Lugha ya kiswahili,huko mitaani,inakua kwa kasi sana lakini katika kilinge cha Elimu sidhani kama inakua wa kasi hiyohiyo.
Si kweli kwamba Lugha ya kiswahili imekua kiasi cha kuweza kufaa kuwa lugha ya kufundishia sekondari na vyuo vikuu, hata kama kuna anaye amini imekua kiasi hicho vitabu viko wapi?
Sijaona mwalimu akifundisha Biology chemistry au physics kwa kiswahili.
Hesabu ya Culculas,linear algebra au Differential equation itafundishwa vipi kwa kiswahili? Msamiati upo??
Neno base, coefficient au hata constant kiswahili ni nini?
Ili Kiswahili kiweze kutumika darasani hadi evel ya University zinahitajika juhudi za makusudi kama kuchukua msamiati toka Kilatini kihindi na Kiarabu.
Maneno karibu yote ya English asili yake ni Kilatini na baadhi ni ya Kiarabu na kihindi.
English pamoja na lugha kadhaa Ulaya ni lugha asilia zenye uwezo wa kuelezea kwa ufasaha ujanja karibu wote uliopo hapa duniani.
Ila kama tunataka tu kuwa na elimu ya kibabaishaji na pengine ya mahudhurio ni kweli tunaweza anza fundisha kwa kutumia kiswahili hadi University.
Tatizo kubwa ni; Watu wengi Tanzania wanadhani wakipewa mtihani wa kiswahili watapata 100%. Ukweli ni kwamba kiswahili kama lugha ni ngumu kujifunza na kuongea kwa ufasaha.
Kiswahili ni kigumu kwa sababu hakijaanza kupewa uzito unaostahili. Serikali haijaanza kufanya hivyo. Walimu shuleni hawajaandaliwa kufundisha kwa kiswahili hayo masomo ya science kwa sababu hawajawezeshwa kufanya hivyo...ni jambo la kisera na mwamko. Ndiyo maana tunalijadili hapa. Tunataka serikali itambue umuhimu wa lugha hii na ianze kujenga mazingira yanayohitajika.
Pia napinga kwamba kiingereza na lugha nyingine ulaya ni lugha asilia...lugha hizo zinahistoria ndefu ya ukuaji...historia yake inaanzia hapahapa africa...hata taaluma ya kuandika ilianza africa (e.g., Nubia ambayo sasa ni Sudan). Wazungu wa kale walipata maarifa mbalimbali kuhusiana na lugha na taaluma nyingine toka kwetu...(soma "the Black Athena" na vitabu vingine vya historia ya ulimwengu). Kwa ujumla asili ya taaluma zote zilizopo duniani ni africa. Hata ushirikina ulianzia kwetu.
Kwa mfano historia inatuambia kwamba watu walishaanza kutumia hisabati ktk maisha yao zaidi ya miaka 30 000 iliyopita huko maeneo ya Kongo na kusini mwa afrika. Wazungu na waarabu wameendeleza tu na kuzifanya taaluma zile ziwe za kisasa na bora zaidi.
Huyu hapa pia anakubaliana na mimi hasa kuhusu eneo la sahara:
"African literacy began in the Sahara over 5000 years ago (Winters 1971, 1981a,1983). This earliest form of writing was a syllabic system that included hundreds of phonetic signs, which over time was shortened to between 22 and 30 key signs. This civilization was later spread to the rest of the world, including the Arab and European worlds"
Pia soma hii text
"The original inhabitants of the Sahara were not Berbers or Indo-Europeans (Winters 1985b). This was the ancient homeland of black African people (Anselin 1989, p.16, 1992; Winters 1981,1985b,1989, 1991,1994). The inhabitants of this area lived and created innovations around and after 4000 B.C. We call these people the Proto-Saharans (Winters 1985b, 1991)".
Kwa hiyo ustaarabu wa wazungu umeanza juzijuzi tu. Msemo usemao "Usimwamshe aliyelala, ukimwamsha utalala wewe" una maana kubwa. Lakini ukijitambua umelala na umechoka kulala basi hunabudi kuanza kuamka.
Kwa kifupi maarifa mengi yamejificha kwenye lugha zetu za asili...na kwa sisi wenyewe na akili zetu, ila haujatambua vya kutosha...sawa ni vizuri kujua lugha nyingine ili uazime maarifa toka kwa wengine, lakini kumbuka kwamba chanzo cha maarifa ni ubunifu unaotokana na lugha unayoielewa sana...Hapo unaweza kuunda misingi mipya ya fizikia, kwa mfano, na kutunza ktk maandishi kwa kutumia lugha yako. Wengine wakitaka kujua ni lazima wajifunze kiswahili...that's how it started in europe.
Sasa unasema kiswahili kigumu, je kiingereza je? Kumbuka kwamba: Nasisitiza kwamba tujifunze lugha nyingine kama kiingereza tena kwa bidii...lakini jambo la msingi ni kuikubali na kuitumia kikamilifu lugha yetu ktk elimu. Jukumu la serikali nikuhakikisha kiswahili kinatumika kama lugha ya kufundishia. Mbona you can innovate using any language you know best...unaweza kubuni mashine hata kwa kutumia kimakonde. Wazungu wanabuni na kuhifadhi maarifa yao ktk lugha yao. Maana yake ni kwamba mimi naweza kufanya hivyo hivyo kwa kutumia lugha yangu...
Nakubali kabisa unaposema kwamba
"Ili Kiswahili kiweze kutumika darasani hadi evel ya University zinahitajika juhudi za makusudi kama kuchukua msamiati toka Kilatini kihindi na Kiarabu. Maneno karibu yote ya English asili yake ni Kilatini na baadhi ni ya Kiarabu na kihindi."
Na hivyo ndivyo wanavyofanya Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) pale chuo kikuu cha Dar es Salaam. Tatizo ni kwamba support ya serikali ni haba hasa kisera na pesa.
Pia angalia video ambayo imekuwa posted na EMT hapo juu...kwa ujumla unaweza kupata taaluma ktk lugha yoyote unayomudu zaidi, si kiingereza tu.