- Thread starter
- #81
Kumbuka Polisi hawatetei Mali zao wanatetea Mali za watu wengine.
Kuua mtu Kwa ajili ya Mali ya mtu Mwingine sio jambo Dogo.
Panya rodi ni kikundi kilichoundwa na haliwezi kikawa kimeundwa na wajinga wanaotoka mate mdomoni. Kuna watu nyuma yake . Kama Wewe kweli ni raia mwema usishabikie Hawa wahalifu wanaotengenezwa kimkakati. Kumbuka kabla ya JPM kuingia madarakani Nini kilikua kimeanza. Watu walianza kuandamana kutoa watu kwenye vituo vya polisi.baadae wakaanza kuchoma vituo moto then wakanza kupora polisi silaha, mwishowe wakawa wanaua polisi .Kwa Siku Moja polisi wanauawa wanne. Walianza Kwa kujifanya wanatetea Haki za binadamu lakini nyuma palikua na agenda za kigaidi na kudhoofisha serikali Kwa kulidhoofisha Jeshi la polisi na kuwatia hofu. Wanaoumia no Raia wema wasiojihusisha na mambo ya madaraka na Siasa za madaraka.
Hakuna Nchi iliyoko serious kulinda amani na usalama wake inawaza kuwaangalia watu wanaunda vikundi vya kihalifu Kwa kutumia silaha. Majeshi YETU yanawajibu Wa kulinda amani na usalama Wa watu Kwa namna yoyote Ile. Ndio MAANA Dunia kote bajeti Kubwa ni za Majeshi na ni Kwa ajili ya kununua silaha za kuua watu wanaojaribu kuvuruga amani na usalama Wa Nchi husika .
Rwanda hakuna mchezo na Wahalifu ,na wanasiasa wanaoleta chokochoko ni kufutilia MBALI . Nchi imetulia kama Uswisi.
Kuwapora na kuwauwa wafanya biashara wa madini Ifakara hakuwezi kuitwa polisi kulinda mali zao.
Kumpora na kumwua mfanya biashara wa madini Mtwara hakuwezi kuitwa polisi kulinda mali zake.
Kumpora Hamza madini yake hakuwezi kuitwa polisi kulinda mali zake.
Kumshambulia Lissu kwa lengo la kumwua hakuwezi kuitwa polisi kulinda mali zake.
Mifano haina mwisho.
Polisi ipo kwa mujibu wa sheria. Ufanyaji kazi wake ni kwa mujibu wa sheria.
Police brutality na extra judicial killings siyo sehemu ya utendaji kazi wa polisi.
Kupambana na uhalifu kihalifu hakukubaliki
Usilinganishe Uswisi na shithole countries za bwana trump ndugu.