Tuwakomalie Polisi kuwarejesha watuhumiwa wakiwa hai

Tuwakomalie Polisi kuwarejesha watuhumiwa wakiwa hai

Polisi wanatuchukulia poa sana. Hawajui waajiri wao ni sisi.

Catherine Ruge anaeleweka vyema kuwa suala la kuzika halipo na halitakuwapo.

"Ingekuwa muafaka zaidi polisi kufahamishwa kuwarejesha watuhumiwa hai kama walivyowachukua."

Haiwezekani wajue kuuwa tu na si kurudisha uhai walioutoa kwa makusudi!

Ninakazia, wasije wakathubutu kwetu. Kwani kwa hakika patachimbika wala hakitakuwa cha mtoto.

Kwamba walimchukua mzima?Nakwenda vipibkulipa gharama zipi za "monchwari" (kama anavyokuita Abdul Nondo)? Monchwari ipi hiyo kwanza? Ninalipa vipi nauli ya polisi yupi?

NInamzika vipi marehemu aliyeuwawa na polisi kwenye mazingira haya?

Kwanini hatuwashauri wahanga kukomaa na polisi kuwarejeshea ndugu zao wakiwa hai?

Kwa nini badala yake tunageuka kuwa waandishi wa habari? Au ni yale ya kutajifutia mileage tu?

Nini mchango wetu kuona ubazazi huu kutoka kwa watu tuliowaajiri unakoma taslimu (forth with)?
Anza kwanza kuwakomalia majambazi,vibaka, panya road waibe kwa staha na wasiue wanaowadhuru.
 
Wakati panya road walipokuwa wanavamia nyumba za watu kuiba, kujeruhi na kuuwa raia wema wasiokuwa na hatia, mbona sikukuona ukija kutoa ushauri wa namna yoyote dhidi ya hao vijana wenu wa panya road?

Au wale waliokuwa wanavunjiwa nyumba zao, kuibiwa na kuuwawa hawakuwa na haki ya kutetewa mitandaoni kama mnavyowatetea panya road?
Tunajua wengi wa wale wanaowatetea panya road ni maboss wao au wanamtandao wenzao.

Sasa na sisi tutaanza kuwashauri polisi wawe wanakuja kufuatilia na kuwachunguza hawa wanaowatetea hawa panya road mitandaoni, kwamba wanawatetea kwa lengo zuri au na wao ni miongoni mwa wafaidika wa vitu vya wizi vinavyopatikana baada ya mwenye navyo kupigwa mapanga na kuuwawa bila sababu.
Acha ujinga, KATIBA na Sheria za Nchi haziruhusu POLICE kumuua mtuhumiwa aliye mikononi mwa POLISI amefungwa pingu.

Mahakama pekee ndo Ina mamlaka kuhukumu mtu KIFO.

Nikuulize swali: Ni KESI ngapi mahakama imehukumu mtu anyongwe na Rais anakwepa Kutia Saini?

Kwann Rais aogope kusain mtu anyongwe afu POLISI alazimishwe kuua, msiwape ndugu zetu POLISI LAANA 😠😠😠
 
Ili iweje kwa hao panya road na majambazi wenye mapanga na visu?
Naona anza kwanza kwa kuwauliza hao majambazi na panya road, kwa nini wanabeba hizo silaha?
Kwa nini wasiende kuiba bila kuiba mahali ambapo panaruhusiwa na katiba ya serikali?
[emoji3062][emoji3062][emoji3062][emoji3062][emoji3062][emoji3062][emoji3062]
 
Polisi kazeni hapo hapo

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app

Wenzako hivi sasa wako hivi:

IMG_20221001_023903_471.jpg

Pita vituoni uwaone.

Pale Musoma ndiyo kabisa, hivi sasa wanazingatia PGO kweli kweli.

Unadhani hawajipendi?
 
Mtu yoyote anayeunga mkono binadamu mwenzake kuuawa kiholela Ni mpumbavu...
 
Ili iweje kwa hao panya road na majambazi wenye mapanga na visu?
Naona anza kwanza kwa kuwauliza hao majambazi na panya road, kwa nini wanabeba hizo silaha?
Kwa nini wasiende kuiba bila kuiba mahali ambapo panaruhusiwa na katiba ya serikali?
[emoji3062][emoji3062][emoji3062][emoji3062][emoji3062][emoji3062][emoji3062]

Hivi ni vigumu kuelewa kiasi hiki?

