Tutajuta kwa suala linaloendelea Ngorongoro, tutake tusitake

Great thread....ila figures kuhusu idadi ya tembo waliopo sasa sio sahihi wapo zaidi ya elf moja isipokuwa wanapatikana crater tu.
 
Kulishakuwa na mipango endelevu ya kupanga matumizi ya ardhi ya vijiji,
Na kila mfugaji kuwa na limiti ya ng'ombe anaoweza kuwa nao,
Ila wafugaji wa kuchunga siyo wafugaji wao no waswagaji,
Na ni wabinafsi Sana hawajali jamii zingine!
Kwa kweli
 
Dunia nzima kwa sasa inateigemea zaidi Tanzania kuhusu wanyama pori. ALIEKWAMBIA NANI? DUNIA INAITEGEMEA TANZANIA
Halafu jamaa muongo eti tembo 30 haahaaa Hilo si kundi 1 Tu!

Hawa jamaa wakianza kutumika na vikundi vya watu fulani fulani yaani huwa wanaweza kuleta taharuki nyuma ya keyboard!

Mbuga za Serengeti, Mikumi, Selous, Tarangire, Mkonazi, CHATO😂

Mbuga za Zim, Tswana, Kruger, Mmaasai Mara huko hazina wanyama?
 
Ngorongoro hakuwez kuwa tembo 30 au 30 Elfu? Hawa watu sijui huwa wanaandikiwa huu ujinga
 
Ngorongoro hakuwez kuwa tembo 30 au 30 Elfu? Hawa watu sijui huwa wanaandikiwa huu ujinga
Mkuu jamaa ana point ila hii exaggeration na fake data, inaonyesha anatumika na amekubali kutumiwa

Labda mtu awe nje ya nchi hii na hajawahi kukanyaga Bongo miaka 30, ndiyo aweza kuamini Ngorongoro ina tembo 30!

Hawa ni watu wana ki NGO Chao, wameanzisha #tag ya Kula $$, hakunaga watu wenye uchungu na hii nchi kihivyo bila mlungula kutembea.
 
Huo utafiti wako wa kimchongo kwamba dunia inategemea Tanzania katika wanyama pori umeufanyia wapi? Pia eleza ni kwa namna gani Masai wamechangia katika kupunguza idadi ya tembo sio blabla tu njoo na takwimu kabisa
 
Dunia nzima kwa sasa inateigemea zaidi Tanzania kuhusu wanyama pori. ALIEKWAMBIA NANI? DUNIA INAITEGEMEA TANZANIA
Unaweza kulinganisha Mbuga zilizopo Tanzania na Zimbabwe na South Africa!? Au unamaanisha nini?
 
Wamasai mmeshawasili[emoji23] Any way Endeleeni kukaa hifadhini na kula swala wazee
 
Wamasai ni kama waTanzania wengine, wasiruhusiwe kuvunja sheria kana kwamba wao ni special group katika hii mchi, watu wengi wameshafungwa miaka 60 hadi maisha kisa tu wamekutwa na kipande cha pembe ya faru, wao ni nani hadi waachwe waue wanyama? Game reserve police wafanye kazi yao bila ubaguzi, awe mmasai au mnyamwezi, washyghulikiwe ipasavyo!
 
Mi nadhani imefika wakati wa kuweka uzio (fensi) kutenganisha makazi ya maasai dhidi ya raslimali 'wanyama poli' ambayo ni nyeti na inatuingizia fedha nyingi, huku tukiratibu maendeleo ya makazi. Kazi hiyo ya kulinda raslimali kwa kuweka uzio pia ilifanywa na kufanikiwa pale Merelani katika eneo lenye uchimbaji wa madini ya Tanzanite!
 
Acha upuuzi wako,wanyama wangekuwa wanaangamizwa kwa Kasi kama unavyosema si wangeshaisha kitambo?

In fact wameongezeka Sana ndio maana ya kuanzishwa bucha za wanyamapori na migogoro ya wanyama kuvamia Mazao ya wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…