Tutakukosoa tu, hakuna aliyelazimisha uwe Rais. Sikiliza wapinzani tunataka nini

Tutakukosoa tu, hakuna aliyelazimisha uwe Rais. Sikiliza wapinzani tunataka nini

Memento

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2021
Posts
4,423
Reaction score
9,986
Ukisikiliza tena kwa makini ni kama naye hapendi kukosolewa. Anasema kabisa sio na kigazeti chako mara uandike samia hivi mara vile, vingine vya uongo vingine vya ukweli.

Hii kauli inalenga kuwatisha waandishi na wakosoaji. Siku 100 tu unaanza kuona kwamba kukosolewa kunauma je miaka mitano ijayo? Si ndio yatakuwa yaleyale ya mwendazake?

Udikteta hata wa mwendazake ulianza hivihivi kwa kufumbiww macho, mwisho ukashamiri. Hakuna aliyekulazimisha uwe mwanasiasa na uwe Raisi, hivyo ukiona kazi ngumu jiuzulu.

Ili kuepuka yote hayo tunahitaji KATIBA MPYA KWA HARAKA SANA. Bila hii katiba mpya tegemea wakosoaji kuongezeka siku hadi siku na tegemea kila aina ya ukosoaji maana tushakua sugu sasa.

Katiba ni kaburi la CCM, hivyo tusitegemee wataikubali kirahisi rahisi. Hakuna mwanaccm anayeweza kuishi nje ya mfumo wa kubebana bebana. WanaCCM kwao cha kwanza ni madarska na vyeo. Walijikomba sana kwa jiwe na leo wanajikomba sana kwa huyu mama. usishangae kesho raisi akawa Steve nyerere wakaanza tena kujikomba kwake.

Hii katiba ya safari hii ni lazima mchakato ukamilike hakuna tena excuse.

KATIBA MPYA NI LAZIMA
 
Anasema eti tumkosoe kwa staha!Atakosolewa kwa staha akiwa nyumbani kwake pamoja na familia yake,lakini akiwa amekalia kiti cha urais ajue kuwa atakosolewa kwa mujibu wa katiba.
Kabisa, Kama anataka kukosolewa kwa staha aachie uongozi. ukiwa kiongozi kukosolewa ni lazima na usiwachagulie wakosoaji cha kukukosoa
 
Kuongoza Taifa hakujawahi kuwa kazi rahsi hata sku moja
 
Yani asikilize mnataka nini?

Mnafikiri Rais ni bibi yenu ee?

Rais atafanya kazi kwa mujibu wa taratibu na ilani ya chama chake cha ccm!

Eti asikilize wapinzani tunataka nini[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Anasema eti tumkosoe kwa staha!Atakosolewa kwa staha akiwa nyumbani kwake pamoja na familia yake,lakini akiwa amekalia kiti cha urais ajue kuwa atakosolewa kwa mujibu wa katiba.
Mbona mmeanza mapema sana kunena kwa lugha? Hadi 2025 si mtatoa ndimi nje?

Si mlikuwa mnademka nae mkisema anawakomesha mataga?
 
Mbona mmeanza mapema sana kunena kwa lugha? Hadi 2025 si mtatoa ndimi nje?

Si mlikuwa mnademka nae mkisema anawakomesha mataga?
Unajua ulichoandika?
 
Kuongoza Taifa hakujawah kuwa kazi rahsi hata sku moja
Hata hawa wenzetu wanaomkosoa mama kwa hili laiti wangepewa huo Urais kunauwezekano ndo wangekuwa wabaya sana. Tukubali tu kila mtu ana vitu anavyoviamini na kuvisimamia mkitaka Rais afanyie kazi mawazo ya kila mwanasiasa ili tu kuwafurahisha sio kitu chepesi. Mwanadamu hakosi mapungufu hata hao akiana Lisu na Mbowe pia wanamapungfu mengi mfano Lisu alishakuwa mbunge jimboni kwake wananchi wanajua mapungufu yake pia hata Mbowe amekuwa mwenyekiti kwa kipindi kirefu bila kuachia kijiti je? akiitwa dictatorr vijana a.k.a nyumbu mtakubali?
 
Sijampata kuona lichama la hovyo Kama CCM kwao mtu akiwa rais ana madaraka zaidi ya mwenyezi Mungu.
 
Back
Top Bottom