Tutaachana lini na lugha ya kiingereza?

Hapo ndipo "Miafrika Ndivyo Tulivyo" comes into play.

Kwa nini hatuna textbooks zetu wenyewe? Si tunajidai tuna akili sana....sasa nini kinachotushinda?

Waingereza wako juu sana. Nani anabisha?

Sasa unaposema miafrika yote ndivyo tulivyo una maana ktk kundi hilo la miafrika, wewe pia umo...lakini kumbuka sisi wengine hatumo. Nyakati za kujidharau sasa zimekwisha...the new world order is not compatible with this...

Halafu unaposema waingereza wako juu sana, huko juu ni wapi? Halafu neno waingereza linahitaji ufafanuzi. Ukienda uingereza saa hizi utawaona watu wanaoonekana kama waarabu, wapakistani, wahindi, wabantu, wabongo na watu weupe ambao sisi hupenda uwaita wazungu...lakini wote hawa ni waingereza na si wote wanajua kiingeraza. Mitaa ya London utasikia lugha mbalimbali na tamaduni mbalimbali. Kwa hiyo unasema wote hawa wako juu? Wapi juu? Hicho kiswahili unachokidharau, wenzio huko uingereza na mahali pengine (Japan, China, Ujerumani, Scandinavia, Marekani nk) wanakimezea mate kwa sababu ya utamu wake. Halafu Rais wa Gabon alipomwomba JK ampelekee mwalimu wa kiswahili ili ajifunze kiswahili unadhani ni mambo ya mzaha...unayo dhahabu na unaidharau jamani. Yaani hata wewe askarikanzu unamuunga mkono jamaa huyu!
 
Mkuu huyu Nyani Ngabu ni mbeba box flani ambaye wakati mwingi inabidi umsome katikati ya mistari (read between the lines) ili umuelewe. Sidhani kama amemaanisha hicho alichoandika hapo. Labda nimekosea, lakini nilivyomwelewa hapo Ngabu ameandika kwa kutumia kejeli, unaa (irony) zaidi!
 
English is the lingua franca of the world. We need english more than it needs us. If u cant beat them just join them and beggars are not choosers. International business and politics,as well as relations are all influenced by english language so let us take bitter pills.
 

1. Hizo Nchi ulizozitaja ama zipo Dunia ya kwanza au ya pili na bado pamoja na kutumia lugha zao lakini wanatumia na Kiingereza, sembuse sie tulio mwisho wa Dunia ama Dunia ya tatu au ya nne ndio tujifanye jeuri?

2. Sisi wenyewe bado kiswahili kinatupiga chenga ya kisigino, na kibaya zaidi, hao wasiojua sawa sawa Kiswahili ndio walijaa kwenye fani za ualimu na utangazaji.

3. Bado kiswahili hakijajitosheleza kwa maneno na majina mengi ya vitu.

4....

Tusifanye haraka kukikataa Kiingereza, ikifikia muda wake muafaka, kitazimika chenyewe.
 

Asante mkuu. Kama ndiyo ilivyo basi hasira zangu zimeyeyuka. Halafu naomba ndugu Nyani Ngabu anisamehe kwa kilichonitoka mdomoni...jamani dunia hii!
 

Hizo sentensi mbili za mwisho ni kama zinanichefua vile. Halafu mwonekano wake naye huyu! Ujue kwamba hiyo lugha ya kiingereza si lugha yako mama. Nithibitishie basi kwa kuniandikia angalau aya mbili tu kwa lugha hiyo. Halafu pia niandikie aya mbili nyingine kwa lugha ya kiswahili...Tunachosema wenzio ni hiki: Mudu lugha yako na uitumie katika ukamilifu wake wote, halafu wakati huohuo jibidiishe na lugha kadhaa za wenzio, ikiwa ni pamoja na kiingereza. Halafu pia nakushauri usafiri nje kidogo--nenda uingereza, uchina, scandinavia, na uingereza, kwa mfano. Ukiwa huko, usijihangaishe ktk kushangaa vinavyoonekana tu, pia chunguza sera zao na mijadala yao kuhusu lugha zilizomo nchini mwao. Chunguza hasa sera zinazohusu lugha za kufundishia na kujifunzia---utakaporudi kwenye jukwaa hili ninauhakika utaelewa vizuri tunachojadili. Kwa kifupi, lugha ni moyo wa elimu. Ukicheza na lugha, unacheza na elimu.
 

