masikini hadi leo namimi ni masikini.

Bora hizi digirii ziwe kama hati ya nyumba tuweze kuchukulia mkopo au kuwekwa dhamana mahakani nikiwa na kesi,
Mkuu hapa umekosea, lengo lawewe kusoma zwangendaba halikuwa kuwa uwe tajiri kupitia history ya zwangendaba hapana ila lengo ni wewe uijue historia ya nchi yako kama wanavyofanya mataifa makubwa kutunza iconic wao walioleta michango yao kwenye taifa

Ila ili kuendeleza utamaduni wa kutunza historia ya nchi, mataifa yameweka utaratibu wa kuifundisha vizazi na vizazi kupitia schools na matamasha mbalimbali na makumbusho ya nchi

Pia wakaweka utaratibu wa ku employ walimu, archaeologist na wachunguzi mbalimbali ili kujua ya zamani zaidi kwa ajili ya kuyaenzi pamoja na utalii angalia mfano wa Egypt pyramid n.k

Shida kubwa ni wewe umesoma ukiwa masikini ukitarajia ukimaliza uwe tajiri kupitia kusoma kwako hivyo ulikuwa unapingana na malengo ya history na ulichofundishwa

Taifa linatakiwa liwawezeshe wananchi wake watokane na umasikini kabla ya elimu. Yaani uwe unasoma huku ukiwa na mrungula sio usome kupata mrungula
 
Tatizo elimu yetu, iko kimagharibi sana, hatuna elimu ya kiuhalisia wa kiafrika? yani elimu ya asili, yetu africa? elimu inamtego wa kiutumwa kwa ajili mataifa ya ulaya magharibi, uchina walikuja na mfumo wao, wa elimu asilia, umepiga hatua kubwa sana, nchi za kiafrica ziko nyuma sana, kwa kuendekeza, elimu ya mfumo wa kikoloni.
Naungana nawewe lakini kuna upande ukifikiria ukisoma elimu inayohusu wewe mtanzania tu hususani hii ya formal schooling utakuta kuna fursa nyingi sana tutakosa kimataifa kwakuwa wagunduzi wa hii dunia ni wazungu waafrica tunagundua tunguli tu za kurogana ukifundishwa izo ni sawa ila sio sawasawa
 
Bandari tumefeli kuendesha, Gas ya Mtwara mikataba haieleweki, kwenye madini ndo hakueleweki kabisa.

Mtu msomi wa PhD anaweza akaamka akafuta matokeo ya Uchaguzi mkuu au akaamua kuufuta upinzani.

Kwa kweli katika kaelimu kadogo nilichonacho ila nakubaliana na hao wabunge wanaowabeza wasomi ndani ya Taifa hili.
Tatizo wengi wenu mnachanganya elimu na siasa kitu ambacho si sahihi

Mwanasiasa hata asome vipi atabaki kuwa mwanasiasa. Siasa ni taasisi ya uwongo uwongo inayopingana na ukweli(hasa ukipata fursa aka kitengo)
 
Mimi nimesoma nimefika chuo -Ila wasomi wa Tanzania kwa kiwango kikubwa wapo nyuma Elimu haijawasaidia .

Fatilia vizuri wasomi wetu utagundua hilo jambo.

Wachache uno waona wapo smart ni wale ambao walitumia muda wao na gharama kujitafutia maarifa nje ya mtaala rasmi. Kama kusoma Sana vitabu n.k

MTU msomi hata kiingereza hajui, MTU msomi anatukana matusi , MTU msomi mwizi anaiba pesa za walipa kodi ,MTU msomi mzinzi. Anabeti ,mlevi


Hapa Tanzania hamna wasomi Kama wasomi
Mkuu unazungumzia usomi au unzinzi? Hebu kuwa specific

Kuna watu wazinzi na wachafu kama wamagharibi na ndio waliokuletea elimu ambayo wao wanaitumia kuiongoza dunia kwa ugunduzi wao
 
Fatilia vyema hoja za Hawa jamaa.... Utagundua wanawaponda wasomi na usomi kwa ujumla kwa kua wao wametoboa kwa njia zao bila kusoma.... Fikiria nje ya box
Mkuu, kwanza fahamu kuwa kuna tofauti ya kusoma na kuelimika,wengi wa hawa wanaoitwa/wanaojiita wasomi,hawajaelimika [hawa ndiyo wanaosemwa],wapo serikalini na nje pia na ipo mifano mingi hai inayothibitisha na kudhihirisha ukweli huko.
Tuache ukweli usemwe ili wakujifunza wajifunze na vilaza wabadilike.
 
Mkuu, kwanza fahamu kuwa kuna tofauti ya kusoma na kuelimika,wengi wa hawa wanaoitwa/wanaojiita wasomi,hawajaelimika [hawa ndiyo wanaosemwa],wapo serikalini na nje pia na ipo mifano mingi hai inayothibitisha na kudhihirisha ukweli huko.
Tuache ukweli usemwe ili wakujifunza wajifunze na vilaza wabadilike.
Nakuelewa Sana... Ila approach yao ni unacceptable... Wana shusha hadhi ya elimu yetu kama Haina maana vile.
 
Back
Top Bottom