Tutumie sarafu za mtandaoni Cryptocurrency au Tutumie sarafu moja ya jumuiya ya Afrika Mashariki?

Tutumie sarafu za mtandaoni Cryptocurrency au Tutumie sarafu moja ya jumuiya ya Afrika Mashariki?

Joined
Mar 15, 2018
Posts
26
Reaction score
36
MG_9866-750x536.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, wakati wa uzinduzi wa jengo jipya la Benki Kuu ya Tanzania jijini Mwanza, aliitaka Tanzania kujiandaa na matumizi ya sarafu za mtandaoni au Cryptocurrency.

Ambapo alitoa wito kwa Benki kuu ni vema waanze kufanya kazi za maendeleo hayo. Lakini turudi nyuma kidogo, ilikuwa mwaka 2008 wakati ambapo kulikuwa na anguko zaidi la kiuchumi kote duniani. Mwanauchumi Satoshi Nakamoto, akaandika waraka wake kwa anwani 'Bitcoin - peer to peer - Electronic Cash System' akiutambulisha mfumo mpya wa fedha unaohusisha mtu kwa mtu, ama taasisi kwa taasisi bila mhusika wa kati.

Bitcoin ni fedha ya kidigitali ambayo huondoa uhitaji wa waamuzi na wasimamizi wa fedha kama benki na serikali na badala yake kutumia mtandao wa kompyuta zenye uwezo wa kuthibisha manunuzi moja kwa moja kati ya watumiaji.

Kwa kawaida fedha husimamiwa na Benki kuu pamoja na serikali lakini tukija kwenye swala la Bitcoin yenyewe husimamiwa na watu tofauti tofauti walio katika mtandao wa kompyuta zinazotumia cryptograpy ambayo ni aina ya ulinzi wa taarifa zinazoweza kusomwa na mtumaji pamoja na mpokeaji tu. Fedha hii ya kidigitali hutumia teknolojia ya Blockchain katika kufanya miamala.

Unapokuwa unatuma fedha kutoka kwa mtu A hadi mtu B, ama kutoka kwa Benki A hadi Benki B, lazima ziende kwa Benki Kuu. Au kama ni mobile money, lazima zipitie kwa wale ambao wamewapa huduma. Lakini Cryptocurrency inahakikisha fedha zinatoka kwa mtu mmoja hadi mwingine bila kupitia mtu kati, ambaye hufanya gharama kuwa juu Zaidi.

Kwa upande wa pili tukizungumzia sarafu ya Afrika Mashariki ambapo moja kwa moja narejea Moja ya sarafu zilizofanikiwa katika jumuiya mbalimbali duniani ni pamoja na sarafu ya Euro ambayo imekuwa ikitumika bara la Ulaya katika nchi mwanachama ili kuhakikisha lengo la kukuza uchumi kwa wanachama kupitia shughuli za kibiashara, uwekezaji na uchukuzi zinafanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Mchakato wa kuanzisha umoja wa fedha unaolenga kuanzishwa kwa sarafu moja kwa nchi za wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulianza Januari 2011 wakati majadiliano kati ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kuandaa itifaki ya kuanzisha umoja wa fedha yalipoanza rasmi. Majadiliano hayo yalikamilika mwezi Julai 2013 na itifaki ya kuanzisha umoja wa fedha kupitishwa na Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki Novemba 2013 katika mkutano wa 15 wa wakuu hao uliofanyika jijini Kampala.

Faida itakayopata Tanzania kutokana na umoja wa fedha na hasa kuwepo kwa sarafu moja ya jumuiya ya Afrika Mashariki ni pamoja na; Faida itakayopata Tanzania kutokana na umoja wa fedha na hasa kuwepo kwa sarafu moja ya jumuiya ya Afrika Mashariki ni pamoja na; Kupunguza gharama za kufanya biashara katika nchi wanachama na hivyo kuhamasisha ukuaji wa biashara kati ya nchi wanachama na ukuaji wa uchumi kwa ujumla.

Kwa kuwa na sarafu moja, umoja wa fedha utaepusha athari za ubadilishaji wa fedha ndani ya jumuiya. Kuwezesha nchi wanachama kuwa na kiwango kidogo na tulivu cha mfumuko wa bei. Kuwezesha nchi wanachama kuwa na viwango vidogo vya riba vya kukopa. Kutumia sarafu moja kutaleta uwazi katika bei na hivyo kuongeza ushindani wa soko ndani ya jumuiya.

Kwasasa wadau sijaelewa kauli ilitolewa na Rais kuwa tujiandae na Cryptocurrency kuwa italeta maendeleo makubwa ya maendeleo ya uchumi au serikali iendelee na mchakato wa kutafuta sarafu moja ya jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa italeta maendelo ya uchumi Afrika Mashariki hususani Tanzania.
 
Back
Top Bottom