Hao wote hamna kitu wote ni watu wa kuongeza 0Pedeshee Chief kiumbe, papa misifa, papa mo,
Bora yule binti yake diagi amesoma nadhani Yuko nssf sasa hivi at least Yuko vzrIdd janguo yupo kinondoni tu
Katuliaa hakuna hela za baba sahv
Anafanya kazi
Ova
Ndo nauona umenikumbusha mbaali Sana daahhAwali ya yote nitangulize angalizo kwa vijana ambao maturity stage imewakuta miaka hii ya mitandao ya kijamii. Itabidi msome kimyakimya huku mkiwa mmeshika peni na karatasi kuchukua notes.
Huu uzi ni wa sisi ma-seniors, maudhui yake yatagusa zaidi vijana wenzangu ambao maturity liwakuta kuanzia late 90s to early 2000s.
Mwaka 2002 mpaka 2012, mziki wa dansi ulikuwa upo kwenye prime time.
Kwa uchache tu, band zilizotamba ni FM Academia, Akudo Impact, Twanga Pepeta na Diamond Musica. Zingine zilikuwa zinaibuka na kupotea ndani ya muda mfupi.
Umaarufu wa hizi band ulienda sambamba na trend ya wanamuziki kutaja majina ya baadhi ya watu kwenye mashairi yao.
Majina ya hawa watu yalivuma na kuwa maarufu kuliko sura zao kwasababu miaka ile kulikuwa hakuna social platform za ku-share picha na video kama ilivyo hivi sasa.
Kutokana na kujichanganya kwangu ukijumlisha na ujanja wangu wa kimjini mjini wa miaka ile, nilifanikiwa kufahamiana na baadhi mapedeshee au wazee wa mujini ambao majina yao yalikuwa yanatajwa kwenye mziki wa dansi.
Nitataja ninaowakumbuka na wewe ongeza wa kwako.
Naandika majina yao kama yalivyokuwa yanatamkwa kwa mbwembwe na wanamuziki.
Kwa mfano kama mtu alikuwa anaitwa John, wanamuziki walikuwa wanatamka papaa John Young Millionaire Muzee ya ma-Range Rover[emoji3][emoji3].
Haya twende kazi:
Pedeshee Mychoice na kati ya Mbeya:
huyu sijui alikuwa anapiga mishe gani huko Mbeya, watu wa Mbeya mtatusaidia.
Braza K na kati ya Tunduma:
Watu wa Tunduma mtatusaidia kutujuza kuhusu huyu jamaa, alivuma sana.
Mamaa Rukia Soloon:
Huyu bibie namfahamu, ana saloon yake ya kike mitaa ya Mikocheni barabara ya Rose Garden. Those days she was very pretty, kwa sasa utu uzima umemchukua.
Mamaa Dotnata Decoration:
Bila shaka wengi mnamkumbuka, aliwahi kuwa muigizaji maarufu kupitia ITV, baadae akaingia kwenye ujasiriamali wa kutoa huduma za catering, shughuli hizi zilimpatia mafanikio sana. sijui kwa sasa yupo wapi huyu mama. FM Academia waliwahi kumtungia wimbo wenye jina lake.
Mamaa Juddy Moshi:
Alikuwa mmiliki wa band ya Daimond Musica kwa financial support ya mshua mmoja ambaye alikuwa ni MD wa Yellow Pages, watu wa zamani wanaelewa. Juddy alikuwa mrembo si kitoto, kwa sasa umri wake umesonga mbele.
Pedeshee Akayesu Ndama Mutoto ya Ng'ombe:
Sina haja ya kumuelezea, ni mtu maarufu wa nyakati zote. Wajanja wa mujini watamuelezea zaidi. Jina lake lilitajwa sana kwenye nyimbo za dansi zilizovuma.
Young Millionaire Bill gate Muzamir Katunzi:
Christian Bella aliwahi kutunga mpaka wimbo wenye jina hilohilo la Muzamir Katunzi. I don't know him personally, but it's told he was financially successful.
Papaa Msofe Chuma cha Reli hakishiki Kutu.
Sina haja ya kuandika mengi kuhusu umaarufu wa Papaa Msofe. Itoshe tu kusema jina lake liliimbwa sana halafu ni wachache waliokuwa wanajua sura yake. Walianza kuiona kwenye media alipokuwa anahudhuria viunga vya mahakama kujibu kesi yake.
Papaa Martin Kasianju.
Ni marehemu kwa sasa, huyu mshua ndio alikuwa mmiliki wa Band ya FM Academia. Nilikuwa namfahamu personally. licha ya kwamba alikuwa ni mjasiriamali na muajirwa Serikalini, pia alikuwa ni Senior Officer wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Andrew Traders na Kariakoo Big Supply: Jamaa alikuwa ni mfanyabiashara wa kuuza tairi za gari Mtaa wa Agrey Kariakoo huku akipiga michongo yake ya "general supply". Watu wa mujini wa zamani wanaelewa vizuri maana ya kampuni kusajiliwa kwa jina la general supply. Katika biashara ya kuuza tairi, alishirikiana na kaka yake, ila yeye akawa maarufu zaidi na akaaminika na wadau.
