MWALLA
JF-Expert Member
- Dec 12, 2006
- 16,952
- 10,500
View attachment 235838
Kutokana na hoja hizo zinazolibana Taifa, Sikuwa natarajia kama ipo siku viongozi wetu watawadhihaki wananchi, kwani haiwezekani uwaambie kuwa kura ya maoni itafanyika Aprili 30, wakati uandikishaji unavyokwenda hauridhishi, hii ni kuwadhihaki tu.
Tumefanya makosa, turudi nyuma na tutumie uandikishaji kwa daftari letu, kisha tufanye uchaguzi na Kura ya Maoni, kwa kutumia BVR inahitaji mwaka mmoja au miwili zaidi kuhakikisha tunaandikisha watu wote.
tatizo Serikali haipo tayari kusikiliza ushauri kwani tulishasema huwezi kuandikisha watu wote kwa kipindi hiki kilichobaki, lakini haikusikia, hizo mashine zikimaliza kuandikisha zibaki hapo kwa ajili ya kuwaingiza watu wanaofikisha umri wa kuandikishwa na mchakato huu uwe endelevu, jambo ambalo sidhani kama litafanyika.
Kutojua ukweli ni adui mkubwa, wanazungumza Katiba hawajaisoma...kuzungumzia jambo ambalo hujui ukweli wake ni tatizo, tusizungumze jambo kama hulijui undani wake
Usiwaelekeze jinsi ya kupiga kura kwani inajulikana na wanachotakiwa kukifanya ni kuwaelekeza kilichomo ndani ya Katiba hiyo na siyo kuwaeleza kwamba kapigeni kura ya NDIO kama anavyofanya kiongozi wa CCM BABA RIZ. hii siyo sahihi kwani ni watu wazima wanaweza kuamua wao wenyewe, alisema Msekwa.