Tusiwasakame Yanik Bangala na Djuma Shabani kuwa ni watovu wa nidhamu, Je Feisal Salumu nae ni mtovu wa nidhamu??

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Jangwani Kuna tatizo! Jangwani Kuna tatizo! Jangwani Kuna tatizo!

Naandika Kama shabiki mkereketwa niliyechoshwa na kelele za wachezaji Tena wachezaji ambao ni mafundi haswaa wa mpira Nani asiyejua ubora wa Feisal Salumu alipokua Yanga Sc na ukienda pale msimbazi huwezi kukuta kiungo mkabaji na mwenye kucheza beki wa Kati Kama Yanick Bangala.

Naam watu wa mpira wameshanielewa Nini NALIA NGWENA naongea kuhusu talanta za Hawa wachezaji, kila nikikumbuka majalo ya Djuma Shabani pamoja na ufundi aliounesha kwenye mechi muhimu ya fainali ya kombe la shirikisho Yes! Hakika alikua bado anastahili kuwa Yanga sc.

UondoKaji wa Feisal Salumu ulileta maswali mengi sana na kuchangiwa na mzaha ndani yake "eti alichoka kula ugali na sukari"

Kwa jicho la pili na wenye akili walielewa Nini kinachoendelea jangwani lakini kwa kuwa Yanga sc ni timu kubwa na wenye mashabiki Lia Lia Basi Jambo lilifunikwa kishabiki zaidi na kesi juu ya Feisal salumu iliamuliwa ikulu.

Je asingefahamika ikulu Kama Denis nkane ama chrisprin Ngusi Nini kingeendelea juu ya talanta ya kijana mdogo (Zanzibar finest)??

Leo zimeibuka tetesi za utovu wa nidhamu za Yanick Bangala na Djuma Shabani kwa kuwa Yaniki bangala na Djuma Shabani bado wanacheza mpira huwezi kusikia wakifunguka juu ya hizo tuhuma Bali wanaacha zigo la miba/misumari liwaangukie ili maisha yaendelee na ndicho kilichotokea kwa Feisal Salumu alipohojiwa "Nini viongozi yanga wamekutendea??
Aligoma katakata kusema.

Nitakua mtu wa mwisho kupiga kelele za kusema Yanick Bangala na Djuma Shabani ni watovu wa nidhamu wakati kilichomuondoa Feisal Salumu hakijulikani ni wazi Kabisa Jangwani Kuna tatizo na si wachezaji.

Nawasilisha hoja.
 
Labda tuanze na swala la Feisal kosa la Yanga ni lipi?

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Upo sahihi kabisa wabongo sio yanga tu hata timu za mikoani hata tukikua tulikua tunaona fugisu wanazofanyiwa wachezaji na kuonekana wabaya kumbe viongozi ndio nongwa sana
 
Achana namaneno hao wote niwaajiliwa pale yanga, we unadhani huyo feisal kwakumsikiliza tu mamake ambae ndio role model wake anaweza kwel kua naheshima namkataba! Huyo Yannick huko alikotoka anajulikana yuko hivyo kwaio wacha wasepe yanga ipo sana tu
 
Achana namaneno hao wote niwaajiliwa pale yanga, we unadhani huyo feisal kwakumsikiliza tu mamake ambae ndio role model wake anaweza kwel kua naheshima namkataba! Huyo Yannick huko alikotoka anajulikana yuko hivyo kwaio wacha wasepe yanga ipo sana tu
Mchezaji anajua ana mkataba anahojiwa anasema ana 20% za kubaki Yanga kuna haja gani ya kubaki nae? hata kina Sure boy na Aggrey Moris waliondolewa Azam kwa hizo tabia za migomo

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Manara alisema kule wenye akili ni yeye, JK na Mzee Sunday
 
Nadhani viongozi wa utopolo kuna ubabaishaji wanao tangia enzi na enzi,kama walishawahi kumteka kibu mkandaji baada ya mechi ya taifa stars ,ili asajili yanga,basi wasingeshindwa kutaka kuwadhulumu kina bangala na djuma,watu wakidai pesa zao wanazushiwa hawana nidhamu,haya je mayele hana nidhamu,mbona anaondoka zake.???kuna mengi sana yanaendelea chini chini hapo avic town,ila hayatakuja kuwekwa wazi mpaka mchezaji akishachoka ahadi hewa.
 
Achana namaneno hao wote niwaajiliwa pale yanga, we unadhani huyo feisal kwakumsikiliza tu mamake ambae ndio role model wake anaweza kwel kua naheshima namkataba! Huyo Yannick huko alikotoka anajulikana yuko hivyo kwaio wacha wasepe yanga ipo sana tu
Na Feisal ndiyo yupo hivyo?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…