Tuwakumbuke waandishi wetu wa Riwaya

Jamani namkumbuka saana
Shafi Adam Shafi na vitabu vyake vifuatavyo

1.Vuta N'kuvute

2.Nyota Ya Rehema

3.Kasri Ya Mwinyi Fuad

4.Kuli

5.Mbali Na Nyumbani : hiki amekitunga hivi karibuni ni kitabu kizuri saaana
 
Daaah hivyo vitabu vya kale hata Siku hizi havipatikani. ...Kama Simu ya kifo,sigara yenye sumu, mashahidi wa shetani, tutarudi na roho zetu... na zawadi ya Ushindi.. Daaah...wapi navipata Kwa DSM
 
Musiba, ganzel Duh vyuma hivyo hammie rajab nae anakwambia sanda ya jambazi unakutana na malik mbowe
 
Dah! nafurahi jitihada zangu za kukusanya vitabu inazidi kufanikiwa.
baada ya kuipata vitabu vya alfu lela ulela cha kwanza hadi cha nane, vya Shafi A. Shafi vitano, Shaabani Robert sita, Allan Quarterman viwili, Ben mtobwa Saba, juzi kati nimepata Unyama wa Mafia cha Zahir Ally Zorro, Jamaa hodari kisiwani, kisiwa cha hazina, safari za gulivers, oliver twist, na kubwa lao NJAMA cha marehemu A.E. Musiba.

bado navisaka na kununua. maktaba yangu inazidi kunawiri.
 

Mkuu nitapata wapi Alfu lela ulela? Nisaidie pliiz
 
Mkuu nitapata wapi Alfu lela ulela? Nisaidie pliiz
Kuna maduka ya vitabu hapo posta mtaa samora kwenye mzunguko wa sanamu ya Bismin karibu na benki ya posta. nemulo
 
Last edited by a moderator:
John Rutayisingwa- Neema Mpaka kaburini- Naomba mtu yeyote anayefahamu nitakapozipata riwaya za huyu muandishi jamani. Alifariki akiwa bado kijana na alikuwa muandishi mzuri sana.
Mwingine jaani Hassan Katalambula RP)-Huyu akua mbunifsana ata alikuwa n vijaria vya hadithi napicha.
 
Asante mkuu, umemaliza... Mengine ni madogo madogo tu
 
Jamani namkumbuka saana
Shafi Adam Shafi na vitabu vyake vifuatavyo

1.Vuta N'kuvute

2.Nyota Ya Rehema

3.Kasri Ya Mwinyi Fuad

4.Kuli

5.Mbali Na Nyumbani : hiki amekitunga hivi karibuni ni kitabu kizuri saaana

Nyota ya Rehema sio yeye. Shafi vitabu vyake vyote nnavyo plus hicho Mbali na nyumbani nshajinunulia nalala yangu. Kizuri sana. Lkn Kitabu chake cha Haini ndo my favourite
 

Dah. Itabidi tupange urafiki mkuu, maana mie natumia sana pesa kwenye kununua vitabu. Na zaidi napenda sana vya waandishi wa zamani.

Lugha wanayotumia ni adhimu sana.
 
nipo moshi nawezaje kupata ''msako wa hayawani''
 
Mkuu nitapata wapi Alfu lela ulela? Nisaidie pliiz

Kama upo Moshi Vijijini kuna sehemu inaitwa MWIKA KUSINI(eneo la BIBLE) kuna Maktaba ya Jamii ipo Alfu Lela Ulela kuanzia 1 na zaid ya 10
 
Riwaya zipo nyingi;
1.Maisha yangu na Baada ya Miaka 50(S.Robert)
2.PESA ZA MAWE
3.KISIKI KIKAVU
4.MOTO WA MIANZI
5.LILA NA FILA
6.MWISHO WA MAPENZI
7.SAFARI ZA MUHAMED EL MURJEB(Tipp Tippu)
8.MARIMBA YA MAJALIWA
9.PESA ZAKO ZINANUKA
10.ROSA MISTIKA
11.WACHAWI WA WAAFRIKA
12.MFADHILI
13.SIMU YA KIFO
14.BARUA NDEFU KAMA HII n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…