Tusisifie sana shule za private zinafanya vizuri

Tusisifie sana shule za private zinafanya vizuri

Kachumbi

Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
70
Reaction score
30
Mimi ni mdau wa elimu ambaye naguswa sana na usimamizi mbovu wa mitihani ya mwisho ya elimu ya sekondari. Shule nyingi za private zipo kiabiashara zaidi, hazipo tiyari kuona wazazi wanalipa ada kubwa watoto wao wanafeli,huwa wanalazimika kufanya namna yeyote kuhakikisha namba kubwa ya wanafunzi inapata matokeo mazuri.

Licha ya kuweka alama au wastani wa kufaulu ndani ya shule si kigezo tosha cha wao kuwa na matokeo mazuri, wengine wana wastani wa kawaida.Shule za private ni nyngi wenye hela wanaangalia ipi inafanya vizuri zaidi na baadhi ya wazazi pesa si tatizo. wapo wanafunzi wengine wanabebwa katka wastani sababu ya nyazfa za wazazi wao na michango yao ktk shule huska.
Wanapateje matokeo mazuri?

Kwanza wanatoa rushwa sana kwa wazimamizi wa mitihani ya taifa,mathalani mwalmu wa serikal unakuta anapoke laki 3 kwenye mshahara wake, anapofka kituo cha usimamizi anapewa bahasha ya milion 1 nje ya malipo kawaida,alafu anaambiwa jitahd kusimamia vizuri.

Mitihani husoviwa nje na kuingizwa ndan ya chumba cha mitihan bila vikwazo sababu wahuska waliisha pewa chao,pia kwa kujzatiti uweka walnz njia zote za kuingilia magar ya wazmamiz wa mitihan na watoe taarfa manapohs gar hilo.

Pia utoa taarfa kwa maafisa elimu na wangne wanao huska kupeleka wasimamizi wanaoeleweka, pia nao hupewa chao mapema nakuambiana wawe makni.

Cha zaidi asilimia kubwa ya watoto wa maafsa mbalimbali na wenye hela usomea kwenye shule hizo, hakuna afisa anayeweza kukubali mtoto wake afeli iwapo analetewa mbinu mbadala za mtoto wake kufaulu.

Baadhi ya shule udiriki ata kutoa vtisho kwa wasimamizi iwapo wakkataa kutoa ushirikiano mathalan kuambiwa kuamishwa kwenye kituo hcho au atapewe kazi kusimamia tena.

Wengne uchangisha pesa kwa ajil ya kuwapa wasimamizi ili kazi iwe nyepesi, ndo maana wasimamizi wengi wa mitihani upendelea shule za private wakijua kuna chochote na upata uduma nzuri. Wakuu wengi wa shule za Serikali hawana mda huo, na usimamizi wake huwa umeimarika sawasawa.

Wadau si shule zote za private znafanya udanganyifu,baadhi wanafunzi wana uwezo kutosha,kwa hizi shule za wakubwa ndo mipango yao, kuna baadhi ya watoto vgogo ufeli kabisa sababu ya kuwa vilaza sana, Hata kucopy na ku paste hushindwa.

Zaman wakati wa usimamizi mzuri na shule za private hazikuwa nyingi kufanya kuwa za kibiashara zaidi, shule za serikali nyingi zilikuwa zinaongoza, mbali ya hiyo walikuwa wanachuwa nafasi za juu sana,sasa hivi umwone wapi?

Ilichangiwa kuwa ni viongozi wazuri, wazalendo na watiifu, pia walijua elimu nini,na kujua mtu anasitahili kupata kile kinachotakiwa.

Cha zaidi idara ya usalama wa taifa mbovu sana, tena nao wanachangia kushiriki katika maovu kwa kutoa taarifa kwa viongozi shule huska kipi kinaendelea. Hakamatwi mtu, labda inawezeka sababu siku hizi wanafamika kwa kila mtu,siri hamna.

