Tuwachangamshe vipi wanaume wapole

Tuwachangamshe vipi wanaume wapole

Jamani kuna nyie wanaume wapole kupita kiasi yaani wapole sana tufanye nini ili angalau muwe kawaida

Unakuta mwanaume ndo imeshatokea mna mahaba sasa ila hajiongezi yupoyupo hana michezo ya ajabu yaani hana maajabu yoyote

Yaan mpaka kuna muda mtu unahisi yan hapa nilijitongozesha maana unakuta kijana kimya, hela ndo mdomo wake kila unachomwambia anasema sawa habishi hakatai ukisalimia anajibu hana nyongeza ya neno.

Ukileta utani kidogo anacheka haongezi, utani mwengine yaan utajikuta umegeuka kiredio chake kama Huna story mnaweza mkakaa kimya hadi mnuke midomo.

Huyu mwanamme mpole anachojua ni kufunuana usiku tu aibuuu anazo yeye upole anao yeye yaan inagharimu furaha yoote mtu uliokuwa nayo.

Ndio tunapenda wanaume watulivu lakin utulivu ukizidi ni keroo
Sasa tuwachangamsheje jamani angalau mlete amsha amsha
Mimi mwenyewe sipendi mwanamke aliyezubaa hata kidogo
 
Kwenye hela hawa watu ni hatari Sana. Kuna mmoja nimejuana nae ndani ya wiki iliyopita kitu Kama Alhamisi, baada ya kuwa single kwa muda nikaona ngoja nipate mtu wa kupunguzia majanga haya. Aisee mpaka Leo ashanilamba Kama kilo tatu hivi. Na bado sijaonesha hata nia ya kumtongoza imebidi nichange gia angani.
Anakupima nguvu za kiume😁😁😁😁....
 
Tukichangamka Sana mnatuita machepele,Bora tuwe wapolee tu🤷🤷🤷
Wewe, niliwahi kujisogeza karibi na binti flani, nikamwalika dina huku nikijiandaa na uvuvi...wee dada amepoa kama maji ya ziwa magadi...
Baada ya msosi nikamrudisha kwao na sikumtafuta tena😂😂😂😂 upole kupitiliza unaboa
 
Tukichangamka Sana mnatuita machepele,Bora tuwe wapolee tu🤷🤷🤷
Hii inatokea kwangu tu jmn??
Screenshot_20230518-204749_Chrome.jpg
 
Back
Top Bottom