Tutengeneze matajiri wetu sisi wenyewe kwa makusudi kabisa

Tutengeneze matajiri wetu sisi wenyewe kwa makusudi kabisa

Kilamunu

Member
Joined
Aug 25, 2021
Posts
81
Reaction score
208
Habari ndugu zangu,

Naishauri serikali iweke vipaumbele vya kutengeneza matajiri wazawa weusi wenye asili ya ndani ya nchi tokea enzi za mababu. Mfano kama kwa Nigeria alivo Aliko Dangete,au hapa kwetu the Late Reginald Mengi.

Hii Ina maana kubwa sana kwa nchi. Leo hii tajiri namba moja Tanzania kuwa Modewji, au Azam Bakhresa n.k, si afya sana hata kwa usalama wa nchi. Wakiamua kwa Nia thabiti kabisa kuuteteresha uchumi hawashindwi. Mfano kwa Azam akitingisha tu kibiriti Zanzibar hoooi, hoooi.

Kwa upande wa ajira, jamani kuajiriwa na wazawa ni raha na afadhali kuliko hawa wahindi. Yaani Kuna upendeleo wa ajabu huko ndani. Waarabu kiasi flani ahueni laki Bado Bado. Kwa wale ambao tushazunguka kufanya fanya ajira katika hizo pande ushahidi mnao.

Ukiwa kwa Mwafrika mwenzio kidogo Kuna kauhuruma kapo. Sina ushahidi lakini kwa nlivo sikia ni kwamba Reginald Mengi ni alitengenezwa na serikali awe tajiri. Alianza na biashara ya kalamu tu. Kama mnavojua serikali ikiamua hakuna kinacho shindikana Mzee wetu alitoboa.

Mungu amrehemu yule Mzee, kuna kipindi nlikuwa nko kitengo flani akija tu ukimpokea kabegi lake na kumpeleka VIP kukuacha na laki tano ni jambo la kawaida. Na muda wa kurudi atakuuliza, hivi nlikupa chochote? Hii ndio raha ya mwafrica tajiri kwa Mwafrica mwenzie.

Nashauri kwenye bonde kama la Bwawa na Nyerere like eneo linalofaa kilimo basi pawe na mpango kazi watanzania wenye Hela zao wawekwe huko na kuhakikishiwa sapoti zote Ili tutoe watajiri wengi wa ngozi nyeusi.

Ikumbukwe, baada ya serikali kataifisha miradi mingi kipindi hichoooo na yenyewe ikashindwa kuiendeleza ilionekana Bora wabinafsishe kwa watu. Matokeo yake babake Mohammed Dewji alichukua viwanda vingi vya nguo hapa nchini. Huko Tanga alichukua viwanda kedekede ya sabuni n.k, akageukia mashamba ya mikonge.

Baadhi ya viwanda vya nguo pale Tanga alichukua mitambo yake na kupeleka Morogoro huko Tanga akaacha Magofu. Akaenda Lushoto kuhodhi mashamba ya chai pamoja na huko Amani na Mashamba ya Mkonge. Huko Kanda ya ziwa Kuna kiwanda Cha nguo alitaka kung'oa sijui akipeleke wapi mwisho wa siku Serikali ya mkoa ikagoma akatulia.

Kwa UJUMLA HATA HAPA MO DEWJI ALIPO FIKA NIKWA SUPPORT YA SERIKALI eidha kwa serikali kujua ama kuto kujua. Kwa ujumla Mo Dewji hakuna alicho Anza from scratch. Mikopo mikubwa anachukua kwa kupitia Mali za serikali alizo zibinafaisha (majengo na Mashamba).

Wachina walitaka kukichukua kiwanda Cha AfriTex lakini akaleta mizengwe yake wachina wakaachana wa hilo jambo. MUTEX ya Musoma, kabomoabomoa mashine kule akazileta Tanga. Kule akabakiza gofu,spea akaleta Tanga kule kiwanda kikafa.