HAYO NI YANGU WADAU,TOA MAWAZO YENU
 
Ahsante mdau wa elimu. Ulichoongea INAWEZEKANA kina ukweli kwa asilimia kubwa maana kuna watu nilisoma walitoka O'level hizo shule zinazoongoza. Kuja A'level ikawa tofauti sana.

Lakini pia ukiwa kama mdau wa Elimu jitahidi kuandika vizuri. Kuchanganya r nal, pa kuweka h,kukatisha sana maneno.....
 
Kisiki Chao kiko advance acha wafu wazikane.
 
Ahsante mdau wa elimu. Ulichoongea INAWEZEKANA kina ukweli kwa asilimia kubwa maana kuna watu nilisoma walitoka O'level hizo shule zinazoongoza. Kuja A'level ikawa tofauti sana.

Lakini pia ukiwa kama mdau wa Elimu jitahidi kuandika vizuri. Kuchanganya r nal, pa kuweka h,kukatisha sana maneno.....


Simuungi mkono mtoa mada ingawa anajiita mdau wa elimu, sijui mdau wa elimu kwenye lipi. Nitoe uzoefu wangu kdogo unaweza kuleta changamoto hata kwenye shule za serekali na pia unaweza kujibu mashaka ya niliyemnukuu.

Chukua shule zote za binafsi zinazofanya vizuri halafu fuatilia, mfano tuchukue 50 tu zinazofanya vizuri. Jamaa wako serious kweli, hawavumilii uvivu wala uzembe.

Mimi ni mzazi na bahati nzuri watoto wangu wamepita/wanapita katika eneo hili kwa hivyo nina mwanga kidogo ya kinachotokea.

Mfano matokeo haya yaliyotoka yamemuhusu mmoja wa watoto wangu, lakini wakati anarudi nyumbani likizo ya kuingia form 4 arudi analia, uhakika wa kuvuka ulikuwa mdogo. Ni mpaka pale alipoambiwa avuka na akatakiwa kubadili kombi.

Maana yangu ni hii wana wa-stretch vilivyo na kuwafanya wawe kwenye tension wakati wote, hapa si kupata matokeo mabaya mwisho bali ni jinsi gani atavuka darasa. Hii inawasaidia sana na wala si kuhonga kama wengi wanavyofikiri.

Wewe unataka kukimbia km 1500, kiwango cha ushiriki ni dak 4 ndio uweze kuvuzu kushiriki na wewe unajiwekea dak 4 hizo hizo. Sifikiri kama unania ya kufanya vizuri, jiwekee dak 2 na ukiweza kuifikia inakupa nafasi nzuri zaidi ya kufika dak4 za mashindano

Shule za serekali zitiwe moyo ili wawabane watoto kama wenzao wa private wanavyofanya uone kama heshima ya hizi shule haikurudi.

Si kweli kwamba hawa wanaakili zaidi, hapana. Ila wana msaada wa karibu, tena wanabanwa wafanye kilichowapeleka.

Shule za serekali kama mwenyewe hukujali hakuna wa kukusukuma, ndio maana wanapotoka private na kuingia gov hawaonyeshi tofauti yoyote kwa kuwa hakuna wa kuwasukuma.

Jibu la haya yote ni kuwamotivate waalimu gov waweze kuwasaidia watoto, maana waalimu ni hawa hawa wanakwenda private wanafanya maajabu.
 
Tokea lini shule za kata zikashindana na best private schools, Tuangalie hizo shule zenu zina mipango mikakati kweli ya kuwa na performance nzur au ndo siasa. Ww unayesifia a level za gvt. hujui km hawa wanafunzi wa private ndio wanaopata posts huko tena hizo mnazozita vipaji.
 
Kachumbi

Wewe sio mdau a elimu au kama ni mdau you are less knowledgeable on what you are trying to advance! I fail to comprehend kuwa shule kama St Francis, marian, Feza (zote) and the like zinaonga miaka yote tangu zianzishwe!!!!!!! Labda inawezekana
 
Last edited by a moderator:
Kisiki Chao kiko advance acha wafu wazikane.

