Tuwajengee watoto wetu misingi ya kujiamini na kujitegemea kiuchumi

Tuwajengee watoto wetu misingi ya kujiamini na kujitegemea kiuchumi

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
41,558
Reaction score
64,966
Ni vizuri watoto wako wajue kazi au shughuli zinazokuingizia kipato, ikiwezekana uanze kuwapa misingi tangu wakiwa wadogo labda miaka 3+.

Kama wewe ni mfanya biashara au una kampuni yako inafanya shughuli fulani, ni vizuri kuongozana na watoto wako ili kuwajenga kihisia katika utafutaji wako; ikiwezekana ata unapoenda bank nenda nao. Ata kama umri wao hawawezi kufanya chochote...ila wakikaa kwenye yale mazingira mara kwa mara, uwezo wao wa kufikiri unakuwa mkubwa sana.

Wakati mwingine unaweza kuwauliza, ata kama wana miaka 5; 'tufanyeje ili uzalishaji wa kampuni yetu uwe mkubwa?'Jibu watakalokupa usicheke, bali waonyeshe hali ya kukubali wazo lao. Lengo ni kuwajenga katika kujiamini kwenye uchumi. Na hii itakupa credit kwenye malezi ya watoto wako.

Note: 'Wekeza kwenye biashara ili siku ukifariki familia irithi biashara yako,kuliko kuwekeza kwenye kuajiriwa..siku ukifariki familia haitarithi ajira yako'
 
mkuu umenena naanza kuwaandalia mtaji kuanzia now....
 
Kaneno🤔
Wenzetu wamefanikiwa sana kwenye hili. Akifa watoto wanaendeleza pale baba alipoishia, wanaangalia pia ulikuwa unakosea wapi wanaboresha.

Bongo ukifa mpaka miradi inakufuata huko kaburini.
Ndio hivyo mkuu,inabidi tubadilike
 
Mkuu watoto wangu ajira wataisikia kwa jirani lazima wajiajiri..
watasoma Business administration na mtaji watakuta wa 18+ million per ngedere.
sasa nisikie ngedere analalamika umaskini.
 
Mkuu watoto wangu ajira wataisikia kwa jirani lazima wajiajiri..
watasoma Business administration na mtaji watakuta wa 18+ million per ngedere.
sasa nisikie ngedere analalamika umaskini.
Hayo ndio maamuzi sahihi
 
Mkuu watoto wangu ajira wataisikia kwa jirani lazima wajiajiri..
watasoma Business administration na mtaji watakuta wa 18+ million per ngedere.
sasa nisikie ngedere analalamika umaskini.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

stidy
 
Dhaaa kwakwel napambana
Watoto wangu wacje
Kushangaa comments humu kama
Mm

stidy
 
Back
Top Bottom