Tuwakomalie Polisi kuwarejesha watuhumiwa wakiwa hai

Tuwakomalie Polisi kuwarejesha watuhumiwa wakiwa hai

Polisi wanatuchukulia poa sana. Hawajui waajiri wao ni sisi.

Catherine Ruge anaeleweka vyema kuwa suala la kuzika halipo na halitakuwapo.

"Ingekuwa muafaka zaidi polisi kufahamishwa kuwarejesha watuhumiwa hai kama walivyowachukua."

Haiwezekani wajue kuuwa tu na si kurudisha uhai walioutoa kwa makusudi!

Ninakazia, wasije wakathubutu kwetu. Kwani kwa hakika patachimbika wala hakitakuwa cha mtoto.

Kwamba walimchukua mzima?Nakwenda vipibkulipa gharama zipi za "monchwari" (kama anavyokuita Abdul Nondo)? Monchwari ipi hiyo kwanza? Ninalipa vipi nauli ya polisi yupi?

NInamzika vipi marehemu aliyeuwawa na polisi kwenye mazingira haya?

Kwanini hatuwashauri wahanga kukomaa na polisi kuwarejeshea ndugu zao wakiwa hai?

Kwa nini badala yake tunageuka kuwa waandishi wa habari? Au ni yale ya kutajifutia mileage tu?

Nini mchango wetu kuona ubazazi huu kutoka kwa watu tuliowaajiri unakoma taslimu (forth with)?
Umeongea point sana hii nchi mpaka yafanyike Mapinduzi ndio Hawa mbwa tuwaweke kati na hakuna kuwasamehe
 
Naona jambazi linakomaa lisiuawe, lirudishwe likiwa Hai.

Miye siyo jambazi lakini nami nikisema naliona polisi uaji la Mara likikomaa na kuomba mno Mungu Ili hili nalo kupita, utasemaje?

IMG_20221001_023903_471.jpg

Au wewe ni yule kigogo wa Mara aliyeaandaa maandamano feki eti kuungwa mkono?

Believe me - hatupoi!
 
Hivi ile kauli ya Mkuu wa Mkoa ya kuwaambia wazazi wasipowaona watoto wao nyumbani wakawatafute hospitali isipotenguliwa maana yake inaendelea kutumika mpaka sasa, hii maana yake tujiandae kusikia taarifa zaidi za watuhumiwa kuuliwa wakiwa mikononi mwa polisi.

Kiongozi mwenye dhamana kubwa kwa mkoa wako, kuamua kuwaua kinyume cha sheria wale uliotakiwa kuwaongoza, hili halikubaliki, huyu alitakiwa kujiuzulu au kuondolewa kabisa ofisini na mkuu wake, bahati mbaya hakuna kinachofanyika na maumivu kwa watuhumiwa yatazidi.
 
Umeongea point sana hii nchi mpaka yafanyike Mapinduzi ndio Hawa mbwa tuwaweke kati na hakuna kuwasamehe

Kabla ya mapinduzi yapo yaliyopo mikononi mwetu yanayoweza kufanyika na kuwafanya watawala kuwa serious na kujua wajibu wao.

Bila hivyo ni hawa utaowaona walioko busy: kama vipaumbele:

IMG_20221001_070807_035.jpg
 
Binafsi nalipongeza sana jeshi la Polisi kwa moto wanaoutembeza kwa wezi na vibaka

SAFI SANA IGP,,,, WASHA MOTO ENDELEZA MOTO ILI SISI RAIA WEMA TUISHI KWA AMANI
 
Hakuna haki ambayo huwa inakuja yenyewe tu bali hufuatwa na mwenye haki pasipo kuangalia atakutana na madhira yepi

Ukondoo huu tulionao ulianza kumea taratibu 2015 na 2017 ulistawi maradufu. Tumebaki kuwa tunatema nyongo zetu kwenye keyboard tu . Unasikitisha saana na inauma saana tunazidiwa na mzee HAMZA yeye aliona hawezi kuona haki yake inachezewa tuliona alichofanya.

Hata sisi Leo Kwa haki yoyote tunapaswa kuifuata ,ikiwa wao wamefanikiwa kuitisha maandamano ya kupongeza tunafeli wapi sisi kuitisha maandamano yasiyo na ukoma . Tunazidiwa na wanawake kweli wa Iran kichekesho .
 
Lisemeeni na suala la panyaroad

Tulisemee mara ngapi ndugu? Tumeanza kulisemea hilo hata kabla ya operation hii:

Dar: Panya road wavamia nyumba 24, wanne wajeruhiwa

Kwani hata hili likaota na likamea kuwa tatizo polisi walikuwa wapi?

Hivyo wewe:

Ungali hujui kinachogomba ni kuwaua watuhumiwa kinyume cha sheria?