Advance ipi hiyo...Mbona ni hizo hizo hata Advance zinaongozs......??? Marian haijawahi kutoka top 10 si Olevel au Advance toka siku ya kwanza ya kuanzishwa kwake....


Vyuoni ni balaa...Mimi nimesoma na dada mmoja wa Marian Muhimbili na mwisho alikuwa Best overall students.....

upo hapo mkuu
 
Mi nimesoma private school na mwaka niliomaliza tulikuwa wa tano kitaifa sikuwahi kuona mtihani ukiletwa umesoviwa.Asilimia zaidi ya 80 ya lile darasa tumesoma vyuo vya elimu ya juu na tumepata degree.

Hizo ni kauli za viongozi walioshindwa kusimamia shule za serikali wanatafuta uongo wa kuwafariji wazazi wa watoto wa shule za serikali
 
Wadau si shule zote zinafanyaja hujuma katika eneo la mtihani.Mapungufu ya shule za serikali yanafahamika.Zinaweza kuwa zinapata matokeo mazuri ambayo si sitahiki.Mjue kuna ata mbinu chafu huwa zinatumika kwa baadhi ya shule
 
Ahsante mdau wa elimu. Ulichoongea INAWEZEKANA kina ukweli kwa asilimia kubwa maana kuna watu nilisoma walitoka O'level hizo shule zinazoongoza. Kuja A'level ikawa tofauti sana.

Lakini pia ukiwa kama mdau wa Elimu jitahidi kuandika vizuri. Kuchanganya r nal, pa kuweka h,kukatisha sana maneno.....

kuna shule dar sitaji jina hao jamani wanatutia majaribuni unapewa bahasha 2mills uuze mechi msimamizi dah! halafu kujisifia sasa
NECTA ongezeni dau jamani ili tusiishawishike.
 
enzi za mwalimu private walienda kusoma waliofeli. ilikuwa aibu kusema unasoma private, lakini leo.....!
 
Aisee shule nyingi za private zinazofanya vizuri ni kwa sababu ya nidhamu ya hali ya juu ambayo inasimamiwa vizuri. Mtoto anafundishwa namna nzuri ya kutunza muda hivyo anajua ni muda upi wa kufanya kipi.

Muda wa kusoma ni kusoma kucheza ni kucheza kusali ni kusali pia . Hakuna loose time hadi muda wa kulala unalazimishwa kulala. Walimu wako committed na kazi yao kwa sababu tuh wanalipwa vizuri na ni lazima syllabus iishe kabla ya muda.

Kwa hiyo hakuna uchawi wala rushwa kwa baadhi ya shule wanastahili matokeo mazuri, japo kuna shule chache pia zinatoa rushwa sikatai hilo pia.
 
Da Pretty

Alichoandika ni ukweli mtupu. Ukitaka kuamini, hao hao wenye alama za juu wakifika Chuo Kikuu ni wa kawaida mno. Wanahenyeshwa na shule nzuri za kawaida za Serikali kama Kibaha, Tabora, Songea Kilakala et al wanapofika Chuo kikuu.

Lakini wakiwa Secondary shule hizo za Serikali huzidiwa maradufu! Kuna kitu naamini kiko chini ya kapeti.

Ni kweli kunakuwa na screening kubwa ili mwanafunzi abak shule kama Marian, FEZA, Abbey, St Francis et al,lakini inatia shaka kiukweli. Mbona wakifika Chuo kikuu ni wa kawaida tu? Kuna jambo kwa vyovyote!
 
Last edited by a moderator:
Naunga mkono hoja kuna michezo inachezwa shule za private, Ni kweli ufundishaji wa shule za private ni mzuri tofauti na shule za kata ila linapokuja swala la mitihani ya taifa kuna uchakachuaji unafanywa.

Simaanishi kwamba wanafunzi wa private wangefeli endapo kungekuwa hamna udanganyifu ila tungeshuhudia ufaulu wa kawaida tu kutoka shule hizi.