Then wakenya na waganda wakichukua ajira zenu kwaajili ya lugha msilalamike. Kama tayari unajua kiswahili then ni kwa nini usite kujifunza lugha nyingine? Umaimuna huu ndio unaturudisha nyuma. Mkisusa wenzenu wanakula!
 
Then wakenya na waganda wakichukua ajira zenu kwaajili ya lugha msilalamike. Kama tayari unajua kiswahili then ni kwa nini usite kujifunza lugha nyingine? Umaimuna huu ndio unaturudisha nyuma. Mkisusa wenzenu wanakula!

Mjadala umefika mbali sana kuliko hapo ulipo wewe. Soma mjadala mzima halafu utoe maoni yako, maana inavyoonekana, umekurupuka tu. Halafu huo umaimuna unaouzungumzia sijui una uhusiano gani na busara zilizomo kwenye mjadala huu. Nakushauri utafute mkeka ujipumzishe...halafu urudi tena kwenye jukwaa letu na mawazo mapya.
 

Your rather unclear argument is: "If u cant beat them just join them and beggars are not choosers". What does "them" represent? Why should it be that it's you and only you who should either beat or join them? What about them joining you? Which social position do you put yourself in between you and 'them'--higher, lower, equal?

You continue: "beggars are not choosers". Are you a beggar? Begging from whom and why? Is your mind truly free from psychological slavery? How much do you trust yourself as a person from whom others can beg? Why aren't you ready to develop your kiswahili into an international language of trade and commerce? Do you think the English you're so proud of just emerged from nowhere? Vinavyoelea vimeundwa nawe hunabudi kuunda kilicho chako ili nacho kielee. And remember: no one has told you to quit English or any other european language. Sorry for being such a rough contributor! The aim, however, is to let you think about these issues from another perspective and do so more critically.
 
Some food for thought

It is silly how so many African countries speak a European language instead of their native language. The only country that speaks their language is Tanzania which is KiSwahili. I think that since most African countries speak European languages, we might as well switch to a common African language. My guess would be KiSwahili since it is the most widely spoken. YES English is important to learn and we can learn it but our official languages should be KiSwahili. The Arabs have Arabs, us Africans should have KiSwahili.

Do you think this is true? What can we do about it?

Toka kwenye Nairaland

Waafrika ni wagumu sana kukubaliana. Haya mawazo yalishatolewa na akina Nyerere na Nkrumah tangu wakati wa uhuru lakini hakuna aliyetaka kuyafuata.

NB: Tatizo sisi wenyewe tunaosifiwa kuwa na lugha kubwa Afrika nzima bado tunajiona duni na kujidharau. Hadi hii leo, miaka 50 baada ya uhuru bado tuna kasumba ya kuona kujua Kiingereza ni sawa na kuwa mwerevu. Huko Uingereza hata mtoto wa chekechea anaongea Kiingereza. Kwa hiyo tumwone huyo mtoto katuzidi akili kwa sababu anakimudu Kiingereza, siyo?

Iko hadithi ya Waziri flani wa kutoka Pakistan alitembelea London na akaona hata mwendesha taxi na mfagiaji hotelini kwake anaongea Kiingereza sanifu. Aliporudi Pakistan yule Waziri alitoa mshangao wake kwa kusema "Uingereza wameendela sana, hata waendesha taxi na wafagiaji mahotelini wanazungumza Kiingereza cha hali ya juu". Duhu!
 
Last edited by a moderator:

Asante Askari Kanzu! Nimemsikia huyo jamaa kwenye video anavyobabaika. Inaelekea kwa sehemu kubwa hajitambui jinsi alivyotawaliwa kisaikolojia...Hiyo dhana kwamba ukijua lugha ya kiingereza basi umeendelea, kama unavyosema, si ngeni hata hapa nchini. Watu wanaoamini hivyo hupata kigugumizi cha nguvu ukiwaambia kuwa maendeleo hutokea hata kwa kukijua vizuri kimakonde na kukitumia ipasavyo....
 
