Tusiwekeze sana maisha yetu kwenye ushabiki wa soka, tuzikumbuke familia zetu

Lupweko

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2009
Posts
23,566
Reaction score
24,891
Wachezaji, makocha, mameneja, maafisa habari na waajiriwa wengine pamoja na maafisa ubashiri wao wana kila sababu ya kuwekeza huko maana wanaingiza moja kwa moja kipato chao kupitia soka. Mashabiki siku zote huwa ndio watoaji; wanatoa fedha kwa ajili ya kiingilio, wanatoa muda wao, wanatoa maisha yao, wanatoa utu wao.

Sasa baba wa watoto kadhaa unawanyong'onyesha watoto wako wakikuona unalia hadharani tena mbele ya camera, eti kisa Yanga imefungwa, au Simba imefungwa! Jamani hii hapana, furaha ya mpira iwe ni kuangalia burudani, ikitokea timu yako imepoteza basi walau huzunika kiasi tena kimya kimya. Usijitoe utu wako kwa kugaagaa chini au kuangua kilio huku ukirekodiwa. Teknolojia ni jambo la kuogopwa, utakuja kuficha wapi sura yako makaburi yakifukuliwa?





Interlacustrine R, redio, Komeo Lachuma, Mkalukungone mwamba, kavulata

 
Aibu sana..
Nilikuta mama mmoja kavua nguo ya ndani krb na banda umiza anapeperusha juuu...🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…