Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Awali ya yote nitangulize angalizo kwa vijana ambao maturity stage imewakuta miaka hii ya mitandao ya kijamii. Itabidi msome kimyakimya huku mkiwa mmeshika peni na karatasi kuchukua notes.

Huu uzi ni wa sisi ma-seniors, maudhui yake yatagusa zaidi vijana wenzangu ambao maturity stage iliwakuta kuanzia late 90s to early 2000s.

Mwaka 2002 mpaka 2012 mziki wa dansi ulikuwa upo kwenye prime time.

Kwa uchache tu, band zilizotamba ni FM Academia, Akudo Impact, Twanga Pepeta na Diamond Musica. Band nyingine zilikuwa zinaibuka na kupotea ndani ya muda mfupi.

Umaarufu wa hizi band ulienda sambamba na trend ya wanamuziki kutaja majina ya baadhi ya watu kwenye mashairi yao.

Majina ya hawa watu yalivuma na kuwa maarufu kuliko sura zao kwasababu miaka ile kulikuwa hakuna social platform za ku-share picha na video kama ilivyo hivi sasa.

Kutokana na kujichanganya kwangu ukijumlisha na ujanja wangu wa kimjini mjini wa miaka ile, nilifanikiwa kufahamiana na baadhi mapedeshee au wazee wa mujini ambao majina yao yalikuwa yanatajwa kwenye mziki wa dansi.

Nitataja ninaowakumbuka na wewe ongeza wa kwako.

Naandika majina yao kama yalivyokuwa yanatamkwa kwa mbwembwe na wanamuziki.

Kwa mfano kama mtu alikuwa anaitwa John, wanamuziki walikuwa wanatamka papaa John Young Millionaire Muzee ya ma-Range Rover[emoji3][emoji3].

Haya twende kazi:
Pedeshee Mychoice na kati ya Mbeya
:
huyu sijui alikuwa anapiga mishe gani huko Mbeya, watu wa Mbeya mtatusaidia.

Braza K na kati ya Tunduma:
Watu wa Tunduma mtatusaidia kutujuza kuhusu huyu jamaa, alivuma sana.

Mamaa Rukia Soloon:
Huyu bibie namfahamu, ana saloon yake ya kike mitaa ya Mikocheni barabara ya Rose Garden. Those days she was very pretty, kwa sasa utu uzima umemchukua.

Mamaa Dotnata Decoration:
Bila shaka wengi mnamkumbuka, aliwahi kuwa muigizaji maarufu kupitia ITV, baadae akaingia kwenye ujasiriamali wa kutoa huduma za decoration and catering. shughuli hizi zilimpatia mafanikio sana. sijui kwa sasa yupo wapi huyu mama. FM Academia waliwahi kumtungia wimbo wenye jina lake.

Mamaa Juddy Moshi:
Alikuwa mmiliki wa band ya Daimond Musica kwa financial support ya mshua mmoja ambaye alikuwa ni MD wa Yellow Pages, watu wa zamani wanaelewa. Juddy alikuwa mrembo si kitoto, kwa sasa umri wake umesonga mbele.

Pedeshee Akayesu Ndama Mutoto ya Ng'ombe:
Sina haja ya kumuelezea, ni mtu maarufu wa misimu yote. Wajanja wa mujini watamuelezea zaidi. Jina lake lilitajwa sana kwenye nyimbo za dansi zilizovuma.

Young Millionaire Bill gate Muzamir Katunzi:
Christian Bella aliwahi kutunga mpaka wimbo wenye jina hilohilo la Muzamir Katunzi. I don't know him personally, but it's told he was financially successful.

Papaa Msofe Chuma cha Reli hakishiki Kutu.
Sina haja ya kuandika mengi kuhusu umaarufu wa Papaa Msofe. Itoshe tu kusema jina lake liliimbwa sana halafu ni wachache waliokuwa wanajua sura yake. Walianza kuiona kwenye media alipokuwa anahudhuria viunga vya mahakama kujibu kesi yake.

Papaa Martin Kasianju.
Ni marehemu kwa sasa, huyu mshua ndio alikuwa mmiliki wa Band ya FM Academia. Nilikuwa namfahamu personally. licha ya kwamba alikuwa ni mjasiriamali na muajirwa Serikalini, pia alikuwa ni Senior Officer wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Andrew Traders na Kariakoo Big Supply: Jamaa alikuwa ni mfanyabiashara wa kuuza tairi za gari Mtaa wa Agrey Kariakoo huku akipiga michongo yake ya "general supply". Watu wa mujini wa zamani wanaelewa vizuri maana ya kampuni kusajiliwa kwa jina la general supply. Katika biashara ya kuuza tairi, alishirikiana na kaka yake, ila yeye akawa maarufu zaidi na akaaminika na wadau.

Kinje Mutoto wa Mujini:
Najua wengi mnamfahamu na zile deal zake alizokuwa anapiga. sina haja ya kumuelezea zaidi.

