Tusubiri lori liparamie wanaofanya biashara barabarani ndio tuchukue hatua?

Ilishatokeaga boko magengeni 2018 tipa iliacha njia na kwenda kuwagonga bodaboda na baadhi ya wafanyabiashara na kuwapotezea maisha na wengine kujeruhiwa vibaya pembezoni mwa barabara ya bagamoyo
 
Unajidanganya sana.watu wanaandamana kwa sababu ya hoja za msingi na sababu yakufanya hivyo nasio kwasababu wana kazi zakufanya.na ndo maana mara zote serikali imekua ikitumia vitisho vya jeshi la polisi kutisha watu wasiandamane.Kama umesahau hivyo vitisho vilivyotolewa na serikali kupitia jeshi la polisi sema tukukumbushe maana yaonekana unajisahaulisha makusudi.
 
Hasa hapa kwa msuguri round about wameziba njia kabisa
 
Ongezeko la machinga kwenye barabara za mijini ni kama ongezeko la maji kuzunguka kisiwa.
Lisipodhibitiwa itakuja hatari kubwa. Kila kukicha wengi huvutika kuingia umachinga na hatari kuongezeka.
 
Huwezi kuelewa sababu umeshachagua kuwa upande wa kutokuelewa. Mtu ambaye kashajichokea humtishi na polisi, kipindi kile cha Dr. Slaa na mabomu Arusha hakukuwa na vitisho!?,watu walipigwa mabomu ya machozi na bado wakasonga mbele. Unafikiri raia wa South Africa wasio na ajira wanaogopa vitisho!?,hata ulete vifaru vya jeshi watavichoma moto tu. Tatizo hapa strike ni kwa ajili ya wanasiasa. Hata Mbowe kashashtuka ndo maana ka mute,hayo maandamano ya katiba hata bila vitisho hampati mtu.
 
Ilishatokeaga boko magengeni 2018 tipa iliacha njia na kwenda kuwagonga bodaboda na baadhi ya wafanyabiashara na kuwapotezea maisha na wengine kujeruhiwa vibaya pembezoni mwa barabara ya bagamoyo
Du lile tipa liliwasaga vibaya
 
Inawezekana ukawa na hoja ya msingi mdau wangu........kuna vitu vingi vya kuangalia kwenye kundi hili.......ubaya ni kwamba hawa wanaolalamika kuhusu hawa vijana ndio wanunuzi wakubwa hizo bidhaa zao.......
 
Machinga walitengenezwa na wanasiasa kwa malengo ya kisiasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…