Sifa zake:-
1. Awe ni rais mstaafu wa JMT mkongwe kuliko wote.
2. Awe amehudumu kiti cha urais kwa mihula 2 (miaka 10).
Majukumu yake.
1. Kuridhia maamuzi ya serikali juu ya uuzwaji ama ubinafsishai wa rasilimali za nchi.
2. Kumpa ushauri rais juu ya masuala yote yahusuyo nchi.
3. Kumuwajibisha rais (kumfuta kazi ) endapo atakiuka katiba ya nchi.
Baraza la ushauri la kiongozi mkuu litaundwa na watu wafuatao:-
1. Marais wastaafu (ambao ni junior kwa kiongozi mkuu)
2. CDF wastaafu {wote walio hai (w.h)}.
3. VP wastaafu (wote w.h).
4.. PM wastaafu (wote w.h).
5. Spika wastaafu (wote w.h).
7. Majaji wakuu wastaafu (wote w.h)
8. IGP wastaafu wote wote w.h
9. DCI wastaafu wote w.h.
Kwa kuwa mihimili ya bunge na mahakama imekanyagwa na executive, na kumfanya rais kuwa Mungu mtu, basi ofisi hii ndiyo iwe kizingiti cha maamuzi ya hovyo ya rais yeyote aliyeko madarakani.
Haiwezekani atokee rais mmoja mshamba huko, kachaguliwa kimihemko (mf. Jiwe) ama kapata kiti kwa bahati mbaya (mf. Mama) anaanza kuipeleka nchi pabaya halafu hakuna wa kumzuia.
Tuazimie sasa na tuanze na rais mataafu Kikwete awe ndiye ayatollah wetu wa kwanza.
Hizo sifa mkuu hazitoshi kabisa,na niweke wazi, Kikwete hana sifa kimaadili ya kuwa kiongozi mkuu wa nchi.Pamoja na nyingine nyingi,lakini maadili mazuri lazima iwe sifa ya kwanza.Ili kuweza kupata mtu wa namna hiyo,ni lazima ifanyike sample survey kwenye main religions:Ukristo na Uislam, ili kuona ipi dini ina maadili mazuri zaidi,than from that religion, atoke kiongozi huyo.
Idadi ya Washauri is debatable,lakini hao pia ni lazima wawe na moral values zinazokubalika,hiyo iwe sifa ya kwanza.
Ni kweli kwa sasa inaonekana kama Rais ana too much power na ni kama kuna vurugu ya aina fulani hivi,na hii sio afya Kwa Taifa.Ni wazi we need some moderation in the Presidents' powers.Samia anayofanya can even cost us politically.Hapana, Rais hawezi kufukuza hovyo hovyo namna hii.
Wazo lako ni zuri,ila we can coin another name,sio Ayatollah,naamini jina hilo ni affiliated to Islam na lina maana kwenye Uislam.Kiongozi huyo tunaweza tukamuita Rais,halafu mtendaji mkuu wa nchi akawa Waziri Mkuu,kama ilivyo in some countries around the World.