Tuwakumbuke waandishi wetu wa Riwaya

Tuwakumbuke waandishi wetu wa Riwaya

Mkuu salama? Mkuu mmi ni ngonjwa wako maana wewe una dawa ya ugonjwa wangu. VITABU ambavyo unawaza kupata sasa ili nikumbushie enzi jamani plse help
 
Mzimu wa Watu wa Kale, Kisiwa cha Giningi, Duniani Kuna Watu, Siri ya Sifuri, Mke Mmoja Watume Watatu, Mwana wa Yungi Hulewa, By Muhammed Said Abdulla

Mwana jamvi hicho ni "Kisima cha ginigi" nakirafuta sana nijikumbushe nilikisoma 90-91....sijui nitakipata wapi?
 
Bila kusahau vitabu vya ushairi kama:
-AKILIMALI snow white
-SAADAN KANDORO

Unanikumbusha malumbano ya babu yangu marehemu Mkadaru na mzee Mandevu Hamduni "Tandiboi amezidi"....hapa walikuwa mabingwa wa ushairi na kughani
 
Dadi Athumani katunga vitabu vitamu kama 1. MAPUTO 2. OPERESHENI VIPUSA. Msisahau vitabu kama: Mirathi ya Hatari, Njozi Iliyopotea,Pandu, Akuanzae Mmalize, Mbigili Tupu,Bwana na Bibi Myombekere, Kamlete,Akibisha Mlipue, Mashimo ya Mfalme Suleiman, Najisikia kuua tena, Mashetani, Nchi ya Wazuvendi, Miradi Bubu ya Wazalendo, Janga sugu la Wazawa, Harusi, Asali Chungu,Sitaki Sijavunja ungo, Kuli, Kasri la Mwinyi Fuadi, n.k.

Kwa babu yangu Dadi.....mambo ya Nnteko Vano, na "sitaki sijavunja"...ha ha haa jomba likashikwa eti hilo ziwa au chuchu angalia la shangazi lako moja lapata nanasi.....hii haifutiki abadan!
 
Wakuu, kuna kitabu nilisoma nikiwa std 3 miaka hiyo ya 80, kinaitwa NTEKO VANO MAPUTO ingawa sikukimaliza. Natamani nikitafute. Mtunzi alikuwa nani jamani?
Enzi zetu Sekondari za private hazikuwa deal kabisa kama hukufaulu kwenda shule ya Serikali ulilazimika wazazi wafoji ili urudie, siku hizi sekondari za private zinatafutwa kwa mamilioni!
Nashangaa eti siku hizi mtu anafaulu mtihani std 7 hajui kusoma wala kuandika. Watoto wa siku hizi wana bahati!

Mtunzi ni Dadi Athumani, kitabu "Operesheni Vipusa"
 
Mtunzi ni Dadi Athumani, kitabu "Operesheni Vipusa"

Asante Mkuu, enzi tamu sana zile, sijui kama kitabu hiki ki aweza kupatikana nyakati hizi maana hakikuwa maarufu sana kama vitabu vya Allan Qutarman na vile vya Elvis Musiba.
 
Kuna kitabu kinaitwa MBUTOLWE MWANA WA UMMA kiliandikwa na Murray William Kanyama Chiume-1973 nlikua nakipenda sana
 
Kati ya vitabu vyote vilivyotajwa kuna hiki hakijatajwa cha "wauza madawa ya kulevya hunyongewa hapa" sijui mwandishi ni Ganzel na hiki cha ukombozi wa kusi..dah nilivipenda japo kurasa zingine zilikuwa zimepotea.
 
Kuna vitabu kama
Hatia
Utengano
Harusi
Kichwa maji
Kuli
Kiu ya haki .... Vipo vingi mno ila sijui waandishi teh
 
Pepo Za Mabwege
Adili Na Nduguze
Mrithi Wa Baba Ana Radhi
Mashimo Ya Mfalme Sulemani
Kaptura La Max
Pesa Zako Zinanuka
Duka La Kava
Karibu Ndani
Siri Ya Sufuri
Mzimu Wa Watu Wa Kale
Kisima Cha Giningi
Funke Bugebuge
Rosa Mistika
Kuli
 
TUTARUDI NA ROHO ZETU , PESA ZAKO ZINANUKA, DAR ES SALAAM USIKU ,SIMU YA KIFO nk mwandishi BEN R MTOBWA
 
Wadau, siku hizi moyo wa kusoma vitabu vya aina zote-vya Taaluma na Riwaya umepungua sana na imepelekea Watunzi wa Riwaya kutoandika tena vitabu. Leo nawakumbuka baadhi ya Waandishi/ Watunzi wa Riwaya wa Tanzania.

Hamie Rajab
1. Miujiza ya Mlima Kolelo
2. Dunia Hadaa

S.M.Bawji
1. Usiku wa Blaa
2. Kisiwa cha Mayuku

Hamie Rajab_sanda ya jambazi, kamlete akibisha mlipue , gubu la wifi nk.
 
Pepo Za Mabwege
Adili Na Nduguze
Mrithi Wa Baba Ana Radhi
Mashimo Ya Mfalme Sulemani
Kaptura La Max
Pesa Zako Zinanuka
Duka La Kava
Karibu Ndani
Siri Ya Sufuri
Mzimu Wa Watu Wa Kale
Kisima Cha Giningi
Funke Bugebuge
Rosa Mistika
Kuli

Pesa zako zinanuka by Ben R Mtobwa ni bonge la riwaya nilisoma miaka ya 80,ukisoma unaweza mumwaga mchozi.
 
Back
Top Bottom