Tuwakomalie Polisi kuwarejesha watuhumiwa wakiwa hai

Tuwakomalie Polisi kuwarejesha watuhumiwa wakiwa hai

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Polisi wanatuchukulia poa sana. Hawajui waajiri wao ni sisi.

Catherine Ruge anaeleweka vyema kuwa suala la kuzika halipo na halitakuwapo.

"Ingekuwa muafaka zaidi polisi kufahamishwa kuwarejesha watuhumiwa hai kama walivyowachukua."

Haiwezekani wajue kuuwa tu na si kurudisha uhai walioutoa kwa makusudi!

Ninakazia, wasije wakathubutu kwetu. Kwani kwa hakika patachimbika wala hakitakuwa cha mtoto.

Kwamba walimchukua mzima? Ninakwenda vipi kulipa gharama zipi za "monchwari" (kama anavyokuita Abdul Nondo)? Monchwari ipi hiyo kwanza? Ninalipa vipi nauli ya polisi yupi?

NInamzika vipi marehemu aliyeuwawa na polisi kwenye mazingira haya?

Kwanini hatuwashauri wahanga kukomaa na polisi kuwarejeshea ndugu zao wakiwa hai?

Kwa nini badala yake tunageuka kuwa waandishi wa habari? Au ni yale ya kujitafutia mileage tu?

Nini mchango wetu kuona ubazazi huu kutoka kwa watu tuliowaajiri unakoma taslimu (forth with) sasa?
 
Wakati panya road walipokuwa wanavamia nyumba za watu kuiba, kujeruhi na kuuwa raia wema wasiokuwa na hatia, mbona sikukuona ukija kutoa ushauri wa namna yoyote dhidi ya hao vijana wenu wa panya road?

Au wale waliokuwa wanavunjiwa nyumba zao, kuibiwa na kuuwawa hawakuwa na haki ya kutetewa mitandaoni kama mnavyowatetea panya road?
Tunajua wengi wa wale wanaowatetea panya road ni maboss wao au wanamtandao wenzao.

Sasa na sisi tutaanza kuwashauri polisi wawe wanakuja kufuatilia na kuwachunguza hawa wanaowatetea hawa panya road mitandaoni, kwamba wanawatetea kwa lengo zuri au na wao ni miongoni mwa wafaidika wa vitu vya wizi vinavyopatikana baada ya mwenye navyo kupigwa mapanga na kuuwawa bila sababu.
 
Tatizo linaanzia hapa. Kwann unataka tuwashauri na tusishiriki ktk kuwakomalia hao polisi.

Huu mgawanyiko tulionao watanzania utatautafuna sana

Rejea kuona unaniwekea maneno mdomoni mwoga mkubwa wee!

Nimekupa tathmini ya miye kama mimi nini nitafanya. Nimekupa tathmini ya Catherine Ruge kama yeye nini amefanya.

Nimekupa tathmini ya Abdul Nondo kama yeye nini amefanya. Huyu karipoti kama mwandishi wa habari.

Nimekupa tathmini yangu ya nini wengine wanaweza kufanya kwa ndugu wa wahanga, kikaleta tija.

Cha kwako wewe kiko wapi?

Wewe si uko kwenye rekodi ukisema hauko tayari kukabiliana na polisi kwa kuwa unaogopa kufa? Sasa hilo tatizo unalotaka kudai linaanzia hapo, hapo wapi? Pakufikirika?

Weka mkakati wako hapa ulio tayari wewe kuusimamia kuumaliza uovu huu wa polisi.

Ya nini kuandikia mate?
 
Wakati panya road walipokuwa wanavamia nyumba za watu kuiba, kujeruhi na kuuwa raia wema wasiokuwa na hatia, mbona sikukuona ukija kutoa ushauri wa namna yoyote dhidi ya hao vijana wenu wa panya road?

