Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Umenikumbusha mbali, mbali, Mandela baada ya kupata Urais ilikuwa Telkom ukiomba huduma ya simu ndani ya wiki moja unaunganishiwa.

Kulikuwa na jamaa yupo Kuwait Wahindi wanapanga foleni kuanzia asubuhi mpaka usiku non stop mnawaunganisha kuongea na familia zao India kisha yeye anawatumia pesa kupitia western union na wala hamjuwani wala hata hujui anafananaje.
Nlipiga San mishe hizo
Hahaha
Wahindi ndy walikuwa wateja wetu wakuu,alafu wahindi wenyewe wazito

Ova
 
Kuna mtu alikuwa anaitwa Juma Ngida huyu alikuwa mtoto wa mjini kweli kweli na hela ilikuwepo...huyu ndio mtu wa kwanza kuingiza hizi gari Rav 4 mpya nchini ..kipindi mererani inaanza kuchimbwa jamaa akaanza safari akaenda kufika arusha wakamwambia mzee hiki kipindi cha mvua saa hivi barabara ya merelani gari hazipitiki kwa hizi gari za kifahari ujamaa pale pale akatoa mpunga akanunua land cruiser mpya impeleke ...yaan kama ananunua shati vile .ila amefariki kwa sasa aliimbwa mpaka na dudu baya kwenye nyimbo yake ya nidhamu mana jamaa ndio alikuwa anajiita don king minyamihela .
Juma nyamiela alikufa pesa imekata,alikua mpka na mabasi
 
Nimekumbuka mbali sana NIMEONA JINA LANGU hapo,Pia nimeakumbuka akina HASSAN MIUNDOMBINU,ALLY KILEO,KIZAIZAI SUPER TALL,KIZA KINENE,ABDALLAH NYUMBA NYINGI😀Halafu sio wote wanaotajwa kwenye band walikuwa wana pesa wengine walikuwa kawaida tu hasa vijana wa kinondoni
Huyu abdalah nyumba nyingi,yeye alikua na mishe gani
 
Lyatonga si ndy alituchomesha akawaribia wabongo viza UK
Entry
Bandika bandua watu walizipiga sana

Ova
Walioharibu entry viza UK ni Wazanzibar baada ya uchaguzi wa 1995 na Maalim Seif kuporwa ushindi wengi waliingia UK na kuomba political Asylum seeker kwa complain ya wafuasi wa CUF kunyanyaswa na CCM.

Ndio msingi wa Serikali ya Uingereza kutufutia entry na kuanza utaratibu wa kuomba viza ubalozini.

Wazungu wanachukia sana pesa za walipa kodi wao kuwalipa posho wakimbizi.

Na sasa hivi wanataka kukomesha kabisa ukiomba ukimbizi Uingereza unaoelekwa Rwanda, Kagame kashavuta mpunga.
 
Hao Wanamuziki wa Congo wote break yao kuna Don wa Ki Ivory coast anaishi Paris anaitwa Hemed Bakayoko, huyu ndio funga kazi, hii treasure.

Huyu ndio hakauki mdomoni mwa Boss ya Mboka Koffi Ollomide then ndio anakula shavu Samuel Etoo, hizi ni international level.
Acha uongo. Hamed Bakayoko alikuwa waziri mkuu wa Ivory Coast hakuwa akiishi Paris.. pia tayari ni marehemu zaidi ya mwaka. Ushabiki wa vijiweni usilete hapa.
 
mwenye asili ya kihayudi ni moise katumbi, mmiliki wa team ya mpira TP mazembe.

ila huyu bwana mdogo abed achour ni mwarabu mwenye asili ya Lebanon.

familia yake ilihamia congo miaka 50 iliyopita. yeye mwenyewe amezaliwa drc katikati au mwishoni mwa miama ya 80.

ndani ya congo, familia yake imewekeza ktk sector mbalimbali ikiwemo transportation, manufacturing na hospitality.

hapo kwenye hospitality wanamiliki hotel kubwa sana kinshasa. kiufupi dogo ni Don kwelikweli.

akina fally, ferre, innoss'B, heritier wakikutana na huyo dogo, wanahisi ni kama vile wamekutana na na tajiri namba moja duniani billionaire Elon Musk.
Wanamuziki wa Congo wanakwama wapi? Mbona wanaonekana wana hela ila bado wana ishu za kusifia sifia watu ovyo kama vile machawa?
 
Le Mutuz licha ya ujinga ulimjaa kichwani ni baharia, miaka ya 80's na 90's bahari hapa mjini ni flag kubwa.

Kwahiyo usimchukulie powa Le Mutuz yumo naye katika watoto wenye Dar yao, ni kwamba tu ameharibikiwa akili uzeeni na kuingia kwenye uchawa ndio maana watu wanamdharau.
Lemutuz ana akili nyingi ila inaonekana ana stress za kufika uzeeni bila kuwa na mali kulingana na hadhi ya familia yake pamoja na yeye kuishi marekani miaka 30
 
Acha uongo. Hamed Bakayoko alikuwa waziri mkuu wa Ivory Coast hakuwa akiishi Paris.. pia tayari ni marehemu zaidi ya mwaka. Ushabiki wa vijiweni usilete hapa.
Umekurupukia wapi unatoka chooni kukata kimba bila kuchamba?
Ungefuatilia mtiririko wa huu uzi usingeandika hizi pumba zako bwegge jinga kabisa.
 
Wanamuziki wa Congo wanakwama wapi? Mbona wanaonekana wana hela ila bado wana ishu za kusifia sifia watu ovyo kama vile machawa?
Wana pesa mno,magari aliyonayo koffi olomide, fally na JB mpiana wasanii wetu hawana,hao jamaa Wana ma Bentleys,Ferrari,rolls Royce, mtu Kama JB mpiana alikuwa na Mercedes Benz mwaka 1999 huko
Wafuatilie YouTube uone mijengo yao
 
Acha uongo. Hamed Bakayoko alikuwa waziri mkuu wa Ivory Coast hakuwa akiishi Paris.. pia tayari ni marehemu zaidi ya mwaka. Ushabiki wa vijiweni usilete hapa.
Usimpinge Sana huenda Bakayoko alikuwa na nyumba Paris, mtu Kama Mobutu alikuwa Rais wa Zaire wakati at the same time anaishi France,Belgium,uswizi,Monaco nk, hata wanae leo wanaishi Nchi mbili au tatu wakati mmoja mfano nzanga alikuwa waziri congo ila anaishi Congo,Washington na Rabat Morocco
 
huyu pedeshee ni waukweli kitambo sana.
nilianza kumsikia kwenye nyimbo za Kofii miaka ya tisini huko,Nyimbo kama Mico,,Kofi alikua akiimba anaanza na jina la Chaaaachoooo.
Usichanganye mambo. Tchatcho ni aina ya muziki uliobuniwa na Koffi enzi hizo. Akawa anaupromoti kwenye nyimbo zake. Ila Chacho anayeongelewa ni mtu kwa jina la Chacho Mbala.
 
Umemsahau Papaa Shabani Ngalawa (R.I.P). Huyu alikua mwalimu mzuri wa tution miaka ya 1995-2001 hizi za shule ya msingi. Miaka ambayo mtaa mzima unakuta waliofaulu la saba ni wawili au hakuna na katika hao waliofaulu wote walisoma tution kwa huyu mwalimu shabani..

Nakumbuka alichukuaga mkopo wa milioni 200 lengo likiwa kujenga shule yake binafsi maeneo ya kibamba. Akaweka rehani nyumba na shamba lake. Mwisho wa siku pesa zote zikaishia kuwatunza akina ally choki na mwinjuma muumini ktk mabendi na nyingine akanunulia toyota baloon. Benki ikaja ikapiga mnada nyumba na shamba wakamfilisi mazima.

Alitajwa sana kwenye nyimbo za Mwinjuma hasa ile ya Kilio cha Yatima. Alikuja kuugua mda mrefu na aliisha akawa kama mtoto. Amefariki akiwa hana hata pa kulala. Sad!
 
Wakina IDD JANGUO nilikuwa nawaskia sana ali choki akiwataja
Huyu alikua mtoto wa kigogo mbunge wa Kisarawe enzi hizo. Mdingi wake licha ya kua Mbunge alishawahi kua kiongozi mkubwa wa bandari ya DSM pale. Na ana mjengo mkali uingereza kuna baadhi ya wanawe wanaishi huko.. Mzee Janguo alikua na ukwasi saaaana..

Iddi Janguo alikua anamiliki limousine nyeusi ilisumbua saaana mjini wakati ule na alikua anaishi ktk jumba la ghorofa kule mitaa ya Jangwani seabreeze la mshua wake.. Alifanya fujo nyingi mjini wkt ule miaka ya 2005 kushuka chini.. Enzi nipo sekondary nilikuaga natamani nikiwa mkubwa niwe japo na nusu ya mkwanja aliokua nao.. Zile zama watoto wa vigogo walituvimbia sana. Naskia siku hizi yupo Kinondoni ametulia hana tena zile pesa kama wkt ule..

Na alikua anang'oa pisi kali sana. Unaukumbuka ule wimbo wa Dudubaya unaitwa Mashaka kuna mstari aliimba, "Warembo wazuri acheni kugombana, sina chaguo kama IDDI JANGUO, lakini kwa leo warembo nyongeni.. Atakaeshinda ntaondoka nae.. Mshike kiuno (uyoo) mlambe unyayo (uyoo) mshike mabega (uyoo) mkalie kwa juu!!!" [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom