bmbalamwezi
JF-Expert Member
- Mar 12, 2015
- 788
- 195
Tuisome Katiba Inayopendekezwa tuielewe vizuri na tusiburuzwe na Viongozi wa Dini au kundi lolote. Haya ni maneno yaliyosemwa leo na aliyekuwa mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Bw. Amon Mpanju katika mahojiano na TBC kwenye kipindi cha Jambo Tanzania asubuhi ya Jumatatu 6, Aprili, 2015. Mjumbe huyo amesema viongozi wa dini na makundi mengine watuache wananchi tuisome Katiba na tuilewe vizuri kwani inayo mambo mengi mazuri. Amekemea baadhi ya watu wanaopotosha wenzao na kusema mambo ambayo hayamo katika Katiba inayopendekezwa. Kuhusu miiko na maadili ya viongozi na watumishi wa Umma, Bwana Mpanju amesema vimeaanishwa vizuri ndani ya Katiba Inayopendekezwa. Kuhusu kuondolewa kipengele cha wananchi au wapiga kura kumuundoa Mbunge madarakani endapo hawaridhi naye amesema kipengele hiki kingeweza kuleta utata sana hasa katika zama hizi za upinzani.
Vile vile amesema kuwa wajibu huu bado wapiga kura wano kwani wakiona huyo mbunge hawafai wanamnyima kura uchaguzi unaofuata. Hivyo amewahimiza wananchi watumie muda wao vizuri wa kuisoma na kuilewa Katiba Inayopendekezwa na wasikubali kuburuzwa wala kupotoshwa na makundi mbali mbali ya watu. Amesema viongozi wa dini washiriki kutugawa sisi watanzania watuachie uhuru wetu.