kipara kipya
JF-Expert Member
- May 2, 2016
- 20,141
- 24,449
Nchini Msumbiji walifanya uchaguzi wao oktoba 29/2024..uchaguzi ulikuwa na wagombea kutoka vyama kadhaa lakini vilivyokuwana upinzani wa karibu ni Frelimo kilichowakilisha na Daniel chapo huku Podems ikiwakilishwa na Venancio Mondlane..uchaguzi ulifanyika baada ya kampeni kali zilizokuwa na mvutano huku Mondlane na chama chake wakitishia kama hawatotangazwa washindi wataingia barabarani...tume ya taifa ya uchaguzi ikamtangaza Chapo ni mshindi Mondlane akaingiza vijana barabarani wakapigwa..wakatiwa vilema..wakauwawa uchumi ukaanguka...Dola ni dola Mondlane akaishi kama digi digi mwisho wa siku kaiangukia serikali kasaini maridhiano haijulikani kalipwa bei gani bila kujali wale wahanga waliokufa wakitetea tumbo la Mondlane..leo Chapo ana hudumu kama raisi..kila nikitafakari nayaona hapa kwetu kutumika kwa vijana kuumizwa na kuuwawa na kuachwa na vilema vya maisha wao watasaini maridhiano wakikutana kwenye misiba wanacheeka mpaka wana ambiana umenenepa kuliko mimi.....vijana jiongezeni msitumike kama toilet paper na wanasiasa....