Tusisahau: Mateso, Kifo na Mateso ya Tundu Antipas Mughwai Lissu

Tusisahau: Mateso, Kifo na Mateso ya Tundu Antipas Mughwai Lissu

Masoco Africa

Member
Joined
Feb 24, 2025
Posts
22
Reaction score
23
Habari za Wakati huu;
Kwanza nianze kwa kusema tu kwamba kwa wale ambao jana walisahau basi jana ilikuwa ni Siku muhimu sana kwa historia ya nchi yetu.Kwa mujibu wa Taarifa za kihistoria Jana tarehe 7 ya mwezi wa Tisa ya mwaka 2017 ilikuwa ni siku ambayo kwa mara ya kwanza Mbunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alishambuliwa kwa Risasi wakati akiendelea na shughuli za Bunge Jijini Dodoma.

Nafahamu hata Jamii Forum Africa imeingizwa kwenye kipindi cha Mateso na kimsingi sasa huku Jamii forum pia kuna aina ya watu watakuwa hawapo humu so sitarajii kabisa watu wenye IQ ndogo kuwepo humu maana sidhani kama wanajua kwamba kutumia "Intellectual Property" kuingia mtandaoni kwa ajili ya kuchangia uzi wa kula tunda kwa masihara ni matumizi mabaya ya VPN

Katika hostoria ya Siasa za nchi yetu Shambulizi lile ndilo Pekee ambalo mpaka leo bado halijaweza kupatiwa ufumbuzi.Polisi ambao tulitarajia wawe wameshamaliza kesi hii ndio ambao wanatuambia kwamba huwa wanafanya DORIA mitandaoni kiasi cha kuweza kumfungulia TUNDU LISSU kesi ya UGAIDI,Mtu ambaye alifanyiwa UGAIDI halisi mwaka 2017 leo hii anashtakiwa kwa kufanya ugaidi wa maneno Ama kweli ukistaajabu ya MUSA utayaona ya Polisi Tanzania.

Katika Tanzania,Taifa lenye watu milioni 60+ kuna watu wasiojulikana.Watu hawa wasiojulikana wanateka,watu,wanaua watu,wanashambulia watu tena kwa Risasi za MOTO na hawajulikana lakini mtu kama TUNDU Lissu ambaye anajulikana na maneno yake yanajulikana na historia yake inajulikana leo hii anashitakiwa kwa kosa la UHAINI,

Leo Tarehe 8 September Kesi ya Tundu Lissu sasa inaanza kusikilizwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania.Kwa Watanzania wenye akili wanafahamu kabisa kwamba Leo mahakama kuu itakuwa na Wajibu mmoja tu nao ni wa kumuachia Huru Tundu Lissu for "Lack of Merits" Kimsingi aina ya ushahidi na aina ya mashahidi ambao Polisi wanataka kutumia katika Ushahidi dhidi ya Lissu ni wa kubumba.Aina hio ya Ushahidi inaweza kutumika katika kesi ya Ubakaji jinai nyingine ambapo mtoto wa chini ya miaka 18 ambaye kimsingi hana Criminal Consent anaweza kusema alishawishiwa na Mtu mzima ila mtu mzima mwenye akili timamu huwa anakuwa na Criminal Consent na alipaswa awe mahakamani kama mshtakiwa pamoja na TUNDU LISSU.

Kwa mujibu huu ina maana kwamba Jeshi la POLISI liltakiwa likamate angalau nusu ya RAIA wa TANZANIA na kuwafungulia kesi Pamoja na TUNDU Lissu kwa Sababu wote hao ni Coconspirators wa Lissu kwa Mujibu wa Sheria zetu.

Sasa niishauri tu mahakama yetu.Najua mmeshapewa maelekezo kutoka Juu ila nyie ni wanaume."There is nothing for the Judges to fear Except Fear itself" So Mkishapanda kwenye ili Meza yenu ya Juu ya Hukumu Just Dismis the madness,Do not entertain that Kind of case maana ni kushusha heshima ya Mahakama zetu.Warudisheni wakajipange upya walete kesi ambayo kweli itaweza kuijenga mahakama na kuijenga Jamii.

Tunafahamu kwamba Jeshi la Polisi limeshakosa weledi na Aibu katika kujifedheheshesha mbele ya umma.Wanafanya kazi nzuri sana katika kupambana na uhalifu(Petty Crime) ila sasa yanapokuja masuala serious wanathibitisha ile kauli ya aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani ambaye mtoto wake alikuwa na Tabia ya kuchimba polisi Mkwara aliposema kwamba Wanachukua Polisi "Waliofeli" kwa sababu waliofaulu hawawezi kukubali kupokea maelekezo ya kijinga.Binafsi siamini kwamba Kufeli masomo maana yake ni ujinga na kupoteza Utashi.Wapo Polisi wengi ambao ni very smart na ambao wanafanya kazi nzuri ila nafikiri kuna Polisi ambao wanachafua Taswira tu ya Jeshi na huenda hao ni sehemu ya wasiojulikana.

Kimsingi leo niiambie tu Mahakama Chini ya Mzee wetu CJ Masaju. wasipokee maelekezo kutoka juu kama ambavyo nimekutana na Clip yako sehemu fulani ukiwanasihi watumishi wa mahakama kusimamia haki.Basi nakuomba katika Kesi hii ya TUNDU Lissu leo mnaweza kabisa kuidismiss for LACK of MERITS wala msipoteze muda wa RAIA na Mahakama katika kusikiliza hao watu Wasiojulikana.


Ninawatakieni kazi njema Tuendelee kuilinda na Kuitetea Tanzania.
 
Rostam alishawaelezea vizuri hawa majajiccm. Policcm Sina haja ya kuwataja Hilo ni TAWI la ibilisi hapa Tanzania.
 
Katika hostoria ya Siasa za nchi yetu Shambulizi lile ndilo Pekee ambalo mpaka leo bado halijaweza kupatiwa ufumbuzi.Polisi ambao tulitarajia wawe wameshamaliza kesi hii ndio ambao wanatuambia kwamba huwa wanafanya DORIA mitandaoni kiasi cha kuweza kumfungulia TUNDU LISSU kesi ya UGAIDI,Mtu ambaye alifanyiwa UGAIDI halisi mwaka 2017 leo hii anashtakiwa kwa kufanya ugaidi wa maneno Ama kweli ukistaajabu ya MUSA utayaona ya Polisi Tanzania.
Mkuu Lisu amepewa kesi ya uhaini, siyo ugaidi.
 
Kimsingi leo niiambie tu Mahakama Chini ya Mzee wetu CJ Masaju. wasipokee maelekezo kutoka juu kama ambavyo nimekutana na Clip yako sehemu fulani ukiwanasihi watumishi wa mahakama kusimamia haki.

Wameshazoea kula "nyama za watu" hao...
 
Back
Top Bottom