Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Unaujua ule wimbo
Nimepoteza kipenzi changu hapa tanzaniaaa[emoji445]
Nimepoteza mkanda wa kiuono[emoji445]
Nitarudii kwa Hidayaa[emoji445] hidayaaa hidayaaa[emoji445]

Unaambiwa Hidaya alikua ni mrembo vibaya sana enzi za uhai wake akiwa kijana

Ilikua mama moja pisi kali ya Arusha, pepe kalee alifichwa hadi akanyoosha mikono, nadhani bado yupo alikua na mtoto mmoja wa kike aliuliwa na mume wake walikua wakiishi UK
 
mrangi funguka kidogo kuhusu muzamil katunzi. najua huwezi kukosa machache kumuhusu.
Hawa walianza ujanja tu toka zamani
Alipotoka bukoba alipokelewa na ndg
Yake,akamuwekaga kwenye duka la dawa kino studio
Alijua mambo ya mjinimjini
Msofe naye wote walianzia salamander mjini...mambo ya mihuri,pport etc
Huko ndiko walijua michongo mingine
Kwa mtoto wa mjini zamani lazima uende salamander,azam kutega ujue na kupata a,b,c,d
Nashanga sahv mtoto wa mjini anaonekana na kutambulika
Kisa anaenda kidimbwi
Mtoto wa mjini maana yake huko mjini
Unakutana na watu,viongozi wanakupata connection au wanakupa mchongo kwa kukutumia wewwe nk
Siku mtu kwenda Juliana kidimbwi
Anaonekana umjini

Ova
 
Kilivyoingia chuma pale Ikulu ndio ikawa mwisho wa hao watu. Huku ikisemekana walijipatia ukwasi nje ya mstari sahihi.

na ndio ikawa mwisho wa mziki wa dance hapa nchini hadi sasa. Maana walitegemea udhamini wa hao watu.
Hayo mengine sawa, ila kuhusu kukosa umaarufu kwa mziki wa dansi napingana na wewe.

Mziki wa dansi ulikuja kukosa umaarufu baada ya kuvuma kwa bongo fleva kuanzia miaka ya 2010 hivi.

Kabla ya mwaka 2010 ilikuwa ni nusu kwa nusu, yaani mziki wa dansi na bongo fleva ulikuwa unachuana katika mashabiki.

Chuma kimeingia ikulu 2015 huku mziki wa dansi ukiwa hoi bin taabani.

Hilo ni suala la kawaida katika fasihi. Nafikiri tunakumbuka kuna kipindi miaka ya 2000 hivi taarabu ilikuwa juu kuliko bongo fleva, enzi za Hadija Kopa na yule mama sijui alikuwa naitwa nani mpinzani wa kopa.
 
Ilikua mama moja pisi kali ya Arusha, pepe kalee alifichwa hadi akanyoosha mikono, nadhani bado yupo alikua na mtoto mmoja wa kike aliuliwa na mume wake walikua wakiishi UK
Alifariki hivi karibuni. Nadhani mwaka jana kama sijakosea. Baada ya binti yake alifuata yeye.
 
Reila Rashid nadhani, taarabu ilikuwa juu hata sisi wabara wagumu wa kanda ya ziwa tukaijua taarabu.
 
kulikua na wadau wengine sio mapedeshee lakini walipaishwa sana.

Chesco mzee wa matunda.
mama Mingoi.
Meja matunda.
Hassan Miundombinu R.I.P.
Swetu Fundikila R.I.P.
daladala camp.

mrangi ngoja niwa tag wakali wa donta.
Watuma salamu kina top manyota wa chabela camp, chacha muhiri Obare wa Igoma kwa wajanja, Lawena Nsonda wa Makongorosi Chunya nk.
 
Umemsahau papaa misifa,, diamond alikuwa anamtaja sana enzi hizo sasa nae kawa na hela hawataji tena kwenye nyimbo zake anawataja ndugu zake na wafanyakazi wake tu[emoji1787][emoji1787][emoji1787]dah maisha haya
 
@mrangi naelewa ni nini unazungumza kaka , big up tueleweshe vijana wa leo
 
Umenikumbusha late 90s nimemaliza O-Level, nipo home nasubiri majibu yatoke. mshua akanitafutia temporary job mitaa ya mjini posta kwenye ofisi ya rafiki yake.

Ofisi ilikuwa mtaa wa jamhuri jirani na ile round about ambayo inakutanisha india street na mkwepu street, almaarufu mitaa ya azam take away.

Ilikuwa kila ikifika mida ya saa tatu mpaka saa nne asubuhi, lile eneo walikuwa wanatokea mabroo smart kwelikweli kimuonekano. mkononi wamebeba vi-diary.

Walikuwa wanavaa mashati nadhifu, surauli za kadeti na viatu safi vya ngozi. kwa ujumla walikuwa wanapendeza sana, mimi mwenyewe nilikuwa nawa admire.

Siku moja nikamuuliza broo mmoja ambaye tulikuwa tunafanya kazi pale, kwamba hawa jamaa ni akina nani,mbona mda mwingi wanautumia kakaa kwenye vijiwe vya shoe shiners, hawana kazi ya kufanya?.

Akanijibu ukisikia mission town ndio hao, na hapo kwenye vijiwe vya shoeshiners ndio sehemu zao za kupanga mipango na kupeana deals mbalimbali.

Akaniambia kile kipande chote cha mtaa wa mkwepu kinachokatiza club ya billicanas mpaka kule kwenye maungio ya samora avenue, ni territory ya ma-mission town.

Hata papaa msofe alianza kujifunzia upigaji mitaa hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…