Tutafika lini huku: Mbunge mmoja Marekani apitisha hoja ya kumuondoa Spika wa chama chake mwenyewe

Tutafika lini huku: Mbunge mmoja Marekani apitisha hoja ya kumuondoa Spika wa chama chake mwenyewe

Taso

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2010
Posts
2,507
Reaction score
2,412
Jamani wenzetu ni wazalendo, na wamejipa nguvu ya kushughulikia watawala wanaozingua. Unahitaji kura moja kuleta Azimio lijadiliwe!

Nchini Marekani Mbunge Matt Gaetz wa chama cha Republican jana amewasilisha hoja ya kupitisha Azimio la Bunge la kumuondoa Spika wa chama chake mwenyewe akidai ni mtu muongo ambae amekuwa akipitisha miswada isiyo na maslahi mapana ya nchi kama vile kumwaga mapesa vitani Ukraine wakati wananchi wanahangaika na mfumuko wa bei na maisha magumu. Kura itapigwa ndani ya siku mbili za shughuli za bunge.

07dc-explainer-1-1-08d3-superJumbo.jpg

Pichani Mbunge Matt Gaetz akimchana Mcacthy wa chama chake mwenyewe kwamba hafai kuwa Spika wakati wa uchaguzi wa kiti hicho mapema mwaka huu
#################################

Tulia Ackson types of the third world wangeweza ku last hata wiki moja kuongoza maataasisi yenye nguvu na ya watu wazalendo kama hawa ?

Tuna mstaafu mmoja aliwahi kusema hajui kwa nini hatuendelei, tena alikuwa ndio Rais. Majibu ndio kama haya.
 
Unaya kumbuka ya Oscar na Nyerere ? Unaya kumbuka ya Ndugai na Samia ?
 
Jamaa huwa hawana uchawa na unafiki inapofika Hoja ya kutetea wananchi. Huku uchawa ni mkubwa mno
 
Jamaa huwa hawana uchawa na unafiki inapofika Hoja ya kutetea wananchi. Huku uchawa ni mkubwa mno
Hawana njaa ila njoo huku kwetu viongozi wote njaa zilishahamia kichwani hebu niambie kifuatacho hapo unafiki na uchawi ili tu kulinda njaa zao
 
Back
Top Bottom