Japo si nadra kwa panya road na majambazi kubeba visu na panga, si sahihi kumshutumu awaye yote kwa kubeba kisu na panga.

Kubeba kisu au panga hakukufanyi wewe au awaye yote kuwa panya road au jambazi.
 
Kumbukumbu la Torati 19:21

21 Hampaswi kuwahurumia:i Uhai utatolewa kwa uhai, jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu.

Upo uhakikaa gani kuwa waliotolewa uhai na polisi waitoa uhai?

Kumbuka mfanya biashara wa madini Mtwara, wafanya biashara ya madini Ifakara. Hawa waliporwa fedha na kutolewaxuhai na polisi.

Usiwasahau Lissu, Lijenje, Ben, Azory. Hawa ni wahanga wa mamlaka kama navyo kumbushwa mara lukuki na bwana RNA kuwa kuna wavaa makoti marefu meusi.

Kumbuka wa kwenye viroba. Orodha haina mwisho.

NInakazia: ipo tofauti kubwa baina ya watoa uhai na washukiwa.
 
Acha ujinga, KATIBA na Sheria za Nchi haziruhusu POLICE kumuua mtuhumiwa aliye mikononi mwa POLISI amefungwa pingu.

Mahakama pekee ndo Ina mamlaka kuhukumu mtu KIFO.

Nikuulize swali: Ni KESI ngapi mahakama imehukumu mtu anyongwe na Rais anakwepa Kutia Saini?

Kwann Rais aogope kusain mtu anyongwe afu POLISI alazimishwe kuua, msiwape ndugu zetu POLISI LAANA 😠😠😠
Panya road ni lazima wauwawe ili kulinda maisha ya wengine.
Sheria na mahakama vimeshindwa kupunguza uhalifu, ukatili na mauaji yanayofanywa na vijana hao wa panya road.
 
Panya road ni lazima wauwawe ili kulinda maisha ya wengine.
Sheria na mahakama vimeshindwa kupunguza uhalifu, ukatili na mauaji yanayofanywa na vijana hao wa panya road.

Asemaye kuwa sheria na mahakama vimeshindwa ni nani mkuu?
 
Na majambazi tuwakomalie waibe ila wasiue raia.

Ungekuwa umesema na watuhumiwa wa ujambazi tumawakomalia waache utuhumiwa ungekuwa umejitendea haki zaidi.

Zingatia mada ni kuhusu washukiwa si majambazi wala panya road.
 
Tangu hii operation ya panya road ianze, umevurugika sana...lazma kila siku upost, kuna kitu sio bure!!
 
Polisi wanatuchukulia poa sana. Hawajui waajiri wao ni sisi.

Catherine Ruge anaeleweka vyema kuwa suala la kuzika halipo na halitakuwapo.

"Ingekuwa muafaka zaidi polisi kufahamishwa kuwarejesha watuhumiwa hai kama walivyowachukua."

Haiwezekani wajue kuuwa tu na si kurudisha uhai walioutoa kwa makusudi!

Ninakazia, wasije wakathubutu kwetu. Kwani kwa hakika patachimbika wala hakitakuwa cha mtoto.

Kwamba walimchukua mzima?Nakwenda vipi kulipa gharama zipi za "monchwari" (kama anavyokuita Abdul Nondo)? Monchwari ipi hiyo kwanza? Ninalipa vipi nauli ya polisi yupi?

NInamzika vipi marehemu aliyeuwawa na polisi kwenye mazingira haya?

Kwanini hatuwashauri wahanga kukomaa na polisi kuwarejeshea ndugu zao wakiwa hai?

Kwa nini badala yake tunageuka kuwa waandishi wa habari? Au ni yale ya kutajifutia mileage tu?

Nini mchango wetu kuona ubazazi huu kutoka kwa watu tuliowaajiri unakoma taslimu (forth with)?
Issue hii inatuhusu sote,ukisema wahanga wakomalie ni pamoja nami na wewe.Jinsi ulivyoshauri ndivyo watesi wetu wapendavyo-Kutugawanya ili iwe rahisi kutushinda.Wanafahamu kwamba tukiunganisha Nguvu zetu pamoja tutawakomesha mazima.Asili ya mateso mengi wanayopitia wenyenchi hii ni Ukatili wa vyombo vya Dola na Watawala(CCM).
Kuna maandamano ya kupinga Ukatili/Unyama wa POLISI Duniani Jumatatu ya tarehe 03-10-2022.Tuanzie hapo.
 
Back
Top Bottom