Sasa Forbes na wapimaji wengine wa utajiri wakipima hizo rasilimali alizo nazo ni utajiri mkubwa. Mo Dewji halimi korosho ila ni middleman. Azam ana kiwanja Cha sukari na amelima kilimo Cha miwa from scratch. Kama Magufuli alivo mwita Azam na kumpa eneo kubwa la kilimo free kabisa Ili atosheleze chai nchini, ndivo hivohivo serikali nyingine Duniani zinafanya kuwatengeneza matajiri wa ndani.

Nashauri kwa sasa tuweke nguvu zaidi kwa Black Colour (The Native).
 
The first to comment, mkuu huna paragraphs wala space between the lines, baadhi ya watu( wengi) umewapa shida sana na itakuwa ngumu kwao kusoma
 
Wahindi wana fitna sana, inauma sana wao wanatoboa nchini kwetu angali sie tunashangaa tu..

Wamehodhi biashara nyingi sana, wahindi wanakitu wanakiita “Spider web economy” yaani kile kinachoingia kwao hakika kisitoke kwenda kwa mweusi bali kizunguke hapohapo kwao (Indians).

Wavietnam walikuja wakawaletea wamakonde bei nzuri ya korosho, wahindi wakakosa korosho sababu ya bei yao ya kulalia mkulima. Mwisho wa siku Mvietnam akapigwa kila aina ya vita na majungu, leo hii Muhindi ananunua mwenyewe korosho na mwisho wake ndio hizi bei za 1000 tunazosikia huko..​
 
Hivyo viwanda unamvyomnanga Dewji viliporwa kwa makampuni kwa neno la kisiasa la "utaifishaji" na Nyerere kupitia azimio lililofeli la Arusha mwaka 1967 sijui 1968

Utaifishaji ulikuwa ujambazi wa kupora kwa kutumia mabavu ya dola wakataifisha nyumba na mali za hao hao ambao leo pia ndio matajiri pia
 
Hivyo viwanda unamvyomnanga Dewji viliporwa kwa makampuni kwa neno la kisiasa la "utaifishaji" na Nyerere kupitia azimio lililofeli la Arusha mwaka 1967 sijui 1968

Utaifishaji ulikuwa ujambazi wa kupora kwa kutumia mabavu ya dola wakataifisha nyumba na mali za hao hao ambao leo pia ndio matajiri pia
Moo akisimama yeye kama yeye bila hizo rasilimali Hana utajiri hata nusu ya Azam.Ukweli ndio huo.Serikali iwekeze kwa Native kwa sasa.
 
Huu uandishi wako wa kuandika waraka mrefu bila kutengenisha aya ni kutukosea adabu sisi raia wenzako tusio na hatia.
 
Tatizo la watu weus wivu,chuki, hakuna anaependa maendeleo ya mwenzake kuanzia kwenye familia hata kwenye serikali yenyew itamuonea wivu na akifanikiwa sasa asalaaaaale! Wote waliomuwezesha mbwa hakun mtu kama yeye acha hao waarabu na wahind watawale tu sekta ya uchumi
 
Shida kwa Blacks inaanzia kwenye familia. Huwezi jenga jamii imara kama unafamilia dhaifu. Hapo kunaswala la succession au kurithishana biashara kutoka kizazi kimoja kuja kingine.

Leo hii mtoto akimaliza shule say form 4, six au chuo akakosa ajira, akaamua kutaka kusimamia mali za familia lets say nyumba za kupanga, biashara ya duka, shamba au mifugo, mzazi na ndugu zake huanza kumuona analeta tamaa ya mali za familia na kuanza mshambulia atafute mali zake binafsi.

Hapo ndipo yale maneno ya "mtegemea cha ndugu hufa masikini"," toka katafute chako acha kutegemea urithi" etc. Haya maneno hukatisha tamaa na kurudisha sana nyuma jitihada za wale watoto wenye vipaji na uwezo wa kuendeleza mali za familia na kuzidouble na kujenga utajiri wa ukoo.

Ndio maana Afrika ni mara chache sana utajiri kukua kupitia vizazi yaani baba kwenda kwa mtoto then mjukuu na vitukuu. Biashara na mali nyingi hufa na kuzikwa na muasisi sababu ya haiba za ubinafsi kwetu waafrika.

