FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Kwa umri wangu, Kingereza nimeweza kukifahamu vizuri sana kuliko Watanzania wengi, kwa sababu kuu mbili:
1. Nimekulia na kusoma Tanganyika na Tanzania, lugha ya kwanza ya kuanza kusomeshewa ilikuwa ni Kiarabu kwenye madrasa, nilipoanza shule (school) lugha ya kwanza ya kusomeshewa ikawa ni Kingereza, masomo yote tulifundishwa kwa Kingereza kasoro somo la Kiswahili na dini tu, kwa Waislam, lugha ya kusomeshewa dini shule ilikuwa ni Kiswahili, ingawa tulikuwa na vipindi viwili vya kusoma dini katika juma zima.
Waliosoma Dar., watamkumbuka Mwalimu wetu wa somo la Dini ya Kiislam kwenye shule nyingi, za mjini Dar, maana alikuwa akitoka moja anakwenda nyingine kusomesha kipindi cheke, alikuwa akiitwa Maalim JanMohamad na alikua ni vigumu kumsahau kwani alikuwa na ulemavu wa miguu.
Mwalimu JanMohamad alikuwa na asili ya Zanzibar, aliongea Kiswahili na Kingereza vizuri sana, kiasi alikuwa akifundisha kwa lugha zote tatu katika somo lake la dini, Kiarabu, Kiswahili na Kingereza.
2. Nilipoingia utu uzima nikabahatika kuondoka Tanzania na kwenda kuishi nje ya Tanzania, kwa kusoma na kufanya kazi huko kwa miaka mingi sana, nikawa katika mji ambao Kingereza ndiyo ilikuwa lugha ya kwanza, nyingine ikiwa ni Kifaransa kwa apendae, hakikulazimishwa.
Pamoja na mengine, nikaendelea kujifunza na kufundishwa Kingereza miaka yote, hadi leo hii. Nikidhani kuwa Kingereza ni lugha bora duniani. Kwa bahati nzuri au mbaya, nilikuwa sipo sahihi kabisa baada ya kufahamu kuwa Kingereza ni lugha ya kubuni buni tu na haina uasilia.
Nimefikia tamati ya kusema kuwa tusikishobokee Kingereza, siyo lugha ya maana na inapoteza muda mwingi sana kukielewa na hata utapodhani umekielewa utajikuta hujakielewa kwa sababu ni lugha inayobadilika badilika mara kwa mara na pia haina uasili kwa hiyo ina maneno mengi sana ya kuazima kutokea lugha nzingine na kuyabadili badili kidogo ili yasikike kama "Kingereza".
Kingine ambacho hakuna katika Kingereza ni lafdhi ya asili, kila mtu anaeongea Kingereza kwa lafdhi yake na anatamka Kingereza tofauti na mwengine, haijalishi ni Muingereza au kama lugha mama kwake ni Kingereza, atakuwa na kasoro ya matamshi (phenetic) au wengine huita "accent", kwa sababu Kingereza hakina uasili.
Kingine ni hiki cha maneno ya Kingereza, neno lilelile moja linavyoandikwa lakini linatamkwa tofauti na lingine linapoongewa. Hili hakuna lisiye mchosha. Mfano neno chozi ni "tear" kwa Kingereza na hiyo hiyo "tear" pia ni chana. Neno "watch" linaweza kuwa kutazama, kulinda na wakati huo huo ni neno saa. Ndiyo, saa ya mkono ni "watch" kwa Kingereza.
Ndipo Watanzania wengi hufanya utani wa tafsiri ya Kingereza kwa Kiswahili, mfano wa haraka ni sambusa, "clockmosquitoclock". Saa imeshabadilika imekuwa "clock".
Kwa ufupi, tusishobokee Kingereza, kina athari kubwa sana ya kutujaza ujinga. Tukienzi na kukishobokea Kiswahili chetu, ni lugha tamu sana. Tena nasisitiza, serikali iwachane kabisa na mpango wa "Kiswahili sanifu", kwanini ukaisanifu lugha yenye asili? Naamini Kiswahili sanifu ni ujinga wawache kujaribu kukiondowa Kiswahili kwenye uarabu.
Kiswahili ni lugha tamu, historia inatuonesha hata kina Ibn Batuta, waliokuja miaka mingi kabla ya wazungu walikikuta Kiswahili kinaongewa na kuandikwa pwani ya mashariki ya Afrika.
Historia haijaishia hapo, inatuonesha kuwa hata kina Mkwawa. Kimweri, Abdul rauf Songea Mbane na machifu wengine wa bara walikuwa wanaongea na kuandika Kiswahili kwa kutumia herufi za Kiarabu, ambazo hazina shaka ndani yake, barua zao zipo kihistoria.
Mkoloni alipokuja, kama kawaida ili akutawale vizuri ni lazima akudunishe na ujione wewe si lolote si chochote, anaanza kukudunisha kwa lugha take mabayo kama hukuielewa unaonekaza siyo wa maana. Amefanikiwa sna kwenye hilo, mpaka imefikia wakati, tunakidharau Kiswahili chetu na kuona wa maana kati yetu ni yule mwenye kukijuwa Kingereza. Hatupo sahihi kabisa.
Tutakuwa wa maana zaidi tukikienzi Kisahili chetu na kukikuza kutpokana na asili yake na siyo kukisanifu, maana halisi ya neno sanifu, ni kukitania. Hivi kwanini mapoaka tufikie kukitania Kiswahili chetu?
Baraza la Kiswahili Tanzania linafanya kazi mbovu kabisa ya kukiharibu Kiswahili, kukitowa kwenye uasili wake na kukipeleka wapi sielewi.
Asili ya Kiswahili ni Pwani, tusijaribu kukisanifu na kukiondowa uhalisia wake kwa kudhani tu, Kiswahili nilugha ya Kiislam. Ujinga mwingine tuliojazwa na wazungu, mpaka imefikia kuna Watanzania hapa hapoa JF wanasema Kingereza ni "lugha ya kikatoliki" Ni ujinga huo.
Tuyaenzi matamshi na matamko ya Kiswahili, tena nashauri Kiswahili kifundishwe kwa herufi a Kiarabu mashuleni, hatutakosea, ndiyo asili yake.
Kujaribu kukiondowa Kiswahili na asili yake na lafdhi yake ya pwani ya mashariki ya Afrika ni kama kujaribu kuifanya bahari iwe dimbwi.
Nawasilisha.