Tutafute jina lingine mbadala wa Mkuu

Tuongezee "ndu" mwisho wa hilo jina letu la awali.

Kama hapo mwanzoni werevu, wastaarabu na wenye hekima tuliitana 'mkuu' lakini sasa hivi wajinga, wapumbavu na wahuni wamekuwa wengi humu na hawana hadhi ya kuwa referred to as 'mkuu' basi hiyo suffix 'ndu' iwekwe mwishoni ili wawe wamepata jina linaloendana na hadhi yao, au nakosea mkuu?
 
MKuu Ujinga mtupu
 
Mkuu, unaonaje tukitanguliza neno " Muungwana" 🤔
 
Umesema point mkuu
Ngoja tuliangalie hili nalo, likifaa mbona wazo lako litapita bila kupingwa mkuu
 
Kwa heshima kuu niliyonayo kwako mkuu mi naona Ni Bora tuendelee tu kutumia neno mkuu mkuu
 
Mkuu hauna nidhamu mkuu!
 
Ukitupa suggestions mbalimbali itasaidia mkuu
 
Liendelee kutumika maana linafit kwa gender zote.

Pia unaweza kutumia Kiongozi/Chief/Ndugu etc
 
Tunapoelekea siyo pazuri.Tutaanza kuitana chawa si muda.
Mimi:Eee ndiyo nakupata chawa wangu!
Yeiyee:Haina kwere mkare wake.Weye ndiye chawa kimbwa chawa wangu.Basi tutacheki big chawa.
 
Hiyo 'ndu' kwenye mwili wako ndo haina heshima? Labda kama umeibadilishia matumizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…