Tuwakumbuke watu waliotupokea na kutupa njia za kuishi hapa DSM

Tuwakumbuke watu waliotupokea na kutupa njia za kuishi hapa DSM

DR HAYA LAND

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2017
Posts
23,928
Reaction score
63,499
Kwa Mara ya kwanza nilipofika hapa Dsm nilifikia kwa Uncle wangu ni Askari yeye na mke wake.

Nakumbuka nilikaa pale wiki tatu tu lakini niliziona Kama Mwaka mzima .

Asikuambie Mtu yule uncle wangu ndo alinifundisha kumjua Mungu na kunipeleka Shule Hadi kufika Chuo

Mungu Ampe Maisha marefu Sana huyu Uncle wangu ili siku moja ile ndoto yangu ya kununulia lambogini itimie.
 
nilipokelewa na mtoto wa kaka yangu mwaka 2012

akanikopa 250,000 mwaka 2015 akaja kunilipa baada ya miaka 7.

wakati namdai alidai hawezi kunilipa kwa sababu nilikaa kwake miezi miwili bure😓😓😓 so hio ndio gharama za kuishi kwake (wakati huo ananisalimia kabisa ba mdogo😅😅😅)

Any way maisha yana mengi ya kutufundisha
 
Nimekumbuka mbali.
Mwenyeji wangu tulipanga tuonane Ubungo stendi lakini nilipofika hakupokea simu.

Nikapambana kivingine hadi sasa nipo Dar es Salaam ni mwenyeji kila mtaa.
 
Inapendeza, ngoja waje kutoa shuhuda zao...
 
Back
Top Bottom