Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,236
- 10,774
Imekuwa ni kawaida kukutana na video na picha zikionesha maisha ya ndugu zetu Wahadzabe wakiwa wanawinda na kutafuta chakula, huku zingine zikituonesha upekee wa lugha yao ambayo ni moja ya utajiri mkubwa sana wa lugha zaidi ya 1000 zinazopatikana ndani ya bara letu la Afrika.
Lakini katika video hizi zipo video ambazo zinaonesha namna watu kadhaa wakiwapatia Wahadzabe vitu ambavyo kwao ni vigeni kabsa. Vitu kama Pombe kali, Sigara pamoja na Vyakula vilivyosindikwa kama Burger, na vingine.
Hii imetokana na mwingiliano mkubwa kati ya Wahadzabe na watu kutoka nje ya jamii yao. Wengi wakiwa ni watalii, watafiti na hata mashirika yasiyo ya kiserikali wamekuwa wakiwafikia kwa madai ya kuwasaidia.
Watu hawa huwapelekea dawa za kisasa, vyakula vilivyotengenezwa viwandani (vilivyosindikwa) pombe, na hata kuwafundisha kuhusu “maisha ya kisasa.” Kwa mtazamo wa haraka, inaweza kuonekana kama msaada mzuri, lakini kwa undani, huu ni mwanzo wa kuangamia kwa utamaduni wa Wahadzabe.
Kwa kuingiza vitu hivi vya kigeni katika maisha ya Wahadzabe, tunaharibu mfumo wao wa maisha wa asili kabsa, tunapunguza thamani ya maarifa yao ya jadi, na kuwafanya waone kana kwamba maisha yao si bora. Pombe na vyakula vya kisasa vimeanza kuleta madhara ya kiafya na kijamii, huku watoto wa Kihadzabe wakianza kupoteza mawasiliano ya moja kwa moja na mila na lugha yao.
Zipo video zikionesha wahadzabe wakipewa vinywaji vikali na watalii na wengine wakienda mbali na kuanza kuwachunguza miili yao. Mfano bora, ni yule bwana mdogo Dudukee kwa hakika huyu bwana ameshachizika kabsa na utamaduni wa dunia ya huku nje.
Wahadzabe hawahitaji kufanywa kama majaribio ya maendeleo wao sio specimens. Wanahitaji kuheshimiwa na kuheshimu maisha yao. Tunapaswa kujifunza kutoka kwao jinsi ya kuishi kwa uhusiano wa karibu na mazingira, badala ya kuwalazimisha kuiga mifumo ambayo haikuiendana na maisha yao. Dunia inapaswa kuona thamani ya utamaduni wao na kuhakikisha kuwa unalindwa kama sehemu ya urithi wa mwanadamu.
Kuwaheshimu Wahadzabe ni kuacha kuwalazimisha kubadilika. Tuwaache waamue kwa hiari yao kama wanataka kubadilika, na iwapo watahitaji msaada, basi uwe ni wa heshima, unaoelewa na kuthamini maisha yao ya asili pasipo kuwaharibia mtindo wao wa maisha.
Kwa namna watu wanavyoendelea kuwavuruga Dudukee na wenzake kwa hakika 2035, Wahadzabe watakuwa hawapo tena. Tuwaheshimu. Tuwalinde. Tuwaache waishi kama Wahadzabe.