Ungali hujui ni kazi ya polisi kuzuia uhalifu, kuwakamata wahalifu na kuwapeleka kunakohusika?

Ugali hujui uharamia au mauaji kinyume cha sheria ni haramu hata kama yamefanywa na polisi?

Kwa hakika kama nchi tungali na safari ndefu sana.
 
Hukumu ya muhalifu ni kifo, police wanawajua wahalifu wote. Mganga uwajua wachawi wote wa mtaa
 
Kama panya road na majambazi sawa tu wapigwe chuma ila upande wa pili kuna kituo cha police nina bifu nao naogopa wasije Chukulia hii advantage ya panya road wakanipiga chuma bila hatia

Tofautisha panya road na majambazi upade mmoja na "watuhumiwa" wa u panya road na ujambazi kwa upande mwingine.

Nani anayemthibitisha jambazi au panya road? Ni hao ulio na bifu nao?
 
Hukumu ya muhalifu ni kifo, police wanawajua wahalifu wote. Mganga uwajua wachawi wote wa mtaa

Hukumu ya kifo ni kwa mujibu wa sheria ipi na ya wapi?

Polisi wanawajua wahalifu wote kwa mujibu wa nani, sheria ipi au ya wapi?

Kwani polisi ni malaika?

IMG_20220928_193111_561.jpg
 
Polisi wanatuchukulia poa sana. Hawajui waajiri wao ni sisi.

Catherine Ruge anaeleweka vyema kuwa suala la kuzika halipo na halitakuwapo.

"Ingekuwa muafaka zaidi polisi kufahamishwa kuwarejesha watuhumiwa hai kama walivyowachukua."

Haiwezekani wajue kuuwa tu na si kurudisha uhai walioutoa kwa makusudi!

Ninakazia, wasije wakathubutu kwetu. Kwani kwa hakika patachimbika wala hakitakuwa cha mtoto.

Kwamba walimchukua mzima?Nakwenda vipibkulipa gharama zipi za "monchwari" (kama anavyokuita Abdul Nondo)? Monchwari ipi hiyo kwanza? Ninalipa vipi nauli ya polisi yupi?

NInamzika vipi marehemu aliyeuwawa na polisi kwenye mazingira haya?

Kwanini hatuwashauri wahanga kukomaa na polisi kuwarejeshea ndugu zao wakiwa hai?

Kwa nini badala yake tunageuka kuwa waandishi wa habari? Au ni yale ya kutajifutia mileage tu?

Nini mchango wetu kuona ubazazi huu kutoka kwa watu tuliowaajiri unakoma taslimu (forth with)?
Tunaomba police warudishe panya road wakiwa Mochwari
 
Hukumu ya kifo ni kwa mujibu wa sheria ipi na ya wapi?

Polisi wanawajua wahalifu wote kwa mujibu wa nani, sheria ipi au ya wapi?

Kwani polisi ni malaika?

View attachment 2373394
Sheria ya jamii, wahalifu ujulikana kama muhalifu ashafanya police ni sebuleni ashaingia kituo kimoja mara 20 anaenda achiwa na hakimu sababu wenye kesi hawatokei.
Jiulize kwann wahalifu wakikamatwa na raia salama yao ni uona ni kupelekwa police. Muhalifu inatakiwa atenganishwe na Jamii Ili wengine wajifunze kuacha uhalifu. Thus bunduki ndio njia pekee inayoweza ishape Jamii na sio sheria. Sheria ni pesa au ujanja wako wa kucheza na maneno.
 
Ipo wazi kabisa kuna wema watakufa kwa kutokufuatwa kwa sheria. Sheria inatangazwa kuvunjwa hadharani na walinda sheria wenyewe hii ni hatari kwa ustawi wa taifa.

Mimi ni hayo tu.
 
Hili si tulishaliongelea mkuu tukaona labda lahitaji malaika?

IMG_20221001_084439_472.jpg
 
Ipo wazi kabisa kuna wema watakufa kwa kutokufuatwa kwa sheria. Sheria inatangazwa kuvunjwa hadharani na walinda sheria wenyewe hii ni hatari kwa ustawi wa taifa.

Mimi ni hayo tu.

Tunao wajibu na uwezo wa kuhakikisha sheria hazivunjwi. Huo ndiyo ulio msingi wa hoja.

Hatuwezi kuendelea kuona uharamia wa awaye yote nasi tukanyamaza tu kama vifaranga vya kuku?
 
Hukumu ya kifo ni kwa mujibu wa sheria ipi na ya wapi?

Polisi wanawajua wahalifu wote kwa mujibu wa nani, sheria ipi au ya wapi?

Kwani polisi ni malaika?

View attachment 2373394

kwani mahakamani kuna malaika!!!au kuna Mungu??si hawa hawa amajaji wanaopora uchaguzi au umeshasahau??
 
Back
Top Bottom