Nimekulia Sinza ile ya akina Remi ndio wanatamba na Volkswagen imeandikwa.''mambo kwa soksi'' tulikuwa tunajua karibu vijana wote, hivi sasa Sinza imebadirika ni Sinza ya magorofa,mahoteli,vijana wote wa zamani ama wamerudisha namba kwa Sir God ama wamehamia sehemu nyingine nje ya mji,nyumba nyingi tulizokuwa tunapanga chumba kimoja kimoja zimebomolewa na kujengwa mahekalu, nakumbuka pale sinza madukani kulikuwa na mbabe wa kikurya Lucky baba yake alikuwa usalama wa Taifa,namkubuka bibi Uliye alikuwa na mabinti kama 10 hatari sana, nakumbuka akina Banza stone wakiwa wadogo wakicheza disco mtaani, nakumbuka Vatican City ikiwa hotel kumbwa Sinza na Simba walikuwa wakiweka kambi hapo, namkumbuka Fred Mwalasha akiwa ametoka Ulaya na mke wa kizungu ikawa yeye ni bangi na bangi na yeye hadi mwanamke wa kizungu akamkimbia, siku hizi sinza yamejaa madangulo na wazee wale waliokuwa na nyumba ambazo tulikuwa tumepanga nao hatunao duniani ila zile nyumba walizoacha watoto wao wameziuza kwa matajiri na kwenda kunywea pombe na kula sembe. Sinza ya sasa si ile tuliyokuwa tunaitimba, ama kweli siku hazigandi.