MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Wakuu leo nimeamka na kujikuta nikitafakari sana kuhusu mambo ya kifamilia hass yanahusu Baba na Mama. Nikiwaweka kwenye mizani ni kuwa Mama anapewa uzito mkubwa kuliko Baba. Kila upande wa hii dunia jina la Mama linatajwa mno. Ni sahihi kabisa. Kina Mama wana uzito mkubwa kwenye maisha yetu. Nani kama Mama? Hakuna. Ila kuna jambo nitafafanua kwa lugha nyepesi ya kuweza kueleweka hata na wafuasi wa Mbowe.
Ila mimi kama mtu aliyebarikiwa akili nyingi kuna kitu nimekiona kwa kina mama kama udhaifu. Nimepitia pia maandiko matakatifu na kujiridhisha kuwa huu ni udhaifu wa mama zetu. USHAURI. Kina mama wengi wanatoa ushauri kwa hisia badala ya facts. Na watu wengi waliofuata shauri za mama zao kama walivyopewa walijikuta matatizoni. Kina mama wengi wamesababisha watoto wawachukie baba zao kwa kuwashauri ujinga.
Hii hapa ni mifano ya kina mama kwenye biblia waliotoa ushauri wa hovyo.
1. Hawa - stori ya mama yetu inapatikana kwenye kitabu cha Mwanzo sura ya 3. Lile tunda alilompa Baba yetu Adamu limeleta majanga. Alipaswa kupuuzwa.
3. Sara - mama yetu mke wa Nabii Abrahamu alimshauri mumewe atembee na kijakazi (Housegirl) baada ya yeye kutoweza kushika mimba kwa miaka mingi. Lakini mara baada ya yeye kupata mtoto uzeeni akaanza kumchukia babymama wa Nabii na kuropoka kuwa mtoto wa housegirl hatapata urithi. Hii kauli ilimkasirisha sana Nabii Abrahamu.
3. Rebeka - huyu mke wa Isaka. Mwanzo 27 ina stori nzima jinsi alivyomfanya mwanae Yakobo (Israel) kuiba baraka za kaka yake Esau kutoka kwa baba yao Isaka. Inasemekana ndo chanzo cha taifa la Israel kuwa taifa lililolaanika hadi leo.
4. Malkia Yezebeli - soma kitabu cha Wafalme jinsi Yezebeli alivyomshawishi mfalme Ahabu kuachana na imani yake na kuanza kuabudu miungu ya kwao Yezebeli.
5. Mke wa Ayubu alimropokea Ayubu kuwa amkufuru Mungu. Bahati nzuri Ayubu alikataa.
6. Malkia Herodia - kuna siku Mfalme Herode alikuwa na sherehe ambapo binti yake alicheza muziki mbele yake na kumfurahisha sana mfalme. Herode akiwa na furaha akamwambia bintiye achague zawadi yoyote atampatia. Binti akaenda kwa mama yake kuomba ushauri kwa mama yake na kuishia kuambiwa aseme anataka kichwa cha Yohana mbatizaji kwenye bakuli. Hii ilimhuzunisha hata Herode ila kwa sababu alishaahidi ikabidi mtu atumwe gerezani kuleta kichwa cha Yohana. Yohana Mbatizaji alizikwa bila kichwa. Soma Mathayo 14.