Mfano badala ya divisio I 90 na division III 10 tungeona div I 20 na div III 60 huu ndo ukweli na mzazi hata siku moja usitegemee mwanao atakwambia baba tumepewa mtihani ndio maana nimefaulu itabaki siri yake mwenyewe, akikwambia si utamwona kilaza.
 
wakati shule hizi za private zikifundisha shule zetu za kata watoto hawafundishwi, wakati shule hizi zikiwa na walimu wa kutosha, maabara na maktaba shule zetu za kata hazina hizo rasilimali halafu leo wanafaulisha tunasema wanahonga wasimamizi,

Hii sio haki lazima tukubali kuwa matokeo yao ni product ya huduma wanazotoa.
 
Jamani tuacheni majungu wala wivu. Naombeni tuwe wakweli tu, mwanafunzi bila discipline, hawezi kufaulu KAMWE. Discipline hapa simaanishi kumsalimia mwalimu anapoingia darasani, namaanisha vitu vingi sn kuanzia unapoamka, lifestyle yko, unainterract vipi na wenzako, etc.

Kiukweli, shule za private wameliweza hilo kwa asilimia KUBWA sana, mwisho wa siku ndo inapelekea kuwa na matokeo mazuri. Shule zetu za kata HAKUNA discipline kabisa. Ukichangia na mshahara mdogo wa walimu, hali ndo inakuwa mbaya kabisa.

Private schools walimu wnajenga mazingira rafiki na wanafunzi wao, ili iwe rahisi kwao kuwasaidia kielimu, wakati shule za kata, mwalimu na mwanafunzi ni MAADUI. Katika hali hiyo unategemea mwanafunzi akiwa na shida ya kusaidiwa itakuwaje wkt hawaelewani.?

Kijana wangu primary alikuw anasoma Muhimbili, alikuw haeleweki na kilaza hatari. Nikaamua kumuhamishia MARTIN LUTHER, Dodoma. Baada ya miezi kadhaa, alibadilika kupita maelezo na akawa anajua kupanga mambo yke na muda wake vizuri kbs, na darasani akawa yuko vizuri.

Akiwa likizo anajisomea kwa sababu anarudi nyumbani akiwa na homework ya likizo nzima, so hapati muda wa kupoteza hovyo. Sasa hivi yupo form two, St Peter Clever, na mwendo ni ule ule.

Tuacheni imani hizo potofu jamani. Wale watoto wakiwa shule ni kama wapo jeshini au jela, kila kitu kwa ratiba, kusoma, kucheza, kula, kulala etc. Shule za kata hawana muda huo, ni shida tupu. Jamaa wako smart bana...!!!

Private schools wanaenda kwa ratiba, na wanahakikisha mpaka muda fulani, walimu wanakuwa wamemaliza syllabus zao, watoto wanapewa mitihani mpaka wanakonda, na kila mtoto anatunza kwenye faili lake mitihani yake yote kwa ajili ya revision. Muulize mtoto wa shule za kata mtihani aliorudishiwa siku 3 zilizopita kama anao. Ameshautupa siku nyingi.

Kwa uwingi wa shule nzuri zinazofaulisha za private, huwezi kunishawishi kukubali mada yako kwamba WOTE hao kweli wanatoa rushwa. Unanikumbusha jamaa mmoja alikuwa anasema msanii Diamond anaenda sana kwa waganga ndo maana anafanikiwa na anakuwa na hela nyingi sana.

Nilimpa jibu dogo sana, nikamuuliza kwani wewe waganga huwaoni? Nenda na ww uwe tajiri. Mimi sio shabiki wa Diamond kabisa, ila naamini dogo yupo serious sana kwa kile anachokifanya ndo maana anafanikiwa.

Sent from my iPad using JamiiForums app
 
mdau amesema baadhi ya shule sio zote,alchosema mdau ni mkweli mtupu, mwalimu wangu wa cpa review class 2011 aliniambia kitu kama hiki tena tukiwa darasani anafundisha, yeye alisema mtoto wake amekutana na haya mambo akiogopa saana,ingiwa kwa matokea ya mwaka huu mi nafikiri yana uhalal/ ukweli saana
 
Back
Top Bottom