Pedeshee David Kabunga:
Sifahamu alikuwa ni nani, jina lake lilikuwa linatajwa sana.

Papaa Ally Kileo:
He was a prominent lawyer in town, jina lake lilikuwa linatajwa sana kwenye nyimbo za dansi.

Papaa Mutarika Mzee wa Mambo mengi:
Binafsi simfahamu, wajanja wa mujini wa zamani watajazia nyama kumuelezea.

Chef Justice Rugaibura:
Binafsi simfahamu, wajanja wa mujini wa miaka ile watajazia nyama kumuelezea.

Chief Kiumbe le Big Boss:
Anafahamika vizuri, jina lake lilitajwa na kuimbwa sana na wanamuziki wa band. wajanja wa zamani wa mujini watajazia nyama kumuelezea

Papaa Amos Makalla mzee wa Mvomero, Babaa na Gabriele:
Kwa sasa ni RC wa Dar, jina lake lilianza kuvuma kitambo sana kabla hata hajaingia kwenye siasa.

Fikiri Madinda Mukuu wa kazi: Anafahamika vizuri, wajanja wa zamani wa mujini watajazia nyama kumuelezea

Pedeshee Abdul Mkeketa:
Huyu wakati fulani aliwahi kuwa mbunge ktk Mkoa wa Morogoro, sikumbuki ni jimbo gani. kwa sasa ni marehemu.

Charles Mutawali Muzee ya Magari.
Binafsi simfahamu, wajanja wa zamani wa mujini watajazia nyama kumuelezea.

Saidi Mukuu wa lumumba:
Jamaa alikuwa dalali wa kuuza magari pande za Lumumba.

Meddy Kitendawili....?
Ben Mulokozi....?
Salim Chicago Matelefone...?
Kizaizai....?
Omary Tolu...?
Abduli Tolu...?
Joshua Limited...?
Muddy Nyamalonda mzee wa Pamba...?
China wa China...?
Shaibu Mapajero....?
Moris Mariaga Rais wa Sinza...?
Nteze wa Nteze....?
John Nzenze....?
Papaa Madenge....?
Muddy Nyambi....?
Jimmy Chokolete....?

Note of Appreciation
.
wakati naandika huu uzi sikufikiria kama ungepata wafuatiliaji wengi kiasi hiki. niwashukuru wote mnaoufatilia na mnaochangia maoni yenu. asanteni sana wadau.[emoji1431][emoji1431][emoji1431][emoji1431]
Wengi wao ni jamaa flan hivi ukijichanganya tu kwao imeisha, niishie hapo.
 
sina hakika na chanzo cha taarifa hii. ila kama ni kweli, huu ndio utakuwa mwisho wa kulisikia jina la eric mandala kwenye ngoma zijazo za fally ipupa, ferre gora na wengineo.

Eric Mandala Kinzenga, famous Congolese businessman, arrested in Madrid with 200 kilos of cocaine: a crackdown by the DEA and Udyco

The Congolese patron and businessman, was arrested in possession of 200 kilos of cocaine hidden in a van parked in the parking lot of a shopping center. The cargo, coming from Ecuador and transiting through the port of Algeciras, was destined for Morocco.

The operation, carried out by the DEA and Udyco, follows an investigation lasting several months launched in August 2024. Mandala, already under surveillance, was arrested in the company of a Colombian woman, in possession of more than $50,000 in cash. In 2020, he acquired a sumptuous apartment at the Burj Khalifa for 1.85 million euros.

He is now spending his second night in prison in Madrid, while investigations continue.

source: www.jabulaniradio.com
 
Attachments

  • IMG-20250125-WA0006.jpg
    IMG-20250125-WA0006.jpg
    57.2 KB · Views: 5
Boss… Erick Mandala,The one and only (Ngiri, ngiri ngiri).
ndio hivyo tena, pedeshee erick mandala kayakanyaga,
mbaya zaidi kayakanyaga kwa polisi wa kizungu.

ingekuwa kakamatiwa kwenye hivi vinchi maskini vya kiafrika, ingekuwa rahisi kuchezesha mchezo, mambo yasingekuwa mengi.
 
Kweli angekamatiwa Africa angetoa hizo dola elfu 60 alizokamatwa nazo kama hongo ili atoke ila NGOZI nyeupe atajua hajui.
 
sina hakika na chanzo cha taarifa hii. ila kama ni kweli, huu ndio utakuwa mwisho wa kulisikia jina la eric mandala kwenye ngoma zijazo za fally ipupa, ferre gora na wengineo.

Eric Mandala Kinzenga, famous Congolese businessman, arrested in Madrid with 200 kilos of cocaine: a crackdown by the DEA and Udyco

The Congolese patron and businessman, was arrested in possession of 200 kilos of cocaine hidden in a van parked in the parking lot of a shopping center. The cargo, coming from Ecuador and transiting through the port of Algeciras, was destined for Morocco.

