Tusisahau: Ili uwe mwenyekiti wa CCM ni lazima kwanza uwe ni Rais wa JMT!

Tusisahau: Ili uwe mwenyekiti wa CCM ni lazima kwanza uwe ni Rais wa JMT!

Hata kama rais atakuwa Mbowe wa Chadema mwaka 2025?
Mzee wa sonona. Piga U turn maisha yaendelee mkuu. Huo ndiyo ukweli kuwa enzi za jamaa yenu zimefutika ghafla!
 
Hata kama haijaandikwa popote huo ndio ukweli wenyewe kwamba Rais wa JMT ndiye anakuwa mwenyekiti wa CCM.

Na Rais wa Zanzibar anakuwa makamu wa mwenyekiti.

Ramadhan kareem!
Hio iko sawa utaratibu ufuatwe, sio kubadãilisha kwa kuangaliana sura, Mama achukue nafasa Yake hilo ndio jawabu
 
Bila kubadilisha katiba hakuna mpinzani anaweza kutangazwa Rais hata kama amepata kura nyingi.

Kaisome sheria ya vyama vingi utagundua CCM haifananishwi kabisa na vyama vya upinzani, kwa kifupi CCM ni chama dola!
Unaota kukiwa na time huru ya uchaguzi utajificha wapi? Unajua kuwa Lisu alishinda?
 
Mama atapita kwa kura nyingi.


Nakuja kuvuruga kabisa mipango michafu ya kumnyima mama Yetu Uenyekiti wa Chama.

Jambo la kufanya kwa wajumbe ni moja tu.
Kupanga Seating Plan Vizuri kabisa Wajumbe wote wajulikane walipokaa na namba za Viti vyao.
Mfano Wajumbe wako 1800 basi itabidi pawe na vitambulisho vyenye Namba kuanzia moja mpaka 1800. Na viti viwe na namba hizo hizo kisha kila mjumbe akae kwenye Kiti chake kwa namba zake.
Wakati wa kugawa Karatasa kupigikura basi zigawanywe kwa mtiririko huo huo kuanzia namba moja mpaka 1800. Wakati wa kukusanya karatasi zikusanywe kwa mtiririko huo huo. Mkusanyaji awe ni mtu maalumu wa kuweza kubaini nani alikaa wapi na akikua na karatasi iliyogawanywa kwa mtiriko wa namba ngapi.

Hii itasaidia kuwabaini wasaliti wanaotaka kuvuruga AMANI yetu,UMOJA wetu na MSHIKAMANO wetu alianza kuuonyesha mama Samia Suluhu.
Kura tunataka tuone ni kura zisizo na rangi ya ukabila wala ukanda wala udini.
Kura zote kwa mama Samia. Hii nchi ni yetu wote.

Kazi nzuri na ya halali inaendelea.
 
Hata kama haijaandikwa popote huo ndio ukweli wenyewe kwamba Rais wa JMT ndiye anakuwa mwenyekiti wa CCM.

Na Rais wa Zanzibar anakuwa makamu wa mwenyekiti.

Ramadhan kareem!
CCM hawajaweza kujipambanua na serikali ya JMT! Tunahitaji mapinduzi ili hili kundi liondoke.
 
Hata kama haijaandikwa popote huo ndio ukweli wenyewe kwamba Rais wa JMT ndiye anakuwa mwenyekiti wa CCM.

Na Rais wa Zanzibar anakuwa makamu wa mwenyekiti.

Ramadhan kareem!
Ni wakati muafaka wa kubadili mazoea hayo. Haya mazoea yanaakisi umwinyi, ufalme na ubwenyenye kwa kiongozi husika. Ni muhimu kugawana madaraka.
 
Back
Top Bottom