Tusubiri lori liparamie wanaofanya biashara barabarani ndio tuchukue hatua?

Tusubiri lori liparamie wanaofanya biashara barabarani ndio tuchukue hatua?

Munjombe

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2018
Posts
2,107
Reaction score
2,985
Naandika kwa tahadhari tu.

Toka mwaka 2016 kasi ya watu kujenga vibanda, mabanda na kujazana kandokando ya barabara kufanya biashara na shughuli mbalimbali imekua ikiongezeka kila kukicha na kwa kasi kubwa sana.Vijana wanaitana tu toka vijijini kuja mjini kuanzisha misheni town kwa kuuza bidhaa mahali popote wanapotaka ili kujipatia ridhiki.

Si jambo baya kuwa na vijana wanapambana lakini upambanaji wao sio tu umekuja kuua uwezo wao wa kufikiri kwa kutoainvest au kwa kuivest kiwango kidogo sana cha ujuzi na akili kwenye biashara zao na maisha yao bali pia umepunguza nguvu kazi kwenye uzalishaji,kwa kuwa vijana wanaotandaza nguo barabarani mitaa ya kariakoo, Mbezi, Tandika au miji mingine hawazalishi chochote zaidi ya kua na maisha ya hand to mouth au kuwatumikia watu wanaowapa bidhaa waziuze na serikali haipati chochote kutoka kwao zaidi na zaidi wamekua kikwazo kwenye movement ya magari na bidhaa kwa kuwa sasa magari hayapati nafasi tena ya kupita kwa uhuru na kwa haraka mfano ni barabara ya uhuru toka mnazi mmoja hadi karume,ilala boma pale.

Hoja yangu leo haikua kuangalia faida za watu waliojazana barabarani kwenye miji yetu bali kutoa tahadhari tu juu ya hatari inayoweza kutokea mbele ya safari. Mara kadhaa tumeshuhudia magari yakihama njia na kuparamia watu au makazi.Ni juzi tumeshuhudia Basi likaparamia nyumba kule shinyanga. Je, tutasubiri watu wangapi waparamiwe na lori ili tuanze kuwatoa watu barabarani?.Vipi siku gari likihama njia pale mbezi louis ama pale Ubungo Plaza hakutakuwa na dhahama kweli?

Tumekua wazuri sana wa kuanza mikakati baada ya janga kutokea lakini ni muhimu sana tukaanza kujifunza na kua na fikra za kuzuia tatizo badala ya kila siku kuunda kamati au kua na amsha amsha baada ya tukio.Huku kwetu Njombe na mashambani viongozi wa vijiji hawakazani tu kuhimiza njia za kuzuia moto bali wanaweka msisitizo kwe makatazo ya uchomaji moto ovyo angalau sasa misitu hususani pines zinasurvive.

Nihitimishe kwa kusema moto soko la kariakoo sio tu kuna watu hawatalipwa fidia kwa mali zao kutokuwemo kwenye list ya watu walipoteza kwa kua vibanda vyao na mali kulizunguaka soko havitakua kwenye list ya wapangaji lakini huenda vimeibwa na wahuni kwa kutohifadhiwa sehemu sahihi na kutokua kwenye maeneo sahihi.Hivyo sasa tujifunze namna bora ya kupangilia miji yetu na biashara zetu kwa kuangalia usalama wa watu na biashara zao.

Wakubwa tuambieni sasa
Sheria zetu za mipango miji,sheria za usalama barabarani na sheria ya Barabara na hifadhi ya barabara zilikuja kwa kazi gani?

Greatings from Southern Highland.​
 
Fursa ya Raslimali zilizopo nchini ni nyingi Sana na hazijatumika kabisa, kuliko idadi ya watu.Shida ni ukosefu wa uongozi.

Mwafrika akishiba Katu hawezi tunga sera bora ya kuboresha maisha ya watu.

Mwafrika akiwa na njaa huwa na akili,akishiba akili ulala.
 
Mimi nafikiri tuongoje tuone nini kitatokea (wait &see approach)
 
Mbona wameshapalamiwa sana? Mwenge na mbagala walishakufa baada ya lori kuacha njia? tukio la Mbagala kina mama wawili wauza nyanya walifariki, na wengine kujeruhiwa, halafu watu wakaanza kuwalaumu trafiki, inakuwaje wanaawacha watu wafanyie biashara barabarani? Walichowajibu wakasema hilo liko nje ya uwezo wetu waulizeni wana siasa, mjadala ukaishia hapo.
 
Tusubiri... Yakitokea ya kutokea tutaanza kuskia matamko yao
 
NDIYO, SASA WEWE UNATAKA MCHUKUE HATUA GANI KABLA YA TUKIO? UNAWEZA VUKA DARAJA KABLA HUJALIFIKIA?
 
Ni bora ya hii hali ili mradi mwisho wa siku kugawana chochote na wanyonge walee familia zao. Kinyume chake ni Kama kilichotokea Africa ya kusini. Sio kwamba Zuma ana wafuasi wengi bali wasio na kazi yoyote ya kuingiza kipato chochote wako wengi sana. Kwahiyo ikitokea sababu kama ya kukamatwa Zuma basi wahuni wasio na kazi wanaelekea madukani tena kwa wingi. Kwa hapa ni ngumu mtu mwenye meza au kibanda Kariakoo,tandika, buguruni kumshawishi kwenda kufanya fujo. Ndo maana kipindi cha JK maandamano ya upinzani yalifanikiwa sababu machinga walibughudhiwa sana. Na kipindi cha JPM sio rahisi kumshawishi mtu maana wapo bize na umachinga wao. South Africa waliopo mtaani ambapo hawaruhusiwi kujenga vibanda wapo wengi sana ndo maana crime rate ipo juu. Ukiifikiria kwa umakini ukaweka Siasa pembeni utanielewa.
 
Back
Top Bottom