Kwa hiyo woga wako ni kwamba ikipatikana Katiba mpya, CCM inaweza kutolewa madarakani au siyo!
Kwa maana nyingine ni kwamba kwa Katiba ya sasa hakuna namna ya kuitoa CCM madarakani au siyo!
Kwa mantiki hiyo unataka Katiba ya sasa iendelee kwa sababu inailinda CCM kutoachia madaraka au siyo!
Kwa hiyo Katiba yoyote itakayotoa haki sawa kwa vyama vyote vya siasa nchini haifai na haitakiwi au siyo!
Kwa hiyo Katiba inayotakiwa ni ambayo itatoa upendeleo maalum kwa CCM kubaki madarakani asilani!
Kwa hiyo Katiba yoyote itakayotoa mwanya kwa chama chochote nje CCM kutwaa madaraka si ruhusa!
Kwa hiyo kama mwana CCM umelazimika kuanzisha uzi huu kama njia mojawapo ya kufikisha ujumbe maalum.
Swali...kwa kuwa JF ni jukwaa huru na mtu yeyote anaweza akajiunga, ujumbe huu unataka kuufikisha kwa nani? Wana CCM, Wapinzani au Watanzania? Je ujumbe wako ni ushauri, onyo, tahadhari, ombi, pendekezo, agizo au amri na walengwa ni akina nani?
Nadhani nikikuita mjinga nitakuwa nakuonea...wewe ni mpumbavu, period!