Kinje Mutoto wa Mujini:
Najua wengi mnamfahamu na zile deal zake alizokuwa anapiga. sina haja ya kumuelezea zaidi.
Pedeshee David Kabunga:
Sifahamu alikuwa ni nani, jina lake lilikuwa linatajwa sana.
Papaa Ally Kileo:
He was a prominent lawyer in town, jina lake lilikuwa linatajwa sana kwenye nyimbo za dansi.
Papaa Mutarika Mzee wa Mambo mengi:
Binafsi simfahamu, wajanja wa mujini wa zamani watajazia nyama kumuelezea.
Chef Justice Rugaibura:
Binafsi simfahamu, wajanja wa mujini wa miaka ile watajazia nyama kumuelezea.
Chief Kiumbe le Big Boss:
Anafahamika vizuri, jina lake lilitajwa na kuimbwa sana na wanamuziki wa band. wajanja wa zamani wa mujini watajazia nyama kumuelezea
Papaa Amos Makalla mzee wa Mvomero:
Kwa sasa ni RC wa Dar, jina lake lilianza kuvuma kitambo sana kabla hata hajaingia kwenye siasa.
Fikiri Madinda Mukuu wa kazi: Anafahamika vizuri, wajanja wa zamani wa mujini watajazia nyama kumuelezea
Pedeshee Abdul Mkeketa:
Huyu wakati fulani aliwahi kuwa mbunge ktk Mkoa wa Morogoro, sikumbuki ni jimbo gani. kwa sasa ni marehemu.
Charles Mutawali Muzee ya Magari.
Binafsi simfahamu, wajanja wa zamani wa mujini watajazia nyama kumuelezea.
Saidi Mukuu wa lumumba:
Jamaa alikuwa dalali wa kuuza magari pande za Lumumba.
Meddy Kitendawili....?
Ben Mulokozi....?
Salim Chicago Matelefone...?
Kizaizai....?
Omary Tolu...?
Abduli Tolu...?
Joshua Limited...?
Muddy Nyamalonda mzee wa Pamba...?
China wa China...?
Shaibu Mapajero....?
Moris Mariaga Rais wa Sinza...?
Ntenze wa Ntenze....?
John Nzenze....?
Papaa Madenge....?
Note of Appreciation.
sikujua kama huu uzi ungewavutia watu wengi kiasi hiki. niwashukuru wote mnaoufatilia na mnaochangia maoni yenu. asanteni sana wadau.[emoji1431][emoji1431][emoji1431][emoji1431]
Hakua na issue yoyote aliku anakaa kwao kota mpk anazeeka..Pedeshee Jimmy Chocolate aliimbwa na marehemu Ndanda kasovo, uyu bwana alikua na mishe gani mtujuze watu wa uko Dar tujue sisi watu wa Bariadi tulikua na Pedeshee JOHN CHEYO, A.K.A MAPESA
Hapana! Mziki wa dansa ulikata kitambo sana.Kilivyoingia chuma pale Ikulu ndio ikawa mwisho wa hao watu. Huku ikisemekana walijipatia ukwasi nje ya mstari sahihi.
Na ndio ikawa mwisho wa mziki wa dance hapa nchini hadi sasa. Maana walitegemea udhamini wa hao watu.
Fomu za kuomba viza kina Mtambo si ndio dili yao kuwajazia watu?Hawa jamaa wasiojua kusoma na kuandika uwaga wajanja wajanja sana, ila nafikiri hicho ni kipaji fulani mungu kawapatia. Kuna jamaa tuko nae huku mamtoni pande za kwa Biden ni mtoto wa Kariakoo, jamaa hajui kusoma wala kuandika ila mayai anayatema utadhani muamerika na kazi anayofanya ni driver taxi. Sasa uwa najiuliza alipataje pataje viza??? Na yupo USA kitambo toka early 2000s. Ana familia na anaishi vizuri.. kimbembe aletewe barua lazima aniletee nimsomee na kuijibu lazima nimuandikie, jamaa ni mjanja mjanja sana huyo Kizai zai anasubiri.
Haji Mbabe...?Ben Mulokozi....?
Salim Chicago Matelefone...??/
Kizaizai....?
Omary Tolu...?
Abduli Tolu...?
Joshua Limited...?
Muddy Nyamalonda mzee wa Pamba Kali...?
China wa China...?
Shaibu Mapajero....?
Moris Mariaga Rais wa Sinza...?
Ntenze wa Ntenze....?
Mtu aliyekuwa anampenda Ibilisi Jahiri Magufuli basi ujuwe huyo mtu ni mchawi.I
Ukitaka kukosana nao na hata wanaweza kuzila ofa uliyowapa watajie tu jina la Jiwe na utawala wake
Kuna mwingine very smart ila ukimuandikia message lazima akupigie.Jamaa wakanisanua hajui kusoma.Hawa jamaa wasiojua kusoma na kuandika uwaga wajanja wajanja sana, ila nafikiri hicho ni kipaji fulani mungu kawapatia. Kuna jamaa tuko nae huku mamtoni pande za kwa Biden ni mtoto wa Kariakoo, jamaa hajui kusoma wala kuandika ila mayai anayatema utadhani muamerika na kazi anayofanya ni driver taxi. Sasa uwa najiuliza alipataje pataje viza??? Na yupo USA kitambo toka early 2000s. Ana familia na anaishi vizuri.. kimbembe aletewe barua lazima aniletee nimsomee na kuijibu lazima nimuandikie, jamaa ni mjanja mjanja sana huyo Kizai zai anasubiri.
