Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unajidanganya sana.watu wanaandamana kwa sababu ya hoja za msingi na sababu yakufanya hivyo nasio kwasababu wana kazi zakufanya.na ndo maana mara zote serikali imekua ikitumia vitisho vya jeshi la polisi kutisha watu wasiandamane.Kama umesahau hivyo vitisho vilivyotolewa na serikali kupitia jeshi la polisi sema tukukumbushe maana yaonekana unajisahaulisha makusudi.Ni bora ya hii hali ili mradi mwisho wa siku kugawana chochote na wanyonge walee familia zao. Kinyume chake ni Kama kilichotokea Africa ya kusini. Sio kwamba Zuma ana wafuasi wengi bali wasio na kazi yoyote ya kuingiza kipato chochote wako wengi sana. Kwahiyo ikitokea sababu kama ya kukamatwa Zuma basi wahuni wasio na kazi wanaelekea madukani tena kwa wingi. Kwa hapa ni ngumu mtu mwenye meza au kibanda Kariakoo,tandika, buguruni kumshawishi kwenda kufanya fujo. Ndo maana kipindi cha JK maandamano ya upinzani yalifanikiwa sababu machinga walibughudhiwa sana. Na kipindi cha JPM sio rahisi kumshawishi mtu maana wapo bize na umachinga wao. South Africa waliopo mtaani ambapo hawaruhusiwi kujenga vibanda wapo wengi sana ndo maana crime rate ipo juu. Ukiifikiria kwa umakini ukaweka Siasa pembeni utanielewa.
Kaondoka sasa, kaosge mcundu wako uendelee na shughuli zako.Yule dhalim ndiye alikuwa anawa encourage ili kupata cheap popularity
Ongezeko la machinga kwenye barabara za mijini ni kama ongezeko la maji kuzunguka kisiwa.Naandika kwa tahadhari tu.
Toka mwaka 2016 kasi ya watu kujenga vibanda, mabanda na kujazana kandokando ya barabara kufanya biashara na shughuli mbalimbali imekua ikiongezeka kila kukicha na kwa kasi kubwa sana.Vijana wanaitana tu toka vijijini kuja mjini kuanzisha misheni town kwa kuuza bidhaa mahali popote wanapotaka ili kujipatia ridhiki.
Si jambo baya kuwa na vijana wanapambana lakini upambanaji wao sio tu umekuja kuua uwezo wao wa kufikiri kwa kutoainvest au kwa kuivest kiwango kidogo sana cha ujuzi na akili kwenye biashara zao na maisha yao bali pia umepunguza nguvu kazi kwenye uzalishaji,kwa kuwa vijana wanaotandaza nguo barabarani mitaa ya kariakoo, Mbezi, Tandika au miji mingine hawazalishi chochote zaidi ya kua na maisha ya hand to mouth au kuwatumikia watu wanaowapa bidhaa waziuze na serikali haipati chochote kutoka kwao zaidi na zaidi wamekua kikwazo kwenye movement ya magari na bidhaa kwa kuwa sasa magari hayapati nafasi tena ya kupita kwa uhuru na kwa haraka mfano ni barabara ya uhuru toka mnazi mmoja hadi karume,ilala boma pale.
Hoja yangu leo haikua kuangalia faida za watu waliojazana barabarani kwenye miji yetu bali kutoa tahadhari tu juu ya hatari inayoweza kutokea mbele ya safari. Mara kadhaa tumeshuhudia magari yakihama njia na kuparamia watu au makazi.Ni juzi tumeshuhudia Basi likaparamia nyumba kule shinyanga. Je, tutasubiri watu wangapi waparamiwe na lori ili tuanze kuwatoa watu barabarani?.Vipi siku gari likihama njia pale mbezi louis ama pale Ubungo Plaza hakutakuwa na dhahama kweli?
