Tusishobokee Kingereza, ni moja katika lugha mbovu duniani

Tusishobokee Kingereza, ni moja katika lugha mbovu duniani

Kiingereza ndio Engine ya biashara duniani kama USD tu..unaweza kuiponda hiyo lugha ukiwa unalima zako matikiti msata ila ukiwa mtu wa safari na kazi zako zinahitaji utoe maelezo huko unakokwenda utaelewa umuhimu wa Lugha ya Malkia..
 
Kwahiyo madam huko ulipoenda mlikuwa mnaongea kiswahili?? Kwann hukuona umuhimu wa kingireza hapo.
Kiingireza ni muhimu katika dunia ya Leo mana kiswahili hakivuki mipaka
 
Shida ni siku nchi inapata mtu wa hisia kama wewe kuongoza lazima Kila kitu kitaharibika
 
atakuwa na kasoro ya matamshi (phoenetic) au webgine huita "accent",kwa sabau Kingereza hakina uasili.

Lugha kubwa duniani zote zina lafudhi za kubadilika iwe Kifaransa, kiarabu, kispanyola, kiingereza, kiSwahili n.k

Lugha zote kubwa duniani ni muhimu sana ikiwemo Kiingereza.

Waliosoma enzi za Tanganyika, na baadaye Tanzania ya 1970s, 1980s wasitake kuwaambia vizazi vya sasa kuwa Kiingereza kibezwe na kuachwa.

Rwanda ilikuwa inaongea French hadi miaka ya 1990s lakini wamestuka na kukitilia mkazo kiingereza pia kwa kuelewa umuhimu wake katika dunia kijiji (globalisation)

Huku pia lugha yao mama kama kinyarwanda inatiliwa mkazo, bila kusahau pia kutokana na historia ya kiSwahili eneo la Afrika ya Mashariki na Maziwa Kuu lugha ya kiswahili inatumika .

Tanzania tuachane na dhana ya kupuuza umuhimu wa kujifunza na kufundishwa lugha za kigeni kama Kiingereza na pia kwa nyongeza kiarabu, kifaransa n.k ili kuweza kwenda na dunia hii ya kisasa.
 
Lugha kubwa duniani zote zina lafudhi za kubadilika iwe Kifaransa, kiarabu, kispanyola, kiingereza, kiSwahili n.k

Lugha zote kubwa duniani ni muhimu sana ikiwemo Kiingereza.

Waliosoma enzi za Tanganyika, na baadaye Tanzania ya 1970s, 1980s wasitake kuwaambia vizazi vya sasa kuwa Kiingereza kibezwe na kuachwa.

Rwanda ilikuwa inaongea French hadi miaka ya 1990s lakini wamestuka na kukitilia mkazo kiingereza pia kwa kuelewa umuhimu wake katika dunia kijiji (globalisation)

Huku pia lugha yao mama kama kinyarwanda inatiliwa mkazo, bila kusahau pia kutokana na historia ya kiSwahili eneo la Afrika ya Mashariki na Maziwa Kuu lugha ya kiswahili inatumika .

Tanzania tuachane na dhana ya kupuuza umuhimu wa kujifunza na kufundishwa lugha za kigeni kama Kiingereza na pia kwa nyongeza kiarabu, kifaransa n.k ili kuweza kwenda na dunia hii ya kisasa.
Siyo kweli.

Kingereza hakina asili.

Kiarabu hakibadiliki lafdhi yake, usichanganye lafdhi za watu na lafdhi ya lugha. Kiarabu kinavyoandikwa ndivyo kinavyotamkwa, popote utapo kuwepo.

Kiarabu tunafundishwa madrasa Tanzania ndicho kile kile anachofundishwa madrasa Mchina kwao China. Na hata tukienda kusali China au iwe umatumbini, Kiarabu kinabaki kuwa ni kile kile na lafdhi ile ile.

Kiswahili pia, kinabaki na lafdhi ile ile labda waje waliosomea ujimga kubadili mahari wakaiita mahali na mahali wakapaita mahari.

Kigereza ni tofauti kabisa, hakitamkwi kinavyoandikwa. Mfano inaandikwa "women" inatamkwa "wimen". Inaandikwa "laugh" inatamkwa "laf".

Upo hapo ulipo?
 