Wazaramo wa Kisarawe wanamkumbuka mpaka sasa..... Hahahaaa...Mzee Janguo baada ya kutoka Bandari alikuwa mbunge wa Kisarawe.
Umenikumbusha kwenye nyimbo nyingi za marehemu Madilu System, amemtaja sana Pedeshee Emmanule Sammuele.... Mpaka Kuna wimbo nadhani unaitwa hivyo... Naupenda sana wimbo huu.....drc ndio nchi inayoongoza kuwa na mapedeshe maarufu wanaotajwa sana katika nyimbo za rhumba.
nje ya umaarufu wao, watu hawa ni matajiri kwelikweli. wameendelea kabaki ktk himaya zao za utajiri kwa muda mrefu.
hapa nazungumzia majina ya watu wazito kama adam bombole, tchatcho mbala, moise katumbi chapwe, mamaa tabou fatou na wengineo.
miaka ya hivi karibuni pale kinshasa ameibuka kijana mmoja wa kiarabu mwenye asili ya lebanon anayekwenda kwa jina la abed achour.
abed ni kijana tajiri sana, amekuwa msaada mkubwa ktk kuwapromote na kuwawazesha baadhi ya wanamuziki vijana wa mziki wa rhumba.
jina lake linaimbwa sana siku hizi.huyu hapa ktk video.
View attachment 2273822
Tunamkumbuka kama Shujaa wetu na mtu mwenye mapenzi ya kweli na kisarawe alikuwa mkurugenzi wa Bandarini ila Faida yake mpk Leo baadhi vizazi bado ipo sio yule bwana waziri anafaida yeyote zaidi ya kuongeza wake... Tunamsubiri kwa Hamu 2025...Wazaramo wa Kisarawe wanamkumbuka mpaka sasa..... Hahahaaa...
Huwezi amini kaka ake ni fundi viatu vibovu na ndala zilizokatikaIla alimfaidi sana Aisha, wacha asiwe na kitu, Madinda trans.
Hahahahaaa... Mkuu, nasikiasikia...Tunamkumbuka kama Shujaa wetu na mtu mwenye mapenzi ya kweli na kisarawe alikuwa mkurugenzi wa Bandarini ila Faida yake mpk Leo baadhi vizazi bado ipo sio yule bwana waziri anafaida yeyote zaidi ya kuongeza wake... Tunamsubiri kwa Hamu 2025...
Watu tunajisahau sahau sana hatukumbuki kama kuna kesho ni starehe tu kwenda mbele wengine ukiwa na pesa hukumbuki hata ndugu zako,kwa jamii ya kiafika kusaidia ndugu zako ndio uwekezaji mkubwa,naamini kama madinda angekuwa amewasaidia ndugu zake angalau angekuwepo mmoja wa kumtupia angalau wekundu wa msimbazi mara kwa mara, usiposaidia ikifika kesho wote mnakwama na kurudi kulekule mlikokuwa kabla ya kupata ngekewa ya kutembelewa na vijisenti, wapi Madinda, Madinda(kwa sauti yake) we fala(mhudumu) peleka pale krate haraka,hah haha haya maisha we acha tu.Huwezi amini kaka ake ni fundi viatu vibovu na ndala zilizokatika
Ukiwa na moyo wa kusaidia ndugu wewe wasaidie tu lakini usitegemee kama watakumbuka fadhiraWatu tunajisahau sahau sana hatukumbuki kama kuna kesho ni starehe tu kwenda mbele wengine ukiwa na pesa hukumbuki hata ndugu zako,kwa jamii ya kiafika kusaidia ndugu zako ndio uwekezaji mkubwa,naamini kama madinda angekuwa amewasaidia ndugu zake angalau angekuwepo mmoja wa kumtupia angalau wekundu wa msimbazi mara kwa mara, usiposaidia ikifika kesho wote mnakwama na kurudi kulekule mlikokuwa kabla ya kupata ngekewa ya kutembelewa na vijisenti, wapi Madinda, Madinda(kwa sauti yake) we fala(mhudumu) peleka pale krate haraka,hah haha haya maisha we acha tu.
kuna rhumba moja kali sana ya madilu system inaitwa vice versa.Umenikumbusha kwenye nyimbo nyingi za marehemu Madilu System, amemtaja sana Pedeshee Emmanule Sammuele.... Mpaka Kuna wimbo nadhani unaitwa hivyo... Naupenda sana wimbo huu.....
Yeah walikuwa wote siku hiyo, ilikuwa hatari aiseeNyoshi yuko na bendi yake Bogoz, ukimkuta yupo kwenye mood ni hatari tupu.