The operation, carried out by the DEA and Udyco, follows an investigation lasting several months launched in August 2024. Mandala, already under surveillance, was arrested in the company of a Colombian woman, in possession of more than $50,000 in cash. In 2020, he acquired a sumptuous apartment at the Burj Khalifa for 1.85 million euros.

He is now spending his second night in prison in Madrid, while investigations continue.

source: www.jabulaniradio.com
Yes Eric Mandala wamemnasa Spain Madrid akiwa ameegesha gari kwenye business parking slots, ndani ya gari walimnasa na kilo 200 cocaine pamoja na $50000 sawa na Tsh.. bil 127.
Inasemekana walianza fuatilia hii ishu tangu August 2024 baada ya contena kuvuka kwenda morocco.

Ebwana eeeh wajina kabisa.
 
Kuna yule alichapagwa risasi na wenzake watatu akiwemo mwanamke katika tukio la ujambazi nanenane morogoro nadhani 2003 to 2004,baadhi ya mapeshee walikuwa majambazi na wauza bwimbwi
 
Yes Eric Mandala wamemnasa Spain Madrid akiwa ameegesha gari kwenye business parking slots, ndani ya gari walimnasa na kilo 2 cocaine pamoja na $50000 sawa na Tsh.. bil 127.
Inasemekana walianza fuatilia hii ishu tangu August 2024 baada ya contena kuvuka kwenda morocco.

Ebwana eeeh wajina kabisa.
Bora angekomaa tu na biashara ya madini/ dhahabu kama wenzake, kwenye madini hata kama utaweka uhuni uhuni ni rahisi kusolve ila huku kwenye drugs tena kwa wazungu ebanaeee ni kisanga
 
Bora angekomaa tu na biashara ya madini/ dhahabu kama wenzake, kwenye madini hata kama utaweka uhuni uhuni ni rahisi kusolve ila huku kwenye drugs tena kwa wazungu ebanaeee ni kisanga
Balaa zito hili.....ila sio mbaya kala maisha....
 
hakuna show ya fally ipupa iliyowahi kubamba hapa east africa kama hii ya dar iliyofanyika 2009 chini ya uandalizi na usimamizi wa dada yetu jasmine razack.

kuna kipindi alikuwa bega kwa bega na feisal salum wakati wa sakata lake na club ya yanga. nadhani ni mmoja wa wasimamizi wake wa mikataba.

kuna wimbo mmoja wa fally ipupa katika album yake ya formule 7 ujulikanao kwa title ya MH, kamtaja 'jasmine le tanzanien'.
 
Attachments

  • IMG_20250225_180623.jpg
    IMG_20250225_180623.jpg
    94 KB · Views: 2
  • TikTok_7474686090897542422.mp4
    3.8 MB
Kweli angekamatiwa Africa angetoa hizo dola elfu 60 alizokamatwa nazo kama hongo ili atoke ila NGOZI nyeupe atajua hajui.
Mzungu kukufatilia yuko radhi achukue hata miaka 2 ila akikumqliza jua huchomoki maana wanakuwa na nushaidi wa kutosha

Ova
 
Mzungu kukufatilia yuko radhi achukue hata miaka 2 ila akikumqliza jua huchomoki maana wanakuwa na nushaidi wa kutosha

Ova

Kweli ,huyo mandala apigwe mvua za maisha ,kaharibu na kutia umasikini vijana wengi.

Nilikuwa naangalia taarifa ya habari Azam kuna mfanyabiashara account yake ilifika hadi milioni 900 huku bizness ikirun ,kwasasa huyo mfanyabishara amehifadhiwa kwenye chumba kimoja kwenye nyumba ya aliyekuwa dereva wake. ,fedha imeisha yote coz ya "ngada" alikuwa anatumia.
 
Hawa wasanii wao kusifiasifia kutaja watu tu...wengi magumashi
Nmekumbuka enzi zile za twanga pale mango..... wana vuma mm mwenyewe nlikuwa mdau sana wa ile bendi 😄
Sasa kuna siku show yao pale inapigwa mara akaingia jamaa mmoja alikuwa maarufu kino na mtu wa ngada..jamaa kuingia tu na team twanga wakamrusha....jina 😄 jamaa wacha amind ilibd awafate jamaa wa bendi akataka kuwaletea uzushi.... 😄 ila jamaa naye alishapotea kwenye game choka

Ova
 
Kweli ,huyo mandala apigwe mvua za maisha ,kaharibu na kutia umasikini vijana wengi.

Nilikuwa naangalia taarifa ya habari Azam kuna mfanyabiashara account yake ilifika hadi milioni 900 huku bizness ikirun ,kwasasa huyo mfanyabishara amehifadhiwa kwenye chumba kimoja kwenye nyumba ya aliyekuwa dereva wake. ,fedha imeisha yote coz ya "ngada" alikuwa anatumia.
Hii biashara ina laana mkuu
Lazima itakurudia
Mchimba kisima kaingia mwenyewe

Ova
 
Back
Top Bottom