Tusishobokee Kingereza, ni moja katika lugha mbovu duniani

neno 'sabato" lenyewe ni Kisaswahili "saba" linatokana na Kiarabu "sabt".

Kumbuka hilo.
Siyo shabbat ya kihebrania?
Nimegundua unawadanganya sana raia humu kwa kuupa kipaumbele waarabu.Huko misikitini kwenu kusema uongo si dhambi?
 
Kuhusu neno watch kuwa na maana tofauti mbona hata kiswahili yapo yana maana zaidi ya moja kama vile barabara, paa, ndege, kiboko n.k
 
Kweli?Nafanyia kazi.
 
Mwenzio anaipigia chapuo lugha ya ahera!
Kiarabu na Kiswahili zinaweza kuwa ndiyo lugha za awali za Kimataifa duniani kuliko zingine.

Kingereza ni lugha ngeni kwenye hii ardhi yetu, kilipata mwanya baada kuondolewa Mjerumani.
 
Kiarabu na Kiswahili zinawez kuwa ndiyo lugha za awali za Kimataifa duniani kuliko zingine.

Kingereza ni lugha ngeni kwenye hii ardhi yetu, kilipata mwanya baada kuondolewa Mjerumani.
Unaelewa maana ya lahaja?
 
Mkuu uko sahihi! Changamoto tuliyonayo Waafrika ni inferiority complex zinazotokana na ukoloni.
Tunaaamini ili mtu uhesabike ni msomi ni lazima ujue kiingereza!
 
faiza
 

MKAE KUJIDANGANYA HUKO HUKO . HAKUNA LUGHA MAARUFU NA KUBWA KAMA HII. MKISHINDWA KIINGEREZA MNA. KIPONDA.
 
Siku utakayo acha udini ndo utajua ni jinsi gani akili yako ilikua imelala
 
Au dialect kwa lugha yenye lahaja ya kilatini?
Kwa hiyo umeshindwa kulielezea Kiswahili?

Lahaja ni neno linalotokana na Kiarabu, ni matamshi au ndimi, lafdhi.

Lakini nzuri zaidi ni ndimi, "ndimi za watu wa mvita ni tofauti na za watu wa mzizima lakini wanaelewana".
 
MKAE KUJIDANGANYA HUKO HUKO . HAKUNA LUGHA MAARUFU NA KUBWA KAMA HII. MKISHINDWA KIINGEREZA MNA. KIPONDA.
Unaweza kunishinda Kiswahili lakini hutonishinda Kingereza na Kiarabu

Kiswahili, hususan cha kuandika nimeongeza ujuzi sana hapa JF.

Kiswahili nilikuwa nakiandika kwa herufi za Kiarabu ili Marehem bibi yangu kipenzi, asisomewe na mtu barua nilizokuwa namtumia.

Kumbuka hilo.
 
Unaweza nishinda Kiarabu lakini si
1. Kiswahili
2. Kiingereza na
3. Kijerumani

NA BADO NASISITIZA KIINGEREZA NI MUHIMU SANA DUNIANI.
 
Unaweza nishinda Kiarabu lakini si
1. Kiswahili
2. Kiingereza na
3. Kijerumani

NA BADO NASISITIZA KIINGEREZA NI MUHIMU SANA DUNIANI.
Siku hizi kuna AI, haibs umuhimu wowote. Kujidanganya tu.

Tunaweza kuongea yoyote wakati wowote.

Lugha yenye umuhimu kwa sasa ni Kiswahili, tena wa hali ya juu.
 
Reactions: Lax
Bi Faiza unazingua. Raia walikuwa wanasubiri maoni yako kuhusu bunge la Iraq kutunga sheria inayoruhusu mtoto wa miaka 9 kuolewa halafu unakuja na huu uzi uliojaa akili mgando..!!! Yote uliyoandika YANATAKIWA KUPUUZWA NA YEYOTE MWENYE AKILI TIMAMU.
 
Niliwahi kufundishwa na profesa mmoja chuo kikuu akisema kuwa Lugha mama ndio msingi wa maarifa .hata ukitaka kuwa na wanasayansi Bora , Wana historia na wabobevu wa Kila fani ukimfundisha mtu kwa Lugha yake aliyozaliwa nayo anakuwa Bora zaidi .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…