Wamarekani wenyewe unakuta wanajua Eng Spanish etc
Mbongo kakumbatia kiswahili tuu
Bongo jina kubwa lkn hamna kitu - Prof J
 
Wamarekani wenyewe unakuta wanajua Eng Spanish etc
Mbongo kakumbatia kiswahili tuu
Bongo jina kubwa lkn hamna kitu - Prof J
Wapo Wamarekani wenye asili ya Uhispania wengi tu.

Tanzania tunatakiwa tukumbatie Kiswahili, tusijidhalilishe na lugha ya kijinga, Kingereza. Inatudunisha kimawazo.
 
Kwa umri wangu, Kingereza nimeweza kukifahamu vizuri sana kuliko Watanzania wengi, kwa sababu kuu mbili:

Moja: nimekulia na kusoma Tanganyika na Tanzania, lugha ya kwanza ya kuanza kusomeshewa ilikuwa ni Kiarabu kwenye madrasa, nilipoanza shule (school) lugha ya kwanza ya kusomeshewa ikawa ni Kingereza, masomo yote tulifundishwa kwa Kingereza kasoro somo la Kiswahili na dini tu, kwa Waislam, lugha ya kusomeshewa dini shule ilikuwa ni Kiswahili, ingawa tulikuwa na vipindi viwili vya kusoma dini katika juma zima, waliosoma Dar., watamkumbuka Mwalimu wetu wa somo la Dini ya Kiislam kwenye shule nyingi, za mjini Dar, maana alikuwa akitoka moja anakwenda nyingine kusomesha kipindi cheke, alikuwa akiitwa Maalim JanMohamad na alikua ni vigumu kumsahau kwani alikuwa na ulemavu wa miguu.

Mwalimu JanMohamad alikuwa na asili ya Zanzibar, aliongea Kiswahili na Kingereza vizuri sana, kiasi alikuwa akifundisha kwa lugha zote tatu katika somo lake la dini, Kiarabu, Kiswahili na Kingereza.

Mbili: Nilipoingia utu uzima nikabahatika kuondoika Tanzania na kwenda kuishi nje ya Tanzania, kwa kusoima na kufanya kazi huko kwa miaka mingi sana, nikawa katika mji ambao Kingereza ndiyo ilikuwa lugha ya kwanza, nyingine ikiwa ni Kifaransa kwa apendae, hakikulazimishwa.

Pamoja na mengine, nikaendelea kujifunza na kufundishwa Kingereza miaka yote, hadi leo hii. Nikidhani kuwa Kingereza ni lugha bora duniani. Kwa bahati nzuri au mbaya, nilikuwa sipo sahihi kabisa baada ya kufahamu kuwa Kingereza ni lugha ya kubuni buni tu na haina uasilia.

Nimefikia tamati ya kuasema kuwa tusikixhobokee Kingereza, siyo lugha ya maana na inapoteza muda mwingi sana kukielewa na hata utapoidhani umekielewa utajikuta hujakielewa kwa sababu ni lugha inayobadilika badilika mara kwa mara na pia haina uasili kwa hiyo ina maneno mengi sana ya kuazima lgha nyingine na kuyabadili badili kidogo ili yawe la lafdhi au yasikike kama "Kingereza".

Kingine ambacho hakuna katika Kingereza nilafdhi ya asili, kila mtu anaeongea Kingereza anaongea kwa lafdhi yake na anatamka Kingereza tofauti na mwengine, haijalishi ni Muingereza au kama lugha mama kwake ni Kingereza, atakuwa na kasoro ya matamshi (phoenetic) au webgine huita "accent",kwa sabau Kingereza hakina uasili.

Kingine ni hiki cha maneno ya Kingereza, neno lilelile moja linavyoandikwa lakini linatamkwa tofauti na lingine linapoongewa. Hili hakuna silie mchosha. Mfano neo chozi ni "tear" kwa Kingereza na hiyo hiyo "tear" pia ni chana. Neno "watch" linaweza kuwa kutazama na wakati huo huo ni neno saa. Ndiyo, saa ya mkono ni "watch" kwa Kingereza.

Ndipo Watanzania wengi hufanya utani wa tafsiri ya Kingereza kwa Kiswahili, mfano wa haraka ni sambusa, "clockmosquitoclock".