Unakuta mzazi anamletea upinzani mtoto wake wa kumzaa anapotaka kutake over biashara na kusimamia kwa kumwambia "Nakusomesha ukazane na masomo yako upate elimu utafute kazi uje kutafuta mali zako usitake hizi za urithi"

Hawa wazungu ambao katika jamii yao wapo vema sana hawakuamka tu na kuwa na uwezo wa kifedha na kiuchumi bali walipitia hii hatua ya kurithi na kusimamia biashara za familia na kushika speed.

Baba kama ukinunua mashamba na kujenga nyumba then waachie watoto washike na kuendeleza maana hiyo ni akili mpya na wataona maisha katika sura mpya na sio ya kizamani kama yako. Wataweza tumia hizi rasilimali kufanya mabadiliko na kuja na idea mpya za kibiashara au kiuwekezaji na kuleta mapato makubwa sana.

Then watakuja wajukuu, watapoona babu aliachia watoto wake na wakashirikiana nao watarithi huo utamaduni wa kushiriki ujenzi wa uchumi wa familia then wataendeleza walipoishia watoto wa babu yao na wao kutakeover family business na ikifikia hapo tayari mamilionea watakuwa wameshafikia hatua nzuri.

Cha msingi ni kusisitiza, discipline ya kujituma kufanya kazi ubunifu na kulinda asset za familia. Kuweka mbali tamaa na ubinafsi ila kushare na kusaidiana zaidi bila kuegemeana au kuwekeana mizigo.
 
Huwa mkikosa akili mnakimbilia ooh sio afya kwa usalama wa nchi
Hivi mna nini cha kuogopa katika nchi mpaka muwaogope wenye asili za nje?

Nchi nyingi sana zinaongozwa na wakuja zaidi ya wazawa au wenye asili ya hapo

Mtu mweusi ni shida wala tusilaumu mtu na kusema eti kwa usalama sio nzuri wakashika uchumi

Angalia [emoji631] matajiri wakubwa wengi sana wana asili ya Kiyahudi
[emoji636] Tajiri wa kwanza ana asili ya kihindi anaitwa Hinduja

Sasa hapo ndio mataifa makubwa hayo mbona hatusikii malalamiko ya kiusalama?

Huwa mnashindwa kujua mnakwama wapi
Lakini watoto wenu wakiacha wizi na uongo mtakuwa na Taifa zuri tu

Umeona watoto wa kihindi vijiweni?
Wakitoka shule wanaenda kuuza duka na waarabu wengi hivyo hivyo sasa kuleta hoja ya kiusalama ni udhaifu wetu tu

Siku mkiacha wizi, uzinzi wa kujisifia
Unakuta uzi wa ngono unachangiwa zaidi ya page mia 3 ila wa biashara hakuna zaidi ya kejeli

Latin America kuna nchi 11 zenye maraisi wenye asili ya kiarabu yes waarabu na wanatawala Latin American countries [emoji1]

Na hilo utalisemaje? Kwanini wamekuwa Marais? Walikwenda kama wafanyabiashara na kwa sababu ya uaminifu wakaaminiwa na kushika madaraka

Leo Bashe tu anatukanwa
Badilikeni la sivyo nchi itakuwa na wazawa masikini mpaka mwisho wa Dunia

Arable land yote hiyo bado mnalalamika njaa umejiuliza kwanini
Au MO na Bakhresa ndio wanaiba mahindi
 
Habari ndugu zangu,

Naishauri serikali iweke vipaumbele vya kutengeneza matajiri wazawa weusi wenye asili ya ndani ya nchi tokea enzi za mababu. Mfano kama kwa Nigeria alivo Aliko Dangete,au hapa kwetu the Late Reginald Mengi...
Magufuli alianza na Reginald Mengi na alikuwa anakwenda kumaliza matajiri wengine wa huko Kaskazini akiwatumia akina Sabaya na wengine lakini watu wale wakamshtukia mapema wakampiga stop!

Ni ngumu sana hayo unayopendekeza kutokea hapa Tanzania. Nyerere naye alifukuza matajiri wengi tu na kuwafilisi matajiri wazawa. Kwa viongozi wabovu kama hawa wazo lako haliwezekani.
 
Back
Top Bottom