Tuwaache abiria wa daladala washuke kabla ya sisi kupanda

Mbagala rangi 3 hyoooo...
😁😁😁😁😁😁😁😁
 
Shukurani zangu zikufikie kwa kutusitiri sisi tusio wasafiri tunaoziba mlango ili tupate maokoto, ila ushauri wako utatulaza njaa.
Konda hakai mlangoni kwa bahati mbaya, yeye na sisi wa maokoto ni kundi moja, ni spidi gavana wa kuwanana abiria wasipande kwa haraka, tunachokipata naye tunamgawia.
 
Wiki iliyopita hapo hapo mawasiliano nimekaa mwanzoni nasubiria gari za mbezi watu kibao na mm Nina mzigo kusimama ni masihara maana bongo ni tanuri,basi nikaapa hata dirishani ntaruka,Ile inafika Costa konda akaweka gadi kuwa ndani Kuna wabibi vikongwe wawili inabidi washuke ndio raia wapande,basi raia waliofika wakaanza kushuka huku wengi wakiusifia ustaarabu huo.
Kosa la wale wabibi wakawa wamwisho kutoka na wakawa wanatembea taratibu Ile wanafika mlangoni ikatoka sauti ya muhuni aliyekuwa pembeni.."kwanza hao ndio wanga wenyewe,hebu wasitucheleweshe."
Kilichofua pale ni aibu kuadithia ila ni seme tu wale vikongwe were tough than I thought,la sivyo mngepata habari ITV
 
Mkuu tabia ya nigger haibadiliki ndo inazidi kuwa mbaya.
 
Utamaduni wa Daresalama huo , hautabadilika πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Acha kulegea legea,njoo huku mbagala gari ikisimama unakuta mrembo kavaa taiti ya jinsi anaruka dirishani
 
Nani alitufikisha hapa? Namkumbuka miaka hiyo ya UDA, huu ndio ulikuwa utaratibu, mnapanda Kwa foreni, with exceptional Kwa wazee na wagonjwa.

wahuni sijui walitoka wapi nchi hii mambo yakaenda kombo.
 
Cha kwanza ni kusimamia level seat tu.
 
Ni kutokuwa wastaarabu tu
Mnahitaji kuwa na subra, sijui kwanini wengi wa watu ustaarabu zero
Kwani mkipanga foleni mnapungukiwa nini
Mtanzania ustaarabu sifuri kbs
Wakati wa kupanda wanagombania,kushuka wanagombania yaan wako
Kama mangombeee

Ova
 
Ustarabu wa kupanda kwenye magari labda uanze kufundishwa chekechea.

Wabongo wamezoea ikisimama wanapanda juu
 
Maeneo wanayogombea siti kuna vijana wa stand akiwahi siti anamuuzia mtu anayehitaji kukaa,utaratibu wa hovyo kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…