Kwa ufupi, tusishobokee Kingereza, kina athari kubwa sana ya kutujaza ujinga. Tukienzi na kukishoibokea Kiswahili chetu, ni lugha tamu sana. Tena nasisitiza, serikali iwachane kabisa na mpango wa "Kiswahili sanifu", kwanini ukaisanifu lugha yenye asili? Naamini Kiswahili sanifu ni ujinga wawache kujaribu kukiondowa Kiswahili kwenye uarabu.

Kiswahili ni lugha tamu, historia inayuonesha hata kina Ibn Batuta, waliokuja miaka mingi kabla ya wazungu walikikuta Kiswahili kinaongewa na kuandikwa pwani ya mashariki ya Afrika.

Historia haijaishia hapo, inagtuonesha kuwa hata kina Mkwawa na machifu wengine wa bara walikuwa wanaongea na kuandika Kiswahili, barua zao zipo kihistoria.

Mkoloni alipokuja, kama kawaida ili akutawale vizuri ni lazima akudunishe na ujione wewe si lolote si chochote, anaanza kukudunisha kwa lugha take mabayo kama hukuielewa unaonekaza siyo wa maana. Amefanikiwa sna kwenye hilo, mpaka imefikia wakati, tunakidharau Kiswahili chetu na kuona wa maana kati yetu ni yule mwenye kukijuwa Kingereza. Hatupo sahihi kabisa.

Tutakuwa wa maana zaidi tukikienzi Kisahili chetu na kukikuza kutpokana na asili yake na siyo kukisanifu, maana halisi ya neno sanifu, ni kukitania. Hivi kwanini mapoaka tufikie kukitania Kiswahili chetu?

Baraza la Kiswahili Tanzania linafanya kazi mbovu kabisa ya kukiharibu Kiswahili, kukitowa kwenye uasili wake na kukipeleka wapi sielewi.

Asili ya Kiswahili ni pwani, tusijaribu kukisanifu na kukiondowa uhalisia wake kwa kudhani tu, Kiswahili nilugha ya Kiislam. Ujinga mwingine tuliojazwa na wazungu, mpaka imefikia kuna Watanzania hapa hapoa JF wanasema Kingereza ni "lugha ya kikatoliki" Ni ujinga huo.

Tuyaenzi matamshi na matamko ya Kiswahili, tena nashauri Kiswahili kifundishwe kwa herufi a Kiarabu mashuleni, hatutakosea, ndiyo asili yake.

Kujaribu kukiondowa Kiswahili na asili yake na lafdhi yake ya pwani ya mashariki ya Afrika ni kama kujaribu kuifanya bahari iwe dimbwi.

Nawasilisha.
wewe unakijua, unataka wengine wasikijue
acha roho mbaya kama ya mtume
 
Yamekuingia.

Hunipati kwa Kingereza, Kiswahili, Kiarabu. Na lugha zingine mbili tatu nazielewa kijujuu.

Kwa ubobevu wangu wa lugha, nimefikia tamati, Kingereza ni lugha mbovu katika zote nilizozitaja.

Hi ni namba tofauti kijana. Usilolijuwa ni usiku wa kiza.
Sizitaki mbichi hizi....Sungura akajisemea!
 
Wapo Wamarekani wenye asili ya soain wengi tu.

Tanzania tunatakiwa tukumbatie Kiswahili, tusijidhalilishe na lugha ya kijinga, Kingereza. Inatudunisha kimawazo.
Labda kwa ambae anataka kuishia tandale
 
Siyo kweli.
Modern Standard Arabic (MSA) is a modernized form of Classical Arabic, the language of prayer and recitation throughout the Islamic world. Standard Arabic is the language of literature and education in most Arabic countries. Educated people throughout North Africa and the Arabian Peninsula have good to excellent command of Standard Arabic besides their native Arabic dialect. It is estimated that some 165,000,000 people throughout the Islamic world have some knowledge of Standard Arabic. Standard Arabic is not acquired as a mother tongue, but rather it is learned as a second language at school and through exposure to formal broadcast programs (such as the daily news), religious practice, and print media. The media in which Standard Arabic is not as frequently used as the spoken Arabic dialects are in song, film, and the theater.

1723468436087.png

 
Back
Top Bottom