1. Hizo Nchi ulizozitaja ama zipo Dunia ya kwanza au ya pili na bado pamoja na kutumia lugha zao lakini wanatumia na Kiingereza, sembuse sie tulio mwisho wa Dunia ama Dunia ya tatu au ya nne ndio tujifanye jeuri?
2. Sisi wenyewe bado kiswahili kinatupiga chenga ya kisigino, na kibaya zaidi, hao wasiojua sawa sawa Kiswahili ndio walijaa kwenye fani za ualimu na utangazaji.
3. Bado kiswahili hakijajitosheleza kwa maneno na majina mengi ya vitu.
4....
Tusifanye haraka kukikataa Kiingereza, ikifikia muda wake muafaka, kitazimika chenyewe.[/QUOTE]
Ndugu yangu! Kwanza usijiweke kwenye nafasi ya chini kiasi hicho kwamba wewe ni wa dunia ya tatu au nne. Kiuhalisia, hakuna dunia ya kwanza, pili, tatu, au nne. Watu walioigawa dunia kinadharia wakati huo (ambao ni wasomi wa ulaya na marekani) walikuwa na ajenda yao ambayo hadi sasa wanayo nayo ni "divide the world and rule it". Wanajua kisaikolojia kwamba ukimwambia mtu asiye makini ktk kufikiri kwake kwamba yeye ni wa ngazi fulani ya chini na akaamini basi tayari umempata--utamtawala na atatawalika. Hiyo ndiyo mbinu iliyotumika Rwanda (umeona matokeo yake), ilitumika Afrika ya Kusini (uliona taabu yake), ilitumika kwetu Tanzania (weupe juu, wahindi katikati, mmatumbi chini).
Kuhusiana na hilo, saikolojia yake ni nyepesi tu: ukijiweka juu na wakakuona kama uko juu unapata mamlaka ya kuwapangia matabaka wale wanaodhani upo juu nao chini, na watayakubali matabaka yale. Wakishakubali watajiweka ktk nafasi ambayo inaendana na matabaka ambayo wanadhani wamo na hiyo itawaathiri akilini mwao. Watauona ulimwengu (mind set) kwa namna hiyo ya kitabaka nawe utapata fursa nzuri sana ya kuwatawala maana wanakuona unastahili (upo juu) na wapo tayari kukusikiliza na kukutegemea. Kwa hiyo ugawaji wa dunia katika matabaka unachangia ktk mradi wetu uleule--kujenga "New World Order" na kuutawala mfumo huo. Kwa hiyo, unapotumia maneno hayo (first, second, third country au sijui developed and developing or poor contries) ujue what is behind such categorisation. There is a lot more about this so please find it and wake up mentally (zinduka)!
Pili, kwa mawazo yaliyopo sasa ambayo wadau wamechangia, tusikatae kabisakabisa kiingereza kwani tunakihitaji halafu pia tunahitaji lugha nyingine za nje kwa ajili ya maendeleo yetu binafsi na kitaifa. Tunachotakiwa kukataa ni matumizi ya lugha ya kiingereza kama lugha ya kufundishia na kujifunzia. Kwa sababu kwanza si lugha inayotutambulisha sisi duniani (lugha ni sehemu muhimu sana ya utambulisho wa nchi na watu wake (national identity). Pili, kwa mazingira ya sasa nchini mwetu, mtoto hawezi kumudu lugha ya kiingereza kiasi cha kuitumia kama lugha ya fikra, ubunifu, na hata mawasiliano. Kuna vikwazo vingi vinavyomzuia mtoto huyu kufikia kiwango hicho cha lugha...tunazijua sote kwa hiyo hakuna haja ya kuziorodhesha hapa. Matokeo yake unayaona...huna haja ya kuchunguza sana ili ujue ni kiasi gani watu wetu wameathirika kutokana na mapungufu ya elimu na fikra ambayo, kwa sehemu kubwa, yanachangiwa na ubovu wa sera ya lugha ya kufundishia...
Tatu, ujue vizuri kwamba Kiswahili kimeendelezwa na kimefikia kiwango cha kutosha kabisa kwa matumizi mbalimbali, ikwa ni pamoja na kuitumia kwa tafiti za kisayansi, kiteknolojia na biashara na pia ktk kufundishia toka shule za awali hadi vyuo vikuu. Watembelee Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na utaona maajabu. Kinachokosekana, pamoja na mambo mengine, ni utashi wa kisiasa (political will). There is also lack of seriousness on the part of our Government...sijui wana agenda gani ya siri kuhusiana na elimu ya Tanzania...