Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,768
- 49,949
Rejea sheria mpya ya uchaguzi, Rais Samia, Serikali ya CCM na Bunge bandia la CCM, waliwadharau na kuwapuuza Watanzania wote.
Vyama vya upinzani, taasisi za dini, chama cha wanasheria Tanganyika, watetezi wa haki, na asasi za kiraia, wote walishauri:
1. Kuwe na Tume Huru ya uchaguzi ambayo haiteiliwi na Rais
Rais Samia, Serikali yake na CCM, walipuuza maoni ya wananchi, tena wakawaona ni wajinga. Tume ya uchaguzi ikabakia kuwa chini ya Rais, lakini wakabadilisha tu jina kuwa iitwe TUME HURU YA UCHAGUZI. Hii ni dharau kubwa kwa Watanzania. Tukatae kudharauliwa na kufanywa punguani wa akili.
Jibu ni NO REFORM NO ELECTION.
2. Wadau wote walitoa mapendekezo kuwa ushetani wa wasimamizi kuwaengua wagombea wa upinzani, ukome; na kwamba watumishi wa umma wasisimamie uchaguzi.
Samia, Serikali yake na CCM, kama ilivyo kawaida yao waliyapuuza mapendekezo ya wadau, wakaweka kwenye sheria kuwa eti msimamizi wa uchaguzi asiruhusiwe kuwawekea pingamizi wagombea, ila wapiga kura na wagombea wawe na uhuru wa kuwawekea mapingamizi wagombea.
Hii yote wakilenga kuwapandikiza wapiga wapiga kura wa kuwawekea pingamizi wagombea wa upinzani, kisha msimamizi wa uchaguzi aendelee kuwaengua wapinzani kwa kigezo kuwa wamewekewa mapingamizi na wapiga kura. Mbinu zao hizi za kishetani wanaamini hakuna wa kung'amua kwa sababu wanawadharau Watanzania na kuwaona hawana akili. Tusikubali kufanywa hatuna akili.
Jibu: NO REFORM NO ELECTION.
3. Wadau walipendekeza kusiwepo na mtu wa kupita bila kupingwa. Samia, CCM na Serikali yao, kwa dharau zilezile, wakasema eti hakutakuwepo na kupita bila kupingwa. Akibakia mgombea mmoja, apigiwe kura ya NDIYO au HAPANA. Cha ajabu huyo mgombea anayepigiwa kura anakuwa na wakala, lakini wanazuia mtu yeyote kuwa wakala wa kuhakiki hizo kura. Hivyo kura zote za HAPANA zinaweza kubadilishwa na kuwa za NDIYO, na hakuna wa kupinga. Hapa umebakia ushetani ule ule wa kuenguliwa wapinzani, kisha mgombea wa CCM kutangazwa ameshinda kwa kura za NDIYO, wakati kiuhalisia ushetani umebakia vile vile.
Tusikubali kufanywa taahira. Tusimame pamoja kwa nguvu zetu zote.
NO REFORM NO ELECTION ni mpango wa kuliokoa Taifa kutoka kwa wahuni. Ni wajibu wa kila Mtanzania bila ya kujali ni wa chama gani. Tulipende Taifa letu, tujenge msingi mzuri wa haki wa Taifa letu.
NO REFORM NO ELECTION ni kauli ya hamasa, lakini lililo kubwa ni kuwa tunatakiwa kuvunja mifumo yote ya kishetani katika Taifa letu, inayowafanya wananchi wadharaulwe na kufanyiwa uharamia wa kunyimwa haki zao na kikundi cha waovu wachache.