Au wale waliokuwa wanavunjiwa nyumba zao, kuibiwa na kuuwawa hawakuwa na haki ya kutetewa mitandaoni kama mnavyowatetea panya road?
Tunajua wengi wa wale wanaowatetea panya road ni maboss wao au wanamtandao wenzao.

Sasa na sisi tutaanza kuwashauri polisi wawe wanakuja kufuatilia na kuwachunguza hawa wanaowatetea hawa panya road mitandaoni, kwamba wanawatetea kwa lengo zuri au na wao ni miongoni mwa wafaidika wa vitu vya wizi vinavyopatikana baada ya mwenye navyo kupigwa mapanga na kuuwawa bila sababu.

Hukuona Ushauri wangu? Au una maana nikiweka Ushauri wangu hapa nakuja kukugongea nyumbani kwako Ili uuone?

Kwa taarifa yako ushauri wangu niliweka hapa na huo ulikuwa kabla sana ya operation ya Polisi hata kufikiriwa:

Dar: Panya road wavamia nyumba 24, wanne wajeruhiwa

Zaidi sana nimeeleza wazi kuwa na mara kadhaa mimi ni mhanga wao na labda ninawachukia kuliko wewe:

Kama tunataka Katiba Mpya, Tusiionee "Haya" Haki ya awaye yote

Tambua nisichokubaliana nacho ni police brutality na extra judicial killings yao.

Ni hayo tu ndugu mjumbe.
 
Kama kuna watuhumia wengine tofauti na panya hapo sawa.

"Mtuhumiwa anabakia kuwa raia mwema (innocent) hadi ithibitishwe vinginevyo."

Unapaswa kujishangaa kama wewe una "exception" ya kwako peke yako katika ukweli huo.

Vipi ukifananishwa na panya road? Si inasemekana wanatambulika hata kwa macho yao tu? Vipi kama yako yamezidi kigezo ukasomeka kuwa ndiye panya road mkuu?

"Kwa mikono miwili nawakaribisha kwetu. Ukisikia ya yule "Mwanani" yamejirudia wala usije kushangaa ..."
 
Tatizo linaanzia hapa. Kwann unataka tuwashauri na tusishiriki ktk kuwakomalia hao polisi.

Huu mgawanyiko tulionao watanzania utatutafuna sana

Kwamba tatizo linaanzia wapi? Siyo hapa?

IMG_20221001_005321_603.jpg
 
Duuh! Ama kweli ogopa Mungu na teknolojia

Hatutarudishwa nyuma na watu kama nyie. Mnaifanya nafasi ya kuleta mabadiliko kuwa ngumu unnecessarily.

Haipo shaka kuwa hata kuwashauri wafiwa tu, kukomaa na polisi pia mnaogopa.

Kwani hypocricy maana yake nini?

Mnataka kucheza salama (playing safe) siyo?

NInakazia: ".... wala hamtasikia tukiwalaumu."
 
Hukuona Ushauri wangu? Au una maana nikiweka Ushauri wangu hapa nakuja kukugongea nyumbani kwako Ili uuone?

Kwa taarifa yako ushauri wangu niliweka hapa na huo ulikuwa kabla sana ya operation ya Polisi hata kufikiriwa:

Dar: Panya road wavamia nyumba 24, wanne wajeruhiwa

Zaidi sana nimeeleza wazi kuwa na mara kadhaa mimi ni mhanga wao na labda ninawachukia kuliko wewe:

Kama tunataka Katiba Mpya, Tusiionee "Haya" Haki ya awaye yote

Tambua nisichokubaliana nacho ni police brutality na extra judicial killings yao.

Ni hayo tu ndugu mjumbe.
Siku panya road wakikukata mkono umuite ruge
 
Safi sana jeshi la polisi kwa kuwalaza mapema wakora saba Iringa.Yale yaliyokimbia yatafuteni yapigeni shaba za makalio na watetezi wao wote.
 
Back
Top Bottom