Last edited by a moderator:
Historia inabainisha wazi tulipata uhuru wa bendera,hasa baada ya marekani kuwasihi wazungu waache aina ya ukoloni waliokua wanatumia bali waanzishe aina mpya ya ukoloni[neo-colonialis)
aina hii ina faida nyingi kuliko hasara na walidai aina ile ya ukoloni imepitwa na wakati,kwanza hakuna gharama ya kuweka viongozi kwenye koloni(wanajisimamia wenyewe) pia hakuna tena malalamiko ya tunatawaliwa..tunataka uhuru..
Katika kuanzisha aina mpya ya ukoloni,ndipo tukajengewa misingi ya kuwa tegemezi,kuanzia uchumi hadi lugha, na hii ilifanikiwa nchi nyingi sana,kwa mtindo wa kujifanya waliokuwa wakoloni wetu baada ya uhuru ni kaka au dada au baba yetu,kwahiyo inatubidi tuwasikilize wanalotaka.
Kwahiyo ndugu ni ukoloni mambo leo unaotusumbua,na tatizo kubwa ni utegemezi wa kiuchumi ambapo tunakopeshwa hadi madeni kutuzidi na wazungu wanaamua kutusamehe lakini kwa masharti kama hayo ya kutumia lugha zao,sasa ukiacha kufuata masharti yao ujue utawarudishia fedha zao ulizokopa na haukopeshwi tena,hii kitu ata mwalimu Nyerere ilimpa shida sana,sembuse hawa makanjanja.
Ni hayo tu
kanyigo.
 
anayetamani kukiacha kingeleza na akiache mi ndo kwanza najifunza
 
anayetamani kukiacha kingeleza na akiache mi ndo kwanza najifunza

Wewe baba mweupe (Whiteman), mjadala huu umefikia hatua ambapo tunasema hivi: Jifunze lugha yako, uielewe vizuri na uitumie kikamilifu ktk shughuli zinazohusiana na ujenzi na uendelezaji wa misingi ya kimaendeleo (k.m ktk elimu) na wakati huohuo jifunze kiingereza au lugha nyingine za kigeni kwa bidii zako zote kwani unahitaji sana lugha hizo pia (si kiingereza peke yake). Tupo pamoja sasa?
 
You cant take it just leave it folk! Also u cant change the world let the world change you! Congrats for being a smooth contributor basing on malice aforethought!!
 
Lugha is more than verbs, nouns.pronouns.Its more than simple sentence and compound sentece. Language is vehicle of human experience. Achebe says can English carry the full weight of African experience? If yes then we are well advised to stick to English. English is universal the Gold standard so to speak.
 
 
You cant take it just leave it folk! Also u cant change the world let the world change you! Congrats for being a smooth contributor basing on malice aforethought!!

What a mindset! So this is your other perspective: that you can't change the world and all you can do is let the world change you? Are you such a passive being? What do you mean by "the world"? Do you mean this current order in which the south is dependent on the north? And you think this can not be changed just because it has been shaped by what look to you as demi-gods (the folk in the north)?

I want you to trust yourself as a person, with excellent qualities and capabilities, and who can shape the world just like others in the north do. There is no malice here. If you depend on Britain today, Britain should depend on you tomorrow...and it all depends on you...just look inside you and see how powerful you are in terms of your mental qualities and capabilities---then develop them as much as you can using the language you know best---this is the way to mental liberation.
 
The views of Chinua Achebe do not represent the Alpha and the Omega on this issue. In fact many other African writers offer divergent views on the matter, i.e, including Ngugi wa Thiong'o, who once elaborated his thesis in his publication Decolonizing the Mind: The politics of language in African literature (1986). No one argues that English is not important, it is, but not at the cost of forsaking the mother tongue!

Kwa mfano, hapa tunajadili umuhimu wa lugha ya Kiswahili na mimi ninatumia Kiingereza kujieleza. Lakini pindi niandikapo kwa Kiswahili ninajisikia mtu huru na mwenye kujiamini zaidi. Hapo ndio umuhimu wa kujisifia na lugha asilia unapokuja.
 
You want me to trust myself?? What a joke pal? Its not obligatory to agree with me.....let us agree to disagree over this!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…