Tumekua wazuri sana wa kuanza mikakati baada ya janga kutokea lakini ni muhimu sana tukaanza kujifunza na kua na fikra za kuzuia tatizo badala ya kila siku kuunda kamati au kua na amsha amsha baada ya tukio.Huku kwetu Njombe na mashambani viongozi wa vijiji hawakazani tu kuhimiza njia za kuzuia moto bali wanaweka msisitizo kwe makatazo ya uchomaji moto ovyo angalau sasa misitu hususani pines zinasurvive.
Nihitimishe kwa kusema moto soko la kariakoo sio tu kuna watu hawatalipwa fidia kwa mali zao kutokuwemo kwenye list ya watu walipoteza kwa kua vibanda vyao na mali kulizunguaka soko havitakua kwenye list ya wapangaji lakini huenda vimeibwa na wahuni kwa kutohifadhiwa sehemu sahihi na kutokua kwenye maeneo sahihi.Hivyo sasa tujifunze namna bora ya kupangilia miji yetu na biashara zetu kwa kuangalia usalama wa watu na biashara zao.
Wakubwa tuambieni sasa
Sheria zetu za mipango miji,sheria za usalama barabarani na sheria ya Barabara na hifadhi ya barabara zilikuja kwa kazi gani?
Greatings from Southern Highland.
Huwezi kuelewa sababu umeshachagua kuwa upande wa kutokuelewa. Mtu ambaye kashajichokea humtishi na polisi, kipindi kile cha Dr. Slaa na mabomu Arusha hakukuwa na vitisho!?,watu walipigwa mabomu ya machozi na bado wakasonga mbele. Unafikiri raia wa South Africa wasio na ajira wanaogopa vitisho!?,hata ulete vifaru vya jeshi watavichoma moto tu. Tatizo hapa strike ni kwa ajili ya wanasiasa. Hata Mbowe kashashtuka ndo maana ka mute,hayo maandamano ya katiba hata bila vitisho hampati mtu.Unajidanganya sana.watu wanaandamana kwa sababu ya hoja za msingi na sababu yakufanya hivyo nasio kwasababu wana kazi zakufanya.na ndo maana mara zote serikali imekua ikitumia vitisho vya jeshi la polisi kutisha watu wasiandamane.Kama umesahau hivyo vitisho vilivyotolewa na serikali kupitia jeshi la polisi sema tukukumbushe maana yaonekana unajisahaulisha makusudi.
Du lile tipa liliwasaga vibayaIlishatokeaga boko magengeni 2018 tipa iliacha njia na kwenda kuwagonga bodaboda na baadhi ya wafanyabiashara na kuwapotezea maisha na wengine kujeruhiwa vibaya pembezoni mwa barabara ya bagamoyo
Inawezekana ukawa na hoja ya msingi mdau wangu........kuna vitu vingi vya kuangalia kwenye kundi hili.......ubaya ni kwamba hawa wanaolalamika kuhusu hawa vijana ndio wanunuzi wakubwa hizo bidhaa zao.......Ni bora ya hii hali ili mradi mwisho wa siku kugawana chochote na wanyonge walee familia zao. Kinyume chake ni Kama kilichotokea Africa ya kusini. Sio kwamba Zuma ana wafuasi wengi bali wasio na kazi yoyote ya kuingiza kipato chochote wako wengi sana. Kwahiyo ikitokea sababu kama ya kukamatwa Zuma basi wahuni wasio na kazi wanaelekea madukani tena kwa wingi. Kwa hapa ni ngumu mtu mwenye meza au kibanda Kariakoo,tandika, buguruni kumshawishi kwenda kufanya fujo. Ndo maana kipindi cha JK maandamano ya upinzani yalifanikiwa sababu machinga walibughudhiwa sana. Na kipindi cha JPM sio rahisi kumshawishi mtu maana wapo bize na umachinga wao. South Africa waliopo mtaani ambapo hawaruhusiwi kujenga vibanda wapo wengi sana ndo maana crime rate ipo juu. Ukiifikiria kwa umakini ukaweka Siasa pembeni utanielewa.
Kimetokea mara nyingi tuMimi nafikiri tuongoje tuone nini kitatokea (wait &see approach)