Tuwapuuze CHADEMA na suala la Katiba mpya, wana ajenda ya siri

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Nawasalimu katika jina la Chama cha Mapinduzi. Kwa pamoja mjibu Chama kiendelee.

Nimeona leo niweke hili suala la katiba sawa ili kusaidia wajinga wengi wasioelewa na kuishia kuchotwa kijinga na Chama Cha Mbowe (CHADEMA).

Siku za hivi karibuni kumekuwa na kuhamasishana huko upande wa upinzani kutaka katiba mpya kwa maana iliyopo haifai. Kwa haraka haraka waweza kudhani wapinzani wana nia njema kumbe hakuna. Nitafafanua bila kutoza gharama yoyote ikiwa kama shukrani kwa mwenyezi kwa hii akili kubwa niliyojaliwa ili kusaidia binadamu wenzangu.

Kabla ya kuongelea CHADEMA na suala lao lazima tukubaliane watanzania wengi hawajasoma hii katiba mpya kujua yaliyomo. Wewe unayesoma hapa kuna ibara gani ya katiba waweza ikumbuka na kilichomo humo? Kwahiyo kabla ya kutaka katiba mpya lazima wawaeleze wafuasi wao kuisoma na kuielewa katiba iliyopo.

Kuwaswaga watu kama mifugo sio sawa. Kwa tunaoifahamu katiba hii iliyopo tunakubali kwamba ina mapungufu mengi hasa kwa nyakati hizi za vyama vingi na mabadiliko mbalimbali duniani. Kama enzi za Nyerere aliona ina mapungufu, je vipi nyakati hizi? Haina ubishi lazima kuna marekebisho yafanyike. Kwa mfano sifa ya mbunge ya kujua kusoma na kuandika imepitwa na wakati. Taifa kwa sasa lina wasomi wengi sana kwahiyo hakuna haja ya kupeleka bungeni watu wasio na elimu. Mifano ni mingi sana ya mapungufu kwenye katiba.

Kwanini tuwapuuze CHADEMA? Tunawapuuza kwasababu nia yao ni kutaka katiba itakayowawezesha kushika madaraka na kunufaisha genge la viongozi wachache na sio kumnufaisha mwananchi. Wakati ule wa mchakato wa kupata katiba mpya kupitia rasimu ya Warioba tuliona jinsi gani viongozi wa CHADEMA walivyoweka maslahi yao mbele kwa kudai serikali tatu kwanza badala ya kurekebisha mambo yanayomgusa mwananchi moja kwa moja.

Serikali tatu ni kumuongezea mwananchi gharama ya kuziendesha. Kwahiyo CHADEMA wanataka mabadiliko kwa manufaa ya viongozi sio wananchi wote. Nawasihi wananchi wote tutafute namna nyingine ya kubadili katiba yetu bila kutumjka na hili genge lenye maslahi binafsi.
 
Kwa hiyo Jaji Warioba, Prof Kabudi, Humphrey Polepole, na wale Wajumbe wote waliozunguka Nchi nzima kukusanya maoni kwenye ile Tume ya Katiba nao ni Chadema!

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete aliyeanzisha huu mchakato nae alikuwa Chadema! Una akili mbovu sana ndugu mheshimiwa.
 
Sijakataa mabadiliko ya CHADEMA.. nimekataa kinachowafanya CHADEMA watake katiba mpya. Wana nia ovu.
 
Itaje hiyo NIA OVu ya Chadema ili tuweze kukuamini. Kinyume na hapo, basi utakuwa imepuyanga sana. Maana Katiba ni hitaji la Watanzania wengi, na hasa baada ya hii Katiba ya ccm ya mwaka 1977, ku prove failure katika masuala mengi.
 
Katiba mpya siyo takwa wala hisani ya mtu au chama chochote cha siasa bali ni takwa la jamii - "social need" ambalo halizuiliki. Kama wewe hutaki kwa sababu zako, wengi wengine wanataka kwa sababu zao. Mimi nikiwa sehemu ya wahitaji wa "social product" hii ; ninapayuka tena: KATIBA MPYAA!!!!?
 
Inabidi moderators waanze kufanya appraisals kabla ya kuachia uzi ufike kwa mlaji. Yaani huyu mtu apa atajikuta kwamba ametanua mawazo kumbe ametanua makalio mpaka tigopesa yake inaonekana alafu ndio think-tank [emoji1787][emoji1787]
 
Nawasalimu katika jina la Chama Cha Mapinduzi. Kwa pamoja mjibu Chama kiendelee.

Nimeona leo niweke hili suala la katiba sawa ili kusaidia wajinga wengi wasioelewa na kuishia kuchotwa kijinga na Chama Cha Mbowe (Chadema).

Siku za hivi karibuni kumekuwa na kuhamasishana huko upande wa upinzani kutaka katiba mpya kwa maana iliyopo haifai. Kwa haraka haraka waweza kudhani wapinzani wana nia njema kumbe hakuna. Nitafafanua bila kutoza gharama yoyote ikiwa kama shukrani kwa mwenyezi kwa hii akili kubwa niliyojaliwa ili kusaidia binadamu wenzangu.

Kabla ya kuongelea CHADEMA na suala lao lazima tukubaliane watanzania wengi hawajasoma hii katiba mpya kujua yaliyomo. Wewe unayesoma hapa kuna ibara gani ya katiba waweza ikumbuka na kilichomo humo? Kwahiyo kabla ya kutaka katiba mpya lazima wawaeleze wafuasi wao kuisoma na kuielewa katiba iliyopo.

Kuwaswaga watu kama mifugo sio sawa. Kwa tunaoifahamu katiba hii iliyopo tunakubali kwamba ina mapungufu mengi hasa kwa nyakati hizi za vyama vingi na mabadiliko mbalimbali duniani. Kama enzi za Nyerere aliona ina mapungufu, je vipi nyakati hizi? Haina ubishi lazima kuna marekebisho yafanyike. Kwa mfano sifa ya mbunge ya kujua kusoma na kuandika imepitwa na wakati. Taifa kwa sasa lina wasomi wengi sana kwahiyo hakuna haja ya kupeleka bungeni watu wasio na elimu. Mifano ni mingi sana ya mapungufu kwenye katiba.

Kwanini tuwapuuze CHADEMA? Tunawapuuza kwasababu nia yao ni kutaka katiba itakayowawezesha kushika madaraka na kunufaisha genge la viongozi wachache na sio kumnufaisha mwananchi. Wakati ule wa mchakato wa kupata katiba mpya kupitia rasimu ya Warioba tuliona jinsi gani viongozi wa CHADEMA walivyoweka maslahi yao mbele kwa kudai serikali tatu kwanza badala ya kurekebisha mambo yanayomgusa mwananchi moja kwa moja.

Serikali tatu ni kumuongezea mwananchi gharama ya kuziendesha. Kwahiyo CHADEMA wanataka mabadiliko kwa manufaa ya viongozi sio wananchi wote. Nawasihi wananchi wote tutafute namna nyingine ya kubadili katiba yetu bila kutumjka na hili genge lenye maslahi binafsi.

Mkuu hivi unajua kuwa:

1. Katiba iliyopo haiwawajibishi baadhi ya watendaji wakuu kwa kuikiuka, na hii ni kwa mujibu wa katiba yenyewe?
2. kwa katiba iliyopo pana watu hata kama wakiiba, wakipora, wakiuwa, wakidhulumu nk hiyo ni halali kwa mujibu wa katiba yenyewe?
3. katiba iliyopo inawapa baadhi ya watu mamlaka ya kujifanyia lolote bila kuhojiwa au hata kuwajibishwa tu?
4. Katiba iliyopo haitoi haki sawa kwa watu wote ndani ya nchi?
5. Kuna mianya mingi katika katiba hii ambayo imeweza kuifanya mihimili mingine hata kupoteza uhuru wake wa kiutendaji kwa mujibu wa katiba yenyewe?
6. Kuna utitiri wa nafasi za uongozi wasio na tija wala ridhaa ya wananchi ambao pia ni mzigo mkubwa kwa mlipa kodi?
7. Kuna rundo kubwa la vigogo wasio na tija na wasiolipa kodi wenye uhalali tokea katika katiba yenyewe?
8. Nk, nk.

Bado unadhani hayo yanawagusa wanachadema tu?

Bado hudhani kuwa yote ya namna hiyo yanapaswa kupatiwa ufumbuzi pasipo na kuchelewa sasa, kwa kuyashughulikia ipasavyo kwenye katiba mpya?
 
Tunawapuuza kwa sababu waliharibu mchakato wa rasimu ya katiba iliyokuwa inajibu mambo mengi kama tume huru ya uchaguzi nk.kwa ubinafsi na tamaa ya uongozi.Wakaanzisha UKAWA umoja wa katiba ya wananchi badala ya kupambania katiba wakaigeuza kuwa chama cha siasa baada ya kumchukua lowassa CCM..halafu viongozi wale wale wanapiga kelele katiba mpya???No.inatakiwa viongozi nyuma ya hili waondolewe kwenye uongozi wa kisiasa halafu hao Ukawa waombe kurudi kwenye bunge la katiba ili kupiga kura kupitisha rasimu ili ipelekwe kwa wananchi kupigiwa kura
 
.........Kwa tunaoifahamu katiba hii iliyopo tunakubali kwamba ina mapungufu mengi hasa kwa nyakati hizi za vyama vingi na mabadiliko mbalimbali duniani. Kama enzi za Nyerere aliona ina mapungufu, je vipi nyakati hizi? Haina ubishi lazima kuna marekebisho yafanyike. Kwa mfano sifa ya mbunge ya kujua kusoma na kuandika imepitwa na wakati. Taifa kwa sasa lina wasomi wengi sana kwahiyo hakuna haja ya kupeleka bungeni watu wasio na elimu. Mifano ni mingi sana ya mapungufu kwenye katiba.
Haya ni maneno yako mtoa mada?

Hivi unaelewa unachokiandika lakini?
 
Back
Top Bottom