Tusishobokee Kingereza, ni moja katika lugha mbovu duniani

Tusishobokee Kingereza, ni moja katika lugha mbovu duniani

yote uliyoandika bi mdashi ni kweli lakini hatuna jinsi maana ukitaka kupata maarifa mapya lazima

utumie kiingereza ukitaka kwenda nje ya nchi pia kama hujui lugha ya nchi husika lazima utumie hiyo lugha

sasa unaweza toa njia mbadala kuhusu hayo yote???
Mwenzio anaipigia chapuo lugha ya ahera!
 
Hizo herufi za kubuni tu hazina asili ya maandiko yoyote.
Mbona Kiswahili kilichotimia hakijabuni hizo herufi kama Kiingereza?
Mfano hili neno linaanza na Q "quarter". Unalitanmka kota. Uwe Muingereza au mndengereko. Kwanini lisiwe kota tu hata kwa Kingereza?
Sio kweli inatamkwa hivi ˈkwȯ(r)-tər
Neno lenye x "sox" unalitamka "soks
Sio kweli huu ni uongo.

Neno sahihi ni socks. Inatamkwa /sɒks
". Hizo herufi ulizoweka zote ni wao kujifanya kuwa wana ubora zaidi kwa kujitofautisha,
Umehama kwenye mada kabisa baada ya kushindwa kuonyesha maneno ya kiswahili yenye herufi X au Q .

Umehamia kusema waingereza "wanajifanya"
Elewa kuwa, bila "Alif Be Te" usingekuwa na alphabet.
hazina maana yoyote.
Zingekuwa hazina maana wewe ungeweza kusoma na kumjibu mtu akikuuliza saa ngapi kwa kiiingereza??

Mfano mimi uniulize in a formal way 2:15 ni saa ngapi nitajibu it's quarter past two ambayo ni very basic kwenye usomaji muda sasa bila Q huo umaana ungetokea wapi?
Unafahamu "alif be te" zinapatikana wapi?
Umehama mada kama kawaida turudi kwenye mada kuu kabla hatujahamia kwenye lugha ya kiarabu

Maana mada iliyopo mezani ni ubora wa Kiswahili juu ya Kiingereza na si Kiarabu kama unavyotaka kuhamisha mada.
 
Yamekuingia.

Hunipati kwa Kingereza, Kiswahili, Kiarabu. Na lugha zingine mbili tatu nazielewa kijujuu.

Kwa ubobevu wangu wa lugha, nimefikia tamati, Kingereza ni lugha mbovu katika zote nilizozitaja.

Hi ni namba tofauti kijana. Usilolijuwa ni usiku wa kiza.
Kiingereza ni lahaja kama ilivyo kwa kiswahili.Msingi wake mkubwa ni kilatini kama ilivyo kwa kiswahili ambacho msingi wake mkubwa ni kiarabu
 
Mbona Kiswahili kilichotimia hakijabuni hizo herufi kama Kiingereza?

Sio kweli inatamkwa hivi ˈkwȯ(r)-tər

Sio kweli huu ni uongo.

Neno sahihi ni socks. Inatamkwa /sɒks

Umehama kwenye mada kabisa baada ya kushindwa kuonyesha maneno ya kiswahili yenye herufi X au Q .

Umehamia kusema waingereza "wanajifanya"


Zingekuwa hazina maana wewe ungeweza kusoma na kumjibu mtu akikuuliza saa ngapi kwa kiiingereza??

Mfano mimi uniulize in a formal way 2:15 ni saa ngapi nitajibu it's quarter past two ambayo ni very basic kwenye usomaji muda sasa bila Q huo umaana ungetokea wapi?

Umehama mada kama kawaida turudi kwenye mada kuu kabla hatujahamia kwenye lugha ya kiarabu

Maana mada iliyopo mezani ni ubora wa Kiswahili juu ya Kiingereza na si Kiarabu kama unavyotaka kuhamisha mada.
Wewe vyovyote utakavyosema ni sama, kwa ufupi, hizo ni herufi za kujitungia tu Waingereza. X imetokana namba ya Kirumi. Ambalo na wao walilitoa kws wafoneshia (Phoenecians). Hiyo Q hata wasomi wanajiuliza ipo kwa sababu gani na haitumiki. Wengine wanasema ipo kwa ajili ya kutofautisha tu maandishi lakini haitamkiki, hata uipambe vipi.

Umehakikisha mwenyewe, hata upambe vipi.

Kingereza kisingepata alphabet bila alif be te.

Kumbuka hilo.
 
Lugha mbovu kivipi, heshimuni lugha za watu
 
Siyo kweli.

Kingereza hakina asili.

Kiarabu hakibadiliki lafdhi yake, usichanganye lafdhi za watu na lafdhi ya lugha. Kiarabu kinavyoandikwa ndivyo kinavyotamkwa, popote utapo kuwepo.

Kiarabu tunafundishwa madrasa Tanzania ndicho kile kile anachofundishwa madrasa Mchina kwao China. Na hata tukienda kusali China au iwe umatumbini, Kiarabu kinabaki kuwa ni kile kile na lafdhi ile ile.

Kiswahili pia, kinabaki na lafdhi ile ile labda waje waliosomea ujimga kubadili mahari wakaiita mahali na mahali wakapaita mahari.

Kigereza ni tofauti kabisa, hakitamkwi kinavyoandikwa. Mfano inaandikwa "women" inatamkwa "wimen". Inaandikwa "laugh" inatamkwa "laf".

Upo hapo ulipo?
Kwa hiyo unapendekeza tushobokee kiarabu?
 
Wewe vyovyote utakavyosema ni sama, kwa ufupi, hizo ni herufi z kujitungia tu Waingereza.
Mimi sijasema popote tu kama kujitungia, bali nilihitaji ushahidi wa huo utoshelevu wa lugha ya kiswahili dhidi ya kiingereza na nimekuuliza herufi mbili tu.

Na utaje maneno ya kiswahili yenye herufi X na Q unabaki kusema yaliyopo kwa kiingereza wamejitungia mbona waliotunga kiswahili hawakutunga pia kama kutunga ni rahisi ?
Umehakikisha mwenyewe, hata upambe vipi.
Wapi nimepamba , onyesha pambo hilo.
Kingereza kisingepata alphabet bila alif be te.
Leta ushahidi.
Kumbuka hilo.
 
Two things can be true at the same time:

Mosi, Tukienzi na kukithamni Kiswahili. Hapa TZ inafeli sana kwenye makuzi na ustawi wa hii lugha.

Pili, Tujifunze kingereza na lugha zingine. Dunia ya leo bila kingereza hutoboi asikudanganye mtu. Jifunze Kingereza na lugha zingine za kimataifa zinazozungumzwa na watu wengi duniani.

Kutojua kingereza tayari umepishana na maarifa mengi sana duniani. Machapisho karibu yote yanaandikwa kwa kingereza kwanza na mengi yanabaki katika lugha hiyo bila kutafsiriwa.

Kiswahili na Kingereza ni muhimu.
 
Kwa mtu anayependa kujifunza mambo mapya, ni muhimu kujua Lugha ya kingereza kwani Mambo mengi mazuri yapo katika Lugha hiyo.

Kwa hiyo ukitaka uwe update au sasishwa au wa kileo, lazima ujue kiingereza?
 
Kiswahili chako cha kipemba ni tofauti na cha bara pia,

Unajuwa-unajua
Chukuwa-chukua
Ushanifahamu-umenielewa
Ushanisoma-umenielewa
 
Back
Top Bottom