Tusishobokee Kingereza, ni moja katika lugha mbovu duniani

Ukiona mtu anakidisqualify kiingereza jua hakijui kinamsumbua Sana!! Na hili tatizo wanali watanzania wengi
 
Niliwahi kufundishwa na profesa mmoja chuo kikuu akisema kuwa Lugha mama ndio msingi wa maarifa .hata ukitaka kuwa na wanasayansi Bora , Wana historia na wabobevu wa Kila fani ukimfundisha mtu kwa Lugha yake aliyozaliwa nayo anakuwa Bora zaidi .
Kitendo cha kuponda english kwa ulimwengu wa sasa, na hasa kwa taifa kama hili la kwetu ni utani
 
Ukiona mtu anakidisqualify kiingereza jua hakijui kinamsumbua Sana!! Na hili tatizo wanali watanzania wengi
Kasome upya post namba moja. Hakuna "qualification" wala 'disqualification" ni mawazo yako tu.
 
Sasa inatofauti gan na kiswahili. Maana kiswahili cha kiunguja na kimvita ni tofauti baadhi ya maneno. Na maeneo pia. Mfano mswahili wa tz na wa lamu pale Kenya ni tofauti na hata Congo DRC ni tofauti. Huu ujinga mnawadanganya watu matokeo watu wanakosa kazi nyingi kisa hajui kiingereza. Na ukifuatilia wanaohimiza watu wasisome kiingereza ni vibabu na vibibi anbavyo vimetumia muda wao wote wa maisha kukitumia baada ya kufanikiwa ndio vinakuja na hiz stor
 
Usipojua kingereza utakachokijua kwa ufasaha ni KUZAGAMUANA tu
 
Hapo mwisho uliposema tufundishwe Kiswahili kwa kiarabu ndio umehatibu kabsa...
Sasa itakua kiswahili au kiarabu? Na tofauti na kingereza chenye kutohoa maneno mengi ni nini?

Lengo la uzi ni kuwa tubadili kiswahili kuwa kiarabu...

Jifunze lugha zote kiswahili, kingereza , kiarabu, kifaransa, kihispaniola n.k...
 
Ulipoharibu nikufunganisha kiswahili na kiarabu
 
Huna unachojua katika lugha ya kiarabu wewe wacha kudanganya watu foolish
 
Hizi jitihada unazofanya kuvutia watu kwenye uarabu, ungezielekeza kwenye kuhamasisha uafrika wako ungetia fora.

Hata lugha yetu ya Kiswahili unasema ni ya kiislamu?
Mara ifundishwe kwa kiarabu, mara isisanifiwe..! Kwanini ?
We bibi bora uhamie Afghanistan huko ukaenjoy maisha ya uislamu vizuri.
 
Huna unachojua katika lugha ya kiarabu wewe wacha kudanganya watu foolish
Kwani kuna mashindano hapa? Lugha za maudhi zinahusu nini? Au mjadala wa kiheshima umekushinda?

Punguwani wahed.
 
Hebu andika hayo yote kwa Kiingereza bila kutumia ChatGPT…

Au kama vipi mimi na wewe tufanye mdahalo kwa kutumia lugha ya Kiingereza ambayo wewe unajigamba kuifahamu vizuri sana kuliko Watanzania wengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…