Tuwajengee watoto wetu kuta za kuwalinda na mabaya lakini kuta zisije kuwa jela wakija kuishi maisha tofauti na tunayowazoesha

Tuwajengee watoto wetu kuta za kuwalinda na mabaya lakini kuta zisije kuwa jela wakija kuishi maisha tofauti na tunayowazoesha

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Mtoto anakosea na kurudia na humchapi kwa kuiga dunia ya mbele kwamba asiumie lakini mzazi anajizima data kwamba hapa bongo adhabu zake huwa ni vipigo kwa mtu anaezingua, mtoto kaiba huko akidhani kwamba ataonywa kama ilivyo kwa daddy na mommy, matokeo yake anapokea kichapo kizito sana ambacho hakutarajia, leo hii umefariki mzazi huyo mtoto anaenda kuishi kwa ndugu zake ambao wanaishi maisha halisi ya watanzania wengi atapata shida sana.

Mtoto anarudi nyumbani analia kapigwa na mwenzake unamwambia usirudishie, ntakuhamisha shule, n.k. come on!! hii bongo hata huku ukubwani uonezi ni mkubwa sana, ukimzoesha mtoto kukimbia uonezi si sawa kabisa kwa mazingira yetu ya hapa bongo, nikiwa mtoto nakumbuka nilikuwa naambiwa "KAMRUDISHIE" amini usiamni ndivyo nilivyoweza kujitetea hata nilipofika boarding na hata sasa maisha ya utu uzima huku hakuna ngumi lakini ukilemaa utajuta,

Mtoto anafuliwa nguo na unajua kabisa hii ni bongo sio ulaya, Siku ya siku umeanguka na pesa ya house girl haipo tena wala hakuna pesa ya mashine ya kufulia, hapa bongo sio ulaya ambako hata gerezani wanafua kwa mashine, mzik ataopitia mtoto wako ni kwajili yako, na hapo anaweza kuwa mchafu kwa uvivu wa kufua,
 
Tujue kutofautisha maisha ya kwenye muvi na maisha ya uhalisia wa hapa kwetu.